Utawala wa Samia ni Fundisho tosha kwa Nchi Namna ya kuchagua Makamu wa Rais

Utawala wa Samia ni Fundisho tosha kwa Nchi Namna ya kuchagua Makamu wa Rais

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Kujifunza kutokana na Makosa ndo huku sasa. Hatukutegemea Rais kufa akiwa madarakani. Makamu wa Rais huwa anateuliwa ilimradi ni mtu tu.

Sasa kama Katiba haitabadilishwa japo iseme kwamba

1. Rais akifariki madarakani uchaguzi mkuu ufanyike baada ya siku kama 90 hivi

2. Rais na Makamu wake wote wapigiwe kura siyo mmoja kupita kwa mgongo wa mwenzie

Basi tofauti na hapo tuna safari ndefu sana. Kwa Katiba ya sasa ya kurithi madaraka Makamu wa Rais anapochaguliwa lazima wazingatie haya..

1. Makamu wa Rais hatakiwi kutoka Zanzibar

2. Makamu wa Rais awe na uwezo mkubwa wa kiuongozi sawa na Rais au zaidi.

3. Rais na Makamu wake lazima wawe na Maono sawa isifike mahali mmoja amburuze mwenzake waelewane.
 
Katiba ibadilishwe,

1. Uwepo wa waziri mkuu na makamu wa raisi kwa wakati mmoja kwa nchi masikini namna hii ni upotevu wa rasilimali.

2. Raisi akifariki makamu/waziri mkuu akamate nchi na kuitisha uchaguzi mkuu ndani ya siku 90.

3. Serikali ziwe tatu, kwa muungano huu haijulikani Tanganyika iko wapi. Vyetu vinaliwa tu na wenzetu, vyao hawaruhusu vitoke.
 
Kujifunza kutokana na Makosa ndo huku sasa. Hatukutegemea Raisi kufa akiwa madarakani.. Makanu wa Raisi huwa anateuliwa imradi ni mtu tu.

Sasa kama Katiba haitabadilishwa japo iseme kwamba

1. Raisi akifariki madarakani uchaguzi mkuu ufanyike baada ya siku kama 90 hivi .
2. Raisi na Makamu wake wote wapigiwe kura siyo .mmoja kupita kwa mgongo wa mwenzie

Basi tofauti na hapo tuna safari ndefu sana. Kwa katiba ya sasa ya kurisi madaraka makamu wa Raisi anapochaguliwa lazima wazingatie haya..

1. Makanu wa Raisi hatakiwi kutoka Zanzibar
2. Makamu wa Raisi awe na uwezo mkubwa wa kiuongozi sawa na Raisi au zaidi.

3. Raisi na makamu wake lazima wawe na Maono sawa isifike mahali mmoja amburuze mwenzake waelewane.

4. Raisi na Makamu wake lazima wawe wanaume. Hatujafika level ya kuongozwa na Raisi Mwanamke tupo wachanga sana
🤣Mi naona hoja ya mwanamke ni finyu Sana. Msiangalie jinsi angalieni urais. Kwani hamna wanaume ambao wamezingua. Hoja sio mwanamke, tusiwe hivi Jamani ubaguzi utazidi
 
Suala la Rais na makamu kuwa na uwezo sawa kiuongozi halipendwi na CCM. Rejea JK na Lowasa. Edo alitaka popularity kumzidi bosi akajikuta ametemèshwa ndoano
 
Oky sawa elezea japo kidogo tuone Uzuri wake

Achilia mbali Uzuri wa sura
Mimi kama mtumishi wa umma namshukuru sana huyu mama amenipandisha daraja na hapa hospital ninapofanyia kazi ameleta bilioni 1 ujenzi wa jengo la upasuaji , ujenzi wa laboratory ya kisasa na vifaa vyake namshukuru sana. Na hii amefanya nchi nzima. Sitaki kuelezea mengine watakwambia wengine
 
[emoji1787] Kafanya nini
Katoa ajira nyingi kuliko alizotoa Magu 6yrs
Miundombinu madarasa vituo vya afya vimeota kama uyoga muda mfupi

Saizi chadema wanafanya mikutano enzi za magu sauti ni yeye tuu

Tarura bajet imeongezeka saizi kila kijiji kimechongewa barabara

Kifupi kama una chuki hata uambiwe vipi utapinga tuu
 
Nasema hivi, na nitaendelea kusema hata miaka 7 ijayo ya utawala wa mama samia, kuwa haters wa mama Samia, The Mother of Modern Tanzania, wako hatarini kujifungua kabla ya wakati. Mada hii ni moja ya mamia ya ushahidi niliyonayo!!
 
Katoa ajira nyingi kuliko alizotoa Magu 6yrs
Miundombinu madarasa vituo vya afya vimeota kama uyoga muda mfupi

Saizi chadema wanafanya mikutano enzi za magu sauti ni yeye tuu

Tarura bajet imeongezeka saizi kila kijiji kimechongewa barabara

Kifupi kama una chuki hata uambiwe vipi utapinga tuu
Dah, yaani Acha tu mkuu......mama Samia, The Mother of Modern Tanzania, ni ujumbe tosha kwetu kuwa hiki kiumbe kinachoitwa 'binadamu' achana nacho kabisa. Ni kiumbe kilichojaa chuki, wivu, husda, fitina, uongo, ubinafsi, kujikweza, ubaguzi na kila aina ya uchafu.

Nina imani kubwa, kama walivyoshindwa waliopanga kumzuia kuingia ikulu, basi mashetani hawa wachafu pia watashindwa......tena vibaya sana.
 
Back
Top Bottom