Sumba-Wanga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 5,353
- 1,236
Mwaka huu ni aibu ya kishindo!
Mwaka huu ni aibu ya kishindo!
Manumba kama unasoma haya mambo hebu launch criminal investigation ili tujue kama kuna uzembe katika kumuhudumia Mwalimu na waliohusika wachukuliwe hatua. Hasa kinara wao Mkapa
hata kama hizi taarifa zingetolewa tareh 15/10/1999, bado zisingeweza kurejesha uhai wa mwalimu nyerere, therefore waache wana ukoo bado wana uchungu na kifo cha baba yao ambaye wana amini kifo chake kilikua na utata mkubwa, na wew kama mwanataifa hili pia una haki japo ya kujua kiongozi wako aliekutafutia uhuru wa taifa lako ameishia wapi na ameishia ishia je???tumechoka na habari hizi, sasa walikuwa wapi kusema hayo enzi hizo wanasema leo wakati Nyerere amefariki, inasaidia nini sasa??? Nyerere ndo atafufuka??/
bongo bana watu wanajitafutia umaarufu kwa vitu vya ajabu ajabu sana?? wangetoa taarifa hizo
mapema not now?
Tunahitaji uchunguzi huru na siyo wa Manumba, hapa tunahitaji chombo kama Scotland Yard na huyu Mmakonde wa Msumbiji akithibitika alishiriki kwenye mauaji ya Baba wa Taifa naye anyongwe hadi kifo. porojo nyingine hazihitajiki hapa.hata kama hizi taarifa zingetolewa tareh 15/10/1999, bado zisingeweza kurejesha uhai wa mwalimu nyerere, therefore waache wana ukoo bado wana uchungu na kifo cha baba yao ambaye wana amini kifo chake kilikua na utata mkubwa, na wew kama mwanataifa hili pia una haki japo ya kujua kiongozi wako aliekutafutia uhuru wa taifa lako ameishia wapi na ameishia ishia je???
ni wangu mtazamo
Malimwengu ni sawa kabisa ukweli unauhusiano mkubwa na maendeleo. Tatizo hapa ni ukweli upi unaleta maendeleo. Kwangu mimi nivigumu sana kuujua ukweli unaotoka kwa wanasiasa kwa staili ya kuumbuaana wakati wa kampeni. Kusingekuwa na uhusiano na kuomba kura kidogo ningeelewa lakini kwa staili hii ya kupatia kula tutasikia mengi. Je huu ni uvumi, ukweli, porojo, uongo? umenena vema wenzetu wanatafuata ukweli kwa kutumia technologia je kwetu sisi kutumia tetesi na uvumi huoni tunakiuka kanuni za kisayansi hivo hatuwezi kupata maendeleo ispokuwa kupoteza muda wa kufanya kazi kwa kuendekeza umbeya?ukweli ndio msingi wa kuleta maendeleo unayoyataka, unapoukataa ukweli jua utakaa karne hata kumi bila kupata hayo maendeleo, kama ambavyo huwezi kujenga nyumba bila msingi ndivyo hivyo huwezi kuwa na maendeleo bila ukweli, ndio maana nchi zilizoendelea wanazidi kutumia tekinoljia kutafuta ukweli wa kitu, katika jambo lilijificha uvumbuzi ndipo hutokea
Niliwahi kulihoji hili swala mara nyingi sana ni kwa nini huyu Mmakonde anavaa Bullet proof? je ana maadui gani? sikuwahi kujibiwa, JK pamoja ya kwamba ametuletea maisha magumu mpaka watu wanakula vichwa vya kuku na miguu ya kuku kama mboga ya weekend na watu wazima na akili zao wanashinda majalalani kuokota makopo lakini JK havai Bullet proof. huyu jamaa akiachwa bila kunyongwa basi ziko njia mbadala za kumshughulikia.kwa jins mkapa alivyokua anavaa bullet proof anakua km robot nahisi alikua anaogopa ukweli huu ungejulikana angetandikwa risasi
kweli hii ndo bongo. Tumekuwa tukiambiwa hapa kuwa mwalimu alienda uingereza akiwa mzima wa afya na kurudi marehemu. Leo tunaambiwa alikuwa taabani kabla hata hajaondoka. Aisee!
Hapo ndio unatakiwa kumshukuru Vince Nyerere kwa kuibua hii ishu inaelekea mambo mengi yatajulikana, kama alienda amezidiwa au bukheri wa afya tutajua. Cha muhimu huu mjadala uendelee na ndugu wazidi kufunguka. Dozi ikimkolea Mkapa ataibuka tu na kuomba radhi taifan laana ya kumuua muasisi wa taifa ni mbaya sana. Hebu Jiulize waliomuua Patrice Lumumba iliwachukua miaka mingapi nao kulipa madhambi yao?umeonaee!? Siku zote ukipenda kitu bila kujiuliza umependa kwa ajili gani mwisho wake ni kuwa kipofu wa moyo! Na ni upofu mbaya sana kuliko kitu chochote kile, wasemaji wa hayo ni wale wale, lakini kasoro hiyo hawaioni maadamu tu anayeshambuliwa ni 'magamba' kama ni kweli siku zote alikuwa wapi?
Kweli hii ndo bongo. Tumekuwa tukiambiwa hapa kuwa mwalimu alienda Uingereza akiwa mzima wa afya na kurudi marehemu. Leo tunaambiwa alikuwa taabani kabla hata hajaondoka. Aisee!