Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Mungu ni cheo ambacho kimetokea baada ya Neno kufanya uumbaji Malaika na viumbe wengine kabla uumbaji kufanyika kulikuwa hakuna Mungu kwa sababu cheo Cha Mungu kina demand ibada
MUNGU Nİ MMOJA. ILA HUJIFUNUA KULINGANA NA WAKATI NA UTENDAJI WAKE. TUNAMUOMBA MUNGU KWA JINA LA YESU ABARIKI CHAKULA LAKINI TUNAPOKULA TUNAKULA NA ROHO WAKE.
 
Nimefanya hivyo makusudi ili kukuonyesha kuwa chatGPT sio ya kuaminika. Kama unahitaji kuijua kweli ya Mungu, usiitegemee 100%. Mada yako ungeiandika kwa mtindo wa swali ningeshiriki kuijadili. Lakini umeanza kwa kujivuna kwamba hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wako wa kina wa biblia wakati ume-copy na ku-paste mambo usiyokuwa na uhakika nayo.
 
Kabla hujawatukana waislamu,pambana kwanza na sintofahamu ya kumjua Mungu wa kweli,maana ukristo hauna maelezo yenye kuridhisha na akili ikakinai

Ndio maana nyie wenyewe wala hamumjui yupi ni mungu wa kweli?
Mimi ninayo maelezo kamili kuhusu ukristo ....injili ni sahihi mbona hata mudi boy kakili kuhusu injili ambayo ndiyo ukristo ..tatizo lililopo ni kujua injili ya kweli isiyo chakachuliwa ambayp mimi naijua ...uislamu ndiyo upuuzi ulio dhahiri kabisa ....nimeuliza hapa jf waislamu wote maswali mnashindwa,kunijibu ...nimeuliza SHETANI IBILISI YULE ALIYE LAANIWA LAANA YA MILELE NI DINI GANI? sijajibiwa
 
Sijaona mahala Yesu amesema yeye ni Roho kama ulivuodai bali alisema atamuacha roho kama msaidizi.

Yesu atakuwaje roho wakati roho ndiyo anakaa ndani yake.
Yohana 14:16-19
[16]Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

[17]ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

[18]Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

[19]Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.



Ulimwengu haumuoni sasa hivi sio hautamuona atakapokunaa.
Ila nyinyi mnamuona na anakaa kwenu sasa hivi.

Siwaachi yatima.mm na ndie ninaerudi
 
JF ni ukumbi wa wazi kwa wanachama wote.

Kama unataka mada exclusive kwa watu fulani tengeneza website yako.
Uko sahihi lakini kwa mtu mwenye hekima si kila mada inamhusu kuchangia.

Mfano mimi si mpenzi wa michezo - hivyo mada za michezo nabaki mtazamaji.
 
Kufanya uchambuzi wa kina - deep think siyo kujivuna bali kujivuna ingetokea pale ningesema mimi ninajua kufikiri kwa usahihi - Ndiyo maana mwisho nimesema njoo tujadili [Unajua maana ya kujadili] - huoni uzi umekaa mfumo wa debate?

Kwanini unalazimisha uzi uwe kwenye mfumo wa swali - kwani nyuzi zako zote umeandika kwa mfumo wa swali?

Kama unadai kwamba mtu akitumia chatGPT kupangilia hoja zake haswa za imani - huwa inatabia ya kupotosha bhasi nimekuelewa katika hilo.

Hivyo ninakuomba uwaite Mods wafute nyuzi zako zote humu mana wewe 90% huandika kwa kutumia chatGPT - vipi kama haikupi majibu accurate?

"Toa kwanza boriti iliyo ndani la jicho lako kisha sasa ndipo utakiona kijiti ndani ya jicho langu".

Unashindwa kufundisha unachokiamini ili watu wafunuliwe bali umekazania kuonyesha mimi nina mapungufu - Wewe ni mnafiki mtumishi wa Mungu.

Na kama ukibaki na kiburi chako cha ubishi na kukosoa badala ya kufundisha kwa neno la kweli bhasi ni dhahiri utakua unajiaibisha na sitakuwa tayari kujadili na mtu wa hisia.
 
u're totally wrong!
 
Issue ni kwamba umeanza mada yako kwa kusema uongo. Huo sio uchambuzi wako. Baada ya kukubana kwamba umetumia chatGPT ndio unasema imekusaidia kupangilia hoja. Mbona hukusema hivyo tangu mwanzo? Ulitaka ujionyeshe kuwa unajua. Hayo ndiyo majivuno.

Kama kukuambia umesema uongo ndio kiburi basi ni dhahiri Maandiko huyajui..
 
DR Mambo Jambo karibu utie neno hapa.
Mkuu wangu Vishu!
Hili swala la Homoiusios (ὁμοιούσιος) na Heteroiousios (ἑτεροούσιος) Halikuanza Debate Leo Tangu enzi Zile za Arian Controversy..

Mkuu Nitatia Neno Leo Mida saa Nane au tisa Saa Za Afrika Mashariki Baada ya Kumtumikia Kaisari ila Kifupi Ni Kwamba Ubishi Huu Ulichukua Miaka zaid ya 200 Na Uliamuliwa Kwa Kura za Maoni Ukiongozwa na Constantine..

Kiufupi Uungu wa Yesu ni Mjadala Tangu NiCea mpaka Constantinople..
Nitakuja
 
Karibu sana pasi na kukosa..
 
Mbona nimekujibu,nenda kwenye ule uzi kacheki
 
Kabla hujawatukana waislamu,pambana kwanza na sintofahamu ya kumjua Mungu wa kweli,maana ukristo hauna maelezo yenye kuridhisha na akili ikakinai

Ndio maana nyie wenyewe wala hamumjui yupi ni mungu wa kweli?
Mimi ninayo maelezo kamili kuhusu ukristo ....injili ni sahihi mbona hata mudi boy kakili kuhusu injili ambayo ndiyo ukristo ..tatizo lililopo ni kujua injili ya kweli isiyo chakachuliwa ambayp mimi naijua ...uislamu ndiyo upuuzi ulio dhahiri kabisa ....nimeuliza hapa jf waislamu wote maswali mnashindwa,kunijibu ...nimeuliza SHETANI IBILISI YULE ALIYE LAANIWA LAANA YA MILELE NI DINI GANI? sijajibi
Mbona nimekujibu,nenda kwenye ule uzi kacheki
Weka jibu tena mbona unaogopa ...shetani ibilisi ni dini gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…