"Kwa hiyo kwa mantiki hii unaweza kuanza kujenga hoja kuwa baadhi ya wale waliofanya uamuzi unaoonekana unaenda kinyume au na maadili ya uongozi, au unapingana na masilahi ya umma, walitafakari kuwa njia rahisi ya kurahisisha mipango yao ni kumuondoa huyu mzee mapema. Hiyo unaweza kusema, lakini haitakuwa sahihi kufanya hivyo bila kuwa na ushahidi. Nimewahi kusikia tuhuma kuwa Rais Kikwete anatuhumiwa kuwa ndiye mtu aliyetumwa na nchi za Magharibi kukimaliza Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nilivyosikia tuhuma hizi niliona kichekesho, lakini ukiangalia baadhi ya matukio katika uongozi wake ambayo yanaweza kuashiria hoja hiyo, unaweza kuyapata. Enzi za Mwalimu Nyerere waliotuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya uongozi waliitwa pembeni na kuambiwa wajiuzulu. Miaka ya hivi karibuni wale ambao walikabiliwa na tuhuma za aina hiyo waliombwa kutafakari wao wenyewe uamuzi sahihi wa kuchukua.
Habari hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la JAMHURI
Source: wavuti.com - wavuti
Kamanda huyu mtu alishakufa na tukamzika,vyovyote vile iwavyo kuanza kuchokonoa alikufakufaje ni hatari nyingine,tunaanza kukaribisha matatizo haki ya mungu kwenye nji hii,achana kabisa na hiyo kitu kamanda wangu,wewe unajua kabisa kwamba ni Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya nchi hii halafu unaweka thread kama hii!!!
Halafu kama hwa watu sio wa kuwafuata unajua baadhi yao wanonekana kuchoka na maisha ndiyo maana usiku kucha wanafanya kazi ya kufikiria ni namna gani wanaweza kutuchangisha ili tutwangane.
Yaya bhabha lekaga.
huo uchunguzi utatumia hela zipi, kodi za wananchi au msaada kutoka nje!!!!
Itashangaza kweli; Sababu Wakati Anafariki Rais wa Nchi alikuwa Mwanafunzi Wake? Ndie aliyempigia DEBE awe Rais;Sasa kama ni hakumtakia HALI NZURI YA MATIBATU au HOSPITALI BORA ya KANSA kama vile MAYO CLINIC, USA Mmm...
Ndie aliye UZA MAKAMPUNI YOTE ya SERIKALI; Ndie aliyesaini MIKATABA isiyo na Manufaa ya MADINI nchini; Ndie nayemiliki Majengo Mengi na Nyumba za Zamani za SERIKALI... Na Anaongea KIINGEREZA KIZURI!!!
Nnuoo7,
unaonekana kuwa na ujumbe mzuri lkn sijakuelewa ndg yng.hv unataka kutupatia ujumbe gani hapa?
"""Nimewahi kusikia tuhuma kuwa Rais Kikwete anatuhumiwa kuwa ndiye mtu aliyetumwa na nchi za Magharibi kukimaliza Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nilivyosikia tuhuma hizi niliona kichekesho, lakini ukiangalia baadhi ya matukio katika uongozi wake ambayo yanaweza kuashiria hoja hiyo, unaweza kuyapata""
Aisee!! This is very serious