Utata wa kifo cha Mwalimu Julius K. Nyerere: Siri zaidi zafichuka

Utata wa kifo cha Mwalimu Julius K. Nyerere: Siri zaidi zafichuka

Jasusi,

Kwa maoni yako hii imekaaje. Nitumie hata PM.

"Za-mia",

Unataka na mimi nimwombe views zake kwenye PM? Ungeacha wazi ili aweke hapa sebuleni wote tusome. Jasusi ni mdau wa huko kwa hiyo nina uhakika anaweza kuwa na info za ziada.

Kama nitafika mwisho wa huu uzi bila kuona maoni ya Jasusi basi itabidi niombe hayo maoni aliyokuandikia u-fwd kwangu kwa idhini yake lakini na ninajua hawezi kukataa.
 
Zakumi,
Mbona unaniweka pagumu?

Ninachojua kwa uhakika ni kwamba kuna watu walisherehekea kifo cha Mwalimu na miongoni mwao akiwemo Mkapa na mkewe ambao walifungua chupa ya champagne Ikulu. Kuhusu Dakta Mwakyusa ama ni uzembe, jeuri au dharau lakini hakumhudumia Mwalimu ipasavyo. Alikuwa anakwenda Butiama anamwona Mwalimu na kurudi siku hiyo hiyo DSM.

Mwalimu kwanza alipimwa leukemia New York, na kwa akili zangu, matibabu ya kufuatilia yangefanyika New York na wala si Uingereza. Wakati huo Marekani ilikuwa advanced katika research ya leukemia kuliko Uingereza na dakta Mwakyusa, ambaye alifuatana na Mwalimu New York mara kwa mara, alilijua hilo au alipaswa kujua. Halafu ile St. Thomas ni general hospital wakati Mwalimu alihitaji specialized hospital. Halafu muda mwingi alipokuwa London Mwalimu alikaa hoteli mpaka alipozimia ndio wakamkimbizi St. Thomas. Kwa hiyo kuna maswali mengi tu ambayo yanahitaji majibu.

In short, Mwalimu did not get the best treatement he needed. Hebu jiulize, yule mwandishi habari wa Mkapa Nkurlu, (rip) alipougua walitaka kumpeleka London akakataa kuwa asipelekwe St. Thomas. Alijua kitu gani ambacho sisi hatukijui?
 
Zakumi,
Mbona unaniweka pagumu? Ninachojua kwa uhakika ni kwamba kuna watu walisherehekea kifo cha Mwalimu na miongoni mwao akiwemo Mkapa na mkewe ambao walifungua chupa ya champagne Ikulu. Kuhusu Dakta Mwakyusa ama ni uzembe, jeuri au dharau lakini hakumhudumia Mwalimu ipasavyo. Alikuwa anakwenda Butiama anamwona Mwalimu na kurudi siku hiyo hiyo DSM. Mwalimu kwanza alipimwa leukemia New York, na kwa akili zangu, matibabu ya kufuatilia yangefanyika New York na wala si Uingereza. Wakati huo Marekani ilikuwa advanced katika research ya leukemia kuliko Uingereza na dakta Mwakyusa, ambaye alifuatana na Mwalimu New York mara kwa mara, alilijua hilo au alipaswa kujua. Halafu ile St. Thomas ni general hospital wakati Mwalimu alihitaji specialized hospital. Halafu muda mwingi alipokuwa London Mwalimu alikaa hoteli mpaka alipozimia ndio wakamkimbizi St. Thomas. Kwa hiyo kuna maswali mengi tu ambayo yanahitaji majibu.

Kwa maelezo haya na maswali haya ni dhambi kuu kujaribu kufifisha mjadala huu.....

Nitoe wito kwa wazelendo wenye weledi katika taaluma ya intelijensia, popote pale walipo watupe mchango wao....

Waunganishe hizi dots ili hatimaye haki itendeke juu ya wote walioshiriki ubaradhuri huu....

Kwamba mwisho ninachosema ni kuwa kufungwa kwa mjadala huu kutupe mwanga wa kufungua kile "nini kifanyike"

Na tusitegemee serikali hii au yeyote ya magamba au hata itakayowekwa na majasusi kwamba itatenda haki... hapana..

Hili ni jukumu la kizalendo ambalo lazima lichukuliwe kwa gharama kubwa sana na lazima iwe nje ya mfumo "rasmi" wa kushughurikia haki...

Mtu anayetembea na damu ya Baba wa Taifa kwenye mifuko yake haki yake ni kipande cha chuma ndani ya ubongo.. period!!
 
The "Pandora box" effect, Mkapa amejiongezea maadui wengi zaidi,maybe ni vyema afikri kuhusu more security.
 
Mwaka 1997 Mwalimu akisherehekea siku yake ya kuzaliwa (alipofikisha umri wa miaka 75) pale Diamond Jubilee hall alisema hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya na kwamba alivyokuwa anajisikia hakuwa na wasi wasi wowote kuushuhudia uchaguzi wa mwaka 2000. Alitoa mfano wa mama yake mzazi ambaye pamoja na kuwa na miaka zaidi ya 100 alikuwa bado yuko fit, hivyo Mwalimu hakuwa na mashaka yoyote kuhusu afya yake.

Tukirudi nyuma kidogo, baada ya kutembea karibu Tanzania nzima akimnadi mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo, Mkapa, Mwalimu alianza kuuona upande huo wa Mkapa uliojificha na kuanza kuushtukia. Hivyo alianza kuukosoa uongozi wake hadharani na kutamka kuwa hakubaliani kabisa na mpango wa Mkapa kuuza kila kitu kilichokuwa mali ya Umma kama vile havina wenyewe.

Mwaka moja baadaye, 1998 Mwalimu alianza kujisikia vibaya na hivyo kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam alipokuwa Marekani. Katika uchunguzi huo ndipo waliugundua ugonjwa na, pamoja na tiba ya awali, wakamshauri afanye mipango ya kurudi Marekani kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Kilichowashangaza ni kulikoni? Mwalimu mwaka moja kabla hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya!

Mwalimu hakurudi Marekani na badala yake Mkapa aliamua apelekwe London na ni Mkapa mwenyewe anajua sababu za kuamua hivyo. Maswali yapo na wahusika bado wapo na ni haki ya Watanzania kuufahamu ukweli. Binafsi nafurahi sana kwa Mkapa kuropoka ovyo alipokuwa Arumeru, bila hivyo ukweli kuhusu kifo cha Mwalimu labda ungezikwa kama alivyozikwa lakini hadi lini?
 
Tufike mahali tibadili mwelekeo wa siasa zetu. We cant always bank on conspiracy theories. Umaarufu wa kisiasa sasa uje kwa kutegemea utawasaidiaje watanzania kuondokana na umaskini na utawaleteaje maendeleo. Kuumbuana kisiasa tumefanya sana we now need a different tune. Mambo ya siokoine aliuwawa, ooh xy kapewa sumu, ooh bcd amelogwa haitusaidii na tumechoka.
This is not a conspiracy theory. Believe me.
 
"Za-mia",

Unataka na mimi nimwombe views zake kwenye PM? Ungeacha wazi ili aweke hapa sebuleni wote tusome. Jasusi ni mdau wa huko kwa hiyo nina uhakika anaweza kuwa na info za ziada.

Kama nitafika mwisho wa huu uzi bila kuona maoni ya Jasusi basi itabidi niombe hayo maoni aliyokuandikia u-fwd kwangu kwa idhini yake lakini na ninajua hawezi kukataa.

Keil,

Naona ametusikia. Hii ni issue serious na mtu anayeweza kunishawishi kuwa something was wrong kuhusiana na kifo ni Jasusi.
 
hivi mtu umetawala nchi miaka 25 halafu unashindwa kujenga hata hospitali ya kukutibu wewe mwenyewe na bado watu wanawalaumu watu wengine!!! nyerere alikufa kifo cha kawaida kama watz kwa vile hatuma huduma nzuri za afya.Ujamaa wake ndo unatufanya leo tunatafuta mchawi kwenye kila idara ya serikali..miundombinu,elimu,AFYA n.k
 
Zakumi,
Mbona unaniweka pagumu? Ninachojua kwa uhakika ni kwamba kuna watu walisherehekea kifo cha Mwalimu na miongoni mwao akiwemo Mkapa na mkewe ambao walifungua chupa ya champagne Ikulu. Kuhusu Dakta Mwakyusa ama ni uzembe, jeuri au dharau lakini hakumhudumia Mwalimu ipasavyo. Alikuwa anakwenda Butiama anamwona Mwalimu na kurudi siku hiyo hiyo DSM. Mwalimu kwanza alipimwa leukemia New York, na kwa akili zangu, matibabu ya kufuatilia yangefanyika New York na wala si Uingereza. Wakati huo Marekani ilikuwa advanced katika research ya leukemia kuliko Uingereza na dakta Mwakyusa, ambaye alifuatana na Mwalimu New York mara kwa mara, alilijua hilo au alipaswa kujua. Halafu ile St. Thomas ni general hospital wakati Mwalimu alihitaji specialized hospital. Halafu muda mwingi alipokuwa London Mwalimu alikaa hoteli mpaka alipozimia ndio wakamkimbizi St. Thomas. Kwa hiyo kuna maswali mengi tu ambayo yanahitaji majibu.
In short, Mwalimu did not get the best treatement he needed. Hebu jiulize, yule mwandishi habari wa Mkapa Nkurlu, (rip) alipougua walitaka kumpeleka London akakataa kuwa asipelekwe St. Thomas. Alijua kitu gani ambacho sisi hatukijui?

Jasusi,

Samahani kwa kukuingiza kwenye suala hili na nashukuru kwa mchango wako. Kuna mambo mengi yanapita kichwani lakini ngoja niishie hapa.

Z-10.
 
hivi mtu umetawala nchi miaka 25 halafu unashindwa kujenga hata hospitali ya kukutibu wewe mwenyewe na bado watu wanawalaumu watu wengine!!! nyerere alikufa kifo cha kawaida kama watz kwa vile hatuma huduma nzuri za afya.Ujamaa wake ndo unatufanya leo tunatafuta mchawi kwenye kila idara ya serikali..miundombinu,elimu,AFYA n.k

Bambo,

Mimi ni mmoja ya watu wanaomlaumu siasa za Nyerere. Lakini kwa ugonjwa wake, ni nchi chache zilizo na capabilities za kuutibu.
 
hivi mtu umetawala nchi miaka 25 halafu unashindwa kujenga hata hospitali ya kukutibu wewe mwenyewe na bado watu wanawalaumu watu wengine!!! nyerere alikufa kifo cha kawaida kama watz kwa vile hatuma huduma nzuri za afya.Ujamaa wake ndo unatufanya leo tunatafuta mchawi kwenye kila idara ya serikali..miundombinu,elimu,AFYA n.k

Bambo,

Kuna wengi hawautaki ukweli kuwa chanzo ya matatizo yote Tanzania ni Nyerere. Alikuwa hajui alifanyalo na haambiliki.
 
* Ndugu walitaka apelekwe China, Mkapa akagoma
* Profesa Mwakyusa alimtelekeza, Gachuma akajitosa
* Mazingira ya kutia mashaka yaelezwa, hali inatisha

Na Waandishi Wetu, Musoma

Baada ya Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), kumtaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa aeleze kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kilitokana na nini, ndugu mwingine ameibuka na kuishutumu Serikali ya Mkapa kuwa ilimtesa Mwalimu Nyerere kwa kutompa matibabu ya uhakika kutoka kwa daktari wake, Profesa David Mwakyusa.

Ndugu huyo aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema Profesa Mwakyusa, hakupata kwenda kijijini Butiama kumtibu Mwalimu wakati akiumwa, badala yake alimtumia daktari mmoja aliyetajwa kwa jina la Malima, kumtibu Mwalimu Nyerere. Dk. Malima anatajwa kuwa mmoja wa madaktari waliopendwa mno na Mwalimu na wakazi wengi wa Butiama.

“Mwalimu aliugua, hali ikawa mbaya, Profesa Mwakyusa hakupata kwenda Butiama kumtibu, badala yake akawa anamtumia Dk. Malima. Alikuwa akitibu kwa kutumia simu. Huyu ndiye mtu ambaye tunaweza kusema alimsaidia Mwalimu kuongeza siku za kuishi.

“Dk. Mwakyusa alienda Butiama siku alipoambiwa hali ya Mwalimu inazidi kuwa mbaya, ndipo akapanda ndege, wakaja wakamchukua na kwenda naye Dar es Salaam.

“Lakini wakati huo mfanyabiashara, Christopher Gachuma, alishakwenda kumjulia hali Mwalimu. Akamkuta anataabika kweli kweli. Nakumbuka nilikuwapo na Gachuma alilia machozi. Akamweleza Mwalimu, ‘naomba Mwalimu nikupeleke Nairobi ukatibiwe’. Mwalimu akakataa kata kata, akasema; "kama hawataki... hawa hawataki kunitibu niache nifie hapa hapa nyumbani kwangu". Gachuma alimbembeleza sana, lakini Mwalimu alikataa,” amesema ndugu huyo.

Ndugu huyo amesema kwamba siku chache baadaye, walimu wawili waliomfundisha Mwalimu Nyerere - Mwalimu James Irenge na Mwalimu Kirigini - walifika nyumbani kwa Mwalimu, Mwitongo kumjulia hali mwanafunzi wao (Mwalimu Nyerere).

“Nakumbuka siku hiyo walikwenda moja kwa moja hadi chumbani. Wakakuta Mwalimu anateseka kwa maumivu makali. Walimu wale walilia machozi. Wakamwuliza Mwalimu kuhusu matibabu, akawajibu kuwa mipango inafanywa apelekwe Uingereza. Wakakataa wakisema huko ni hatari, bora apelekwe China,” amesema ndugu huyo.

Mwalimu Kirigini alifariki dunia miezi kadhaa baada ya Mwalimu Nyerere kufariki dunia.

JAMHURI lilipowasiliana na Gachuma, alisema yeye alitoa wazo la kumpatia matibabu baada ya kukuta yupo kitandani anaumwa, na yeye kama Mjumbe wa NEC alikuwa na wajibu wa kumjulia hali kiongozi wake.

“Nilikwenda kumuona, alikuwa anaumwa. Kimsingi nilichomwambia nikasema Mwalimu kuliko kukaa hapa nyumbani ni bora ukatafuta 'second opinion' ya madaktari, akaniambia tayari serikali imekwishamfanyia 'appointment' ya kumpeleka nje,” alisema Gachuma na kuongeza:

“Alikuwa kitandani anaumwa, ila baada ya siku moja au mbili nilipotoka pale [nyumbani kwa mwalimu] ndipo alipopelekwa nje ya nchi.”

Jamhuri ilipowasiliana na Profesa Mwakyusa aliyekuwa daktari binafsi wa Mwalimu Nyerere kwa njia ya simu jana, lakini baada ya salamu mambo yalienda hivi:

Mwandishi: Profesa baadhi ya wanafamilia ya Mwalimu Nyerere wanasema ulimtelekeza baba yao, ulikuwa humpi matibabu inavyostahili.

Prof. Mwakyusa: Sikusikii vizuri, naongea na nani?

Mwandishi: Profesa naitwa Balile

Prof. Mwakyusa: Unasemaje? Nipo kwenye gari Ruvu sikusikii.

Baada ya kusema hivyo, Mwandishi alimtumia ujumbe (SMS) huu: “Profesa shikamoo. Naitwa Deodatus Balile, Mhariri Mtendaji wa gazeti la JAMHURI. Muda mrefu nakutafuta. Tumepata taarifa kutoka familia ya Mwalimu Nyerere na wanasema wakati Mwalimu anaumwa ulimtelekeza ukawa unamtuma Dk. Malima badala ya kumtibu wewe kama daktari wake. Unasemaje? Asante.”

Ujumbe huo ulionyesha kumfikia, na mwandishi alipompigia tena simu baada ya muda akapokea simu, na hata kabla ya kuitikia akasema: “Nipo kwenye gari sikusikii vizuri… naongea na nani?” kisha akaiacha simu hewani huku zikiwapo sauti za matangazo ya mpira kuashiria alikuwa karibu na redio iliyofunguliwa sauti ya juu.

Kwa upande wake Dk. Malima, simu yake ilipokewa na mtoto, aliyeikimbiza kwa mtu mwingine aliyezungumza kwa sauti ya kike na kusema; “Bado yuko hospitalini.” Alipoulizwa angerejea nyumbani saa ngapi, mtu huyo alisema hajui. Baada ya muda siku ilizimwa.

Mwalimu wa Mwalimu Nyerere azungumza

Baada ya kauli ya Mbunge Nyerere kumtaka Mzee Mkapa aeleze chanzo cha kifo cha Mwalimu, Mwalimu Irenge amejitokeza na kusema amefurahishwa mno kusikia kuwa amepatikana kiongozi jasiri wa kuhoji namna Mwalimu alivyougua hadi kufariki dunia.

“Mfikishieni pongezi nyingi Mbunge Nyerere... huyo mtoto amefanya jambo la maana sana kuuliza jambo hili, miaka yote nalia kwa sababu naamini Mwalimu aliuawa.

“Kwa kuwa suala hili limeulizwa hadharani, sasa nipo radhi kufa. Nikifa nitakwenda moyo wangu ukiwa na furaha kwa sababu nimekuwa nikijiuliza ni nani anayeweza kuhoji namna Mwalimu… mwanafunzi wangu alivyokufa,” amesema Mwalimu Irenge mwenye umri wa miaka zaidi ya 120.

Mwalimu Irenge alianza kumfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge kuanzia mwaka 1934 hadi 1936. Alistaafu kazi mwaka 1977. Tangu wakati huo anaishi jirani na shule hiyo. Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Mwalimu Irenge alihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na kusema binafsi hakuafiki Mwalimu kupelekwa kutibiwa nchini Uingereza.

Alisema alipinga kwa sababu alijua Waingereza si marafiki wa kweli wa Mwalimu kwa kuwa aliongoza harakati za kuwang’oa katika Tanganyika na katika mataifa mengine, hasa Afrika Kusini na Zimbabwe ambako Serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikiunga mkono utawala wa kidhalimu wa Wazungu wachache.

Vincent Nyerere amkomalia Mkapa

Mbunge wa Musoma Mjini, Nyerere (Chadema), ametetea uamuzi wake wa kumtaka Rais (mstaafu) Mkapa aeleze mazingira ya kifo cha Mwalimu Nyerere, akisema ni Watanzania wengi ambao wamekuwa wakitaka kupata majibu hayo.

Katika mahojiano maalumu na JAMHURI yaliyofanyika Arumeru mkoani Arusha, Nyerere amesema Watanzania wanachotaka ni majibu ya swali alilomwuliza Mkapa.

“Hapa hakuna ugomvi kama baadhi ya watu wanavyodhani, nilichofanya ni kuuliza swali, sasa ni wajibu wa Mkapa na wanaohusika kutoa majibu, tena majibu yanayojitosheleza. Kama Mzee Mkapa amekuwa akidanganya kwa miaka mingi, ajue sasa wananchi wanataka majibu, na mimi nimeanza kuingiwa na shaka juu ya uadilifu na ukweli wa Mzee Mkapa.

“Kwenye msiba wa baba yangu Josephat Kiboko Nyerere, ndiye aliyenikabidhi ubani, sasa anaposema hanijui, hii inanipa shaka juu ya ukweli wa yale ambayo mara zote ameyasimamia,” amesema Nyerere.

Amekiri kuwa kaka yake, Joseph Butiku amempigia simu na kumtaka ‘amwache’ Mzee Mkapa.

“Butiku ni kaka yangu, amenipigia simu, lakini nashukuru kwamba ametambua kuwa nilichofanya kwanza ni kujibu uongo uliotolewa jukwaani, kwamba mimi sina uhusiano na familia ya Baba wa Taifa. Mimi Mwalimu ni baba yangu mkubwa… huo ndiyo ukweli hata kama Mkapa anataka au hataki.

“Butiku akaniambia kuwa kama nilichokozwa nilikuwa na haki ya kujitetea. Kwa kweli nilichofanya ni kujitetea maana kama Watanzania wangeamini uongo kuwa mimi si wa familia ya Nyerere, hiyo ingeniathiri maana wananchi wasingeniamini. Lakini sasa ukweli umejulikana.

“Uchunguzi wangu umebaini kuwa Mkapa alidanganywa na viongozi wa CCM. Yupo kiongozi alimwambia kuwa Nyerere ni mwiba jukwaani kwa hiyo atafute namna ya kumzima, hasa kwa kuwa anatumia jina la ‘Nyerere’.

“Mzee Mkapa naye bila kujua akaingia kichwa kichwa, baadaye nasikia anasema huo ulikuwa utani. Jukwaani hakuna utani, sisi Chadema hatuna utani, kama wao (CCM) wanafanya utani, sisi hatujui utani,” amesema.

Tendwa naye apigwa kombora

Nyerere alimgeukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, na kumtaka asiingilie masuala ya ukoo, badala yake aendelee na masuala ya vyama.

“Tendwa kasema eti kumzungumzia Baba wa Taifa ni kuhatarisha amani katika taifa. Lakini anajua kuwa mimi nilishambuliwa kwa hiyo nilikuwa na kila sababu ya kujitetea. Yeye ni Msajili wa Vyama vya Siasa, si msajili wa ukoo.

“Kwangu mimi kumzungumzia Mwalimu ni haki kwa sababu zaidi ya kuwa Baba wa Taifa, ni mlezi wangu. Nimesomeshwa kwa kutumia fedha za akaunti maalumu ya Mwalimu katika benki ya NBC. Akitaka kujua aende apitie rekodi za fedha zilivyokuwa zinatolewa ili nilipiwe ada. Hana mamlaka ya kunizuia kumtaja baba yangu mkubwa. Sasa hivi kuna sala maalumu, kwa hiyo anataka hata nisisali hiyo sala ya kumwombea Mwalimu?” Amehoji.

Kwa siku kadhaa sasa, Nyerere ameibua mjadala mkali ndani na nje ya nchi kwa uamuzi wake wa kumtaka Mkapa aeleze ukweli wa kifo cha Mwalimu Nyerere.

Alisema Mkapa hawezi kutamba kuwa ni miongoni mwa watu wanaomuenzi Mwalimu, kwa vile baada ya kushika madaraka alihakikisha anauza viwanda na mashirika yote ya umma, vitu vilivyoasisiwa na Mwalimu.

Alitoa mfano wa Benki ya NBC iliyokuwa ya umma ambayo Mkapa aliiuza kwa bei ya kutupa kwa makaburu wa Afrika Kusini. Mwalimu aliongoza harakati za kuzuia kuuzwa kwa benki hiyo, na hadi anafariki dunia alikuwa ‘haelewani’ na Mkapa juu kuuzwa kwa benki hiyo.

Mashirika ya umma zaidi ya 400 yaliyoachwa na Mwalimu yaliuzwa chini ya uongozi wa Mkapa wa miaka 10.

Wagonjwa wanaopelekwa China ndio hawafi? Hivi si kila binadamu ni mortal!
 
pamoja na kuhusika na kifo cha mwalimu hainiingii akilini kwamba ben alikuwa pekee yake kuna wale waliokuwa wanafanya safari za kwenda london kumwona kila mara na yule aliyeambiwa akahakikishe kama kweli kafa .mzee ngombale. nao walijua ni nini kinaendelea.
 
The "Pandora box" effect, Mkapa amejiongezea maadui wengi zaidi,maybe ni vyema afikri kuhusu more security.
Hivi Mkapa anaweza akawa na Security kuliko Rais wa Marekani!!??.......to Assassinate Mkapa ni kazi rahisi kuliko kumtongoza Wema Sepetu....
 
tumechoka na habari hizi, sasa walikuwa wapi kusema hayo enzi hizo wanasema leo wakati Nyerere amefariki, inasaidia nini sasa??? Nyerere ndo atafufuka??/

bongo bana watu wanajitafutia umaarufu kwa vitu vya ajabu ajabu sana?? wangetoa taarifa hizo mapema not now?

wewe ndo mpumbavu kabisa! kwani wangesema mapema mwalimu angefufuka, kikubwa jambo kama ni la kweli na watuhumiwa wapo watoe majibu, ningekuona wa maana kama ungesema walichelewa kuyasema mapema hayo mpaka watuhumiwa wote wamekufa. acha ujinga wewe kama unaishi kwa kutegemea hao wauji siku zenu unahesabika!!
 
wajinga tupo wengi kweli, hatutaki haki itendeke kwa vile tu muda umepita na aliyekufa harudi, hivi mtu akimuua baba yako, kaka yako au nduguyo yeyote wa karibu utasema mwacheni aendelee na sgughuli zake maana mfu hafufuki? utumbo mwingine haupaswi kabisa kusemwa mbele za watu. yapasa tujipime vuwezo kwanza kabla ya kutoa hoja yeyote. tafadhali

hivi kwa akili yako wewe haki gani unayoitafuta hapo, mkapa afungwe au anyongwe???? au umejisikia kuropoka?? vitu vingine inabidi tuwe tunafikiri kabla ya kuandika, eti haki,,,haki gani nao hao kina nyerere wadogo walioibuka sasa walikuwa wapi sikuzote kama sio njaaa tupu na kutaka umaarufu...

remember ' kama utatoa information/idea/suggestions while its too late then work done is equal to zero' because will be your idea will be useless
 
Bambo,

Kuna wengi hawautaki ukweli kuwa chanzo ya matatizo yote Tanzania ni Nyerere. Alikuwa hajui alifanyalo na haambiliki.
Watanzania bwana..na hiyo ina maana bado tunasafari ndeefu sana,kama kuna watu ambao wengine na elimu zao hizo kidogo za mlimani bado hawaelewi mortality triggers za nchi yetu.wanaingia kwenye mabishano kama haya..je huko vijijini hao wanaosingiziana uchawi mtasemaje maana kila siku watu wanadai wanauawa na ndugu zao..Tatizo hatuna huduma nzuri za afya ambazo zitafanya magonjwa kujulikana mapema na kuanza kuyatibu kwa wakati...tulikuwa na sera mbovu sana wakati wa nyerere na matokeo yake ndio haya..elimu nusunusu na kuwa nyuma kwa kila kitu..
 
wewe ndo mpumbavu kabisa! kwani wangesema mapema mwalimu angefufuka, kikubwa jambo kama ni la kweli na watuhumiwa wapo watoe majibu, ningekuona wa maana kama ungesema walichelewa kuyasema mapema hayo mpaka watuhumiwa wote wamekufa. acha ujinga wewe kama unaishi kwa kutegemea hao wauji siku zenu unahesabika!!

duuu haya sitaki ligi na wewe, ur so smart kaka!! big up uko sahihi
 
Back
Top Bottom