Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Hivi ili iitwe siku ni lazima yapite masaa 72? Unaposikia ziara ya Rais flani siku mbili anakuja leo anaondoka kesho huwa yamefika masaa 48?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi naongelea hizi ambazo zinasema atakaa kaburini siku tatu mchana na usiku.

Mathew 12:38-40

38Then some of the Pharisees and teachers of the law said to him, "Teacher, we want to see a miraculous sign from you."39He answered, "A wicked and adulterous generation asks for a miraculous sign! But none will be given it except the sign of the prophet Jonah.40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.
 
Huo utaratibu wa kuhesabu siku kuanzia saa 6 usiku ulianzishwa na Warumi ,haukuwepo wakati wa Yesu
Wewe Nyaigela wewee!
Kwahiyo unataka kusema Bwana Yesu hajawakuta Warumi wakitawala?
Gavana wa Kirumi wa Jimbo la Judea aliyemhukumu Yesu kwa treason alikuwa ni nani kama si Mrumi Ponsio Pilato?
 

Kiongozi umepitia tena hii hoja yako? kama umepitia tena unaona ndio jibu sahihi au umeleta mada mpya yenye kuleta maswali?

twende sawa saa 9 ijumaa mpaka saa 12 jion ya ijumaa ni siku ya kwanza
haya saa 12 jioni ya ijumaa mpaka 12 asubuhi ya jumamosi ni siku ya pili
saa 12 asubuhi ya jumamosi mpaka 12 jioni ni siku ya tatu
haya yesu kafufuka jumapili asubuhi yani kwa jibu lako ni siku ya nne! hata mimi sijui mambo ya biblia ila umenidanganya
 
mkuu nikiongezea kidogo hapa, kwanz akwenye biblia hakuna mfumo wa kuhesabu siku kwa masaa 24, kama tufanyavyo sasa walichokua wanahesabu ni siku yaani jua lichomozapo na kuzama, hivyo Yesu alikufa mchana wa ijumaa saa tisa akashinda mchana wa jumamosi na jumapili asubuhi akafufuka maana yake ni siku ya tatu hivyo asemacho mtoa hoja ni hoja dhaifu kwa msomaji mzuri wa maandiko.
 
Wewe Nyaigela wewee!
Kwahiyo unataka kusema Bwana Yesu hajawakuta Warumi wakitawala?
Gavana wa Kirumi wa Jimbo la Judea aliyemhukumu Yesu kwa treason alikuwa ni nani kama si Mrumi Ponsio Pilato?
Mkuu hujanielewa pamoja na utukutu wangu. Nilichokisema huu utaratibu wa kuhesabu masaa kuanzia saa sita usiku haukuwepo wakati Yesu akisulibiwa. Ulikuja baadaye.
 
Mkuu kama kalugha ka kikoloni kanapanda ,hebu jaribu kusoma Mathayo 12:38-40 . Utaona kabisa Yesu akisema Mausiku matatu na maMchana matatu , kwa hesabu zako hapo hatupati huo muda

38Then some of the Pharisees and teachers of the law said to him, "Teacher, we want to see a miraculous sign from you."39He answered, "A wicked and adulterous generation asks for a miraculous sign! But none will be given it except the sign of the prophet Jonah.40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.
 
Ijumaa Saa 9 Alasiri mpaka saa 5:59:59:99 usiku ni siku moja na usiku mmoja,
Jumamosi Saa 6:00:00:00 usiku mpaka saa 5:59:59:99 usiku ni siku ya pili na usiku wa pili,
Jupili Saa 6:00:00:00 usiku mpaka wakati anafufuka Alfajiri ya jumapili ni siku ya tatu na usiku wa tatu, maandiko hayakutaja masaa yalitaja siku na usiku

Hivo maandiko na maneno ya Yesu yalikua sahihi siku tatu mchana na usiku .
 
pamoja na hilo mzee hoja yangu ipo wazi kabisa so rudia comment yangu vizuri kuelewa uamue mwenyewe
 
Kwa tafsiri yako ya siku 3 Mchana na usiku bado tunarudi pale pale MAKADIRIO.
Yesu alikufa saa 9 alasiri (mchana) akapitisha jumamosi (asubuhi na usiku) Jumapili asubuhi walivyoenda wakakuta kafufuka!, So bado siku 3 zinakamilika unless unataka neglect siku ya kwanza kisa nusu siku lakini saa 9 alasiri mpaka 12 jioni bado kulikuwa ni muda wa jua so ni mchana!.
Luka 23:44-47
Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki.

Tunaona asubuhi wakakuta kafufuka.
Luka:24.1-3
Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.
 
Mambo ya dini waachie wabobezi wakujuze. Maana tunachofanya kwa Sasa Ni adhimisho tu. Mfano: kwenu mtu akizikwa mnasema matanga siku tatu au nne. Huwa mnahesabu VP?

Kama uliwahi kusafiri nje ya nchi unajua hata Kama umefika saa tano usiku wanahesbu siku Mona.....

Cha msingi tambua alikufa na siku ya tatu alifufuka Kama maandika yasemavyo.

Pia sabatho ilikua Ni siku ya Jumamosi lakini kutokana na umuhimu wa ufufuko wa Kristu Jumapili (ambayo ndio siku ya tatu) ilifanywa kuwa ndio siku ya Bwana
 

Alaaaaaaaaa Kumbe hizo ni sikukuu za Kipagani??? kwa hiyo wanaosherehekea hizo sikukuu ni wapagani??. Anyway nashukuru kwa uthibitisho huo.

[ohana10:17-18]
Halafu Tena anamlalamikia Mungu kumwacha???
Marko 15:34-37 Neno: Bibilia Takatifu.
Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Itakuwa hakuwa Yesu!
 
Kaka mtukutu.
Unapoanzisha mjadala jaribu kufungua macho na ubongo upate pia kujifunza upande usioujua. Kuna vitu havihitaji nguvu nyingi kuvitetea. Ubainifu wake kwa wengineo ni maneno machache tu na uchokonozi wa kifikra ili kuzindua!
 
Kaka mtukutu.
Unapoanzisha mjadala jaribu kufungua macho na ubongo upate pia kujifunza upande usioujua. Kuna vitu havihitaji nguvu nyingi kuvitetea. Ubainifu wake kwa wengineo ni maneno machache tu na uchokonozi wa kifikra ili kuzindua!
endelea mkuu nakusikiliza
 
Kwa kweli hizi hesabu za makanisani zinapingana na hesabu zilizoandikwa hii ni hatari kwa afya ya mwanadamu
 
Mkuu maandiko yanasema USIKU na MCHANA kwa mda wa siku 3, kama hakuna USIKU 3. na MCHANA 3 hicho unachoamini ni uongo
 
Maandiko yanataka USIKU 3 na MCHANA 3 , ili siku 3 zikamilike, nnje ya hapo hakuna siku tatu msilazimishe mambo
 
Mkuu hizo siku tatu za kiyahudi za Masaa kuminambili kila moja Turejee kitabu gani?
 
N kweli mkuu walikuwa wanahesabu kwa utaratibu kwamba jua likizama siku inaisha na nyingine inaanza.Kwa hiyo kama alizikwa Ijumaa jioni na kufufuka jumapili asubuhi siku tatu hazifiki
usiwe mzito kuelewa walikuwa wanahesabu siku sio masaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…