Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Mleta mada naona hujui hata ulichokiandika. Ngoja tuanzie hapa.
Soma haya maandiko, kisha tafakari.

TITO 2:13
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.

MATHAYO 28:18
Yesu akaja karibu, akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani"


Kwa kifupi, kwa mujibu ya Biblia na imani ya Kikristo, unapozungumzia Yesu basi ujue unazungumzia Mungu kamili akiwa na nguvu zote na mamlala yote aliyeamua kujivika unyenyekevu na kutwaa mwili wa binadamu ili kutupa udhihirisho wake.
 
Mwambieni The Chosen Liberator atubu kwa kusema uongo. Vinginevyo jehanam inamngoja
Ana-copy na ku-paste maelezo ya chatGPT halafu anasema eti: "Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia."

Ufu 21:8
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Nashukuru kwa mchango wako.

Lakini mkuu - Hayo mamalaka kapewa na nani? Aliyempa siyo kwamba ni mkuu kuliko yeye.
 
Nimetumia chat GPT kupanga hoja zangu - chat GPT isingeweza kujenga hizo hoja bila mimi kutaka - Key point ni yangu.

Jibu hoja usinijibu mimi kwamba napotosha au usijibu jinsi nilivyoijenga hoja.

Kama napotosha leta ukweli wako wa maandiko ili Mungu apate kujifunua ndani yetu.
 
Inashangaza sana ....!!

Kama nyinyi wenyewe hamuwezi kujenga hoja, badala ya kujadiliana - mnashindana nani bora zaidi.

Huyo Mungu wenu hayupo - Si unaona mnavyochanganyana.

Angekuwepo mngeelewana.
 
Bado hamjasema na mtasema tu
 
Jitahidi kuwa mkweli ndugu yangu. Ona sasa chaGPT aliyekuandikia points hizo alivyokugeuka! Amekanusha kichwa chako cha mada na kukuaibisha:

✅ Kanusho:​

Sentensi inayodai kwamba "Utatu ni wa majukumu tu si mamlaka, na kwamba Yesu si mkuu kuliko Baba" ni ya uongo wa kisasa wa teolojia (hasa kutoka kwa wapinga-Uungu au baadhi ya wanatheolojia wa "egalitarian Trinity"). Biblia inafundisha tofauti ya asili na mamlaka kati ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu — ingawa wote ni Mungu mmoja kwa asili.

Kwa hiyo, tunakana wazi:

✘ "Yesu ni Mungu lakini si mkuu kuliko Baba" – si sahihi.
 
Mungu hana umoja.
Hana chama.
Hana kikundii cha viungu.
Mnavyotaka kusema kuna mungu mkubwa,kuna kadogo na kuna kadogo dogo zaidi.

Inamana na mbinguni atakuwepo mama yao na shangazi
aisee!
 
Kabla hujawatukana waislamu,pambana kwanza na sintofahamu ya kumjua Mungu wa kweli,maana ukristo hauna maelezo yenye kuridhisha na akili ikakinai

Ndio maana nyie wenyewe wala hamumjui yupi ni mungu wa kweli?
 
Sasa umefanya nini? Umekosoa mimi kutumia chatGPT na kusema imenidanganya kisha umejibu kwa kutumia hiyohiyo chatGPT - je, haijakudanganya kama ulivyodai imenidanganya?


Mkuu weka pembeni majivuno ya kwamba wewe ndiye mjuvi sana kuliko wengine kisha tujadili hoja kwa upendo - Sasa ungekuwa mchungaji ungeweza kuwa na hekima ya kujadili na mtu kama mimi kama lengo lako ni kupinga si kufundisha?


Pita 1wakholintho1:13 ujifunze sifa za upendo - kisha lete hoja sio kupinga kwa kutumia teolojia ambazo ni mafundisho ya kibinadamu - tetea hoja kwa neno sio maneno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…