Utawala wa Trump wafuta misaada yote ya silaha kwa Ukraine na uchunguzi unafuata

US hana cha kumfanya Russia, yy cha msingi amkoromea Zelenskyy atafute means ya kumalizana na Putin.
Ukitaka kujua kipo ,Putin akatae ofa sasa, ndio mtajua nini ana maanisha Trump, huyu sio Biden
 
Mkuu wa NATO Mark Rutte amesema Ulaya itanunua silaha toka Marekani na watazipeleka Ukraine.
 
Kwani Putin katoa masharti mangapi NATO na US wame yavunja mpaka anatishia Nyuklia
kwani nani hana silaha za Nuclear? Maanake ukiona wanakutishia unazitumia. Hata US alitishia kutumia silaha za Nuclear kwa Cuba,baada ya Russia kutaka kufunga silaha za maangamizi Cuba. So alicho kikataa yy ndicho wanacho taka kukifanya NATO na US kufunga silaha za maangamizi Ukraine, so Russsia kutishia yupo sawa na mpaka unamuona taifa linatishia basi linamsuli mkubwa kifedha na kivita.
 
 
Kabla vita kuanza alikuwa na msuli ila kwasasa msuli umepungua inabidi aombe msaada kwa Iran na Korea ya KIM ndio kapewa wanajeshi 12000 wamsaidie kule Kursk ,Putin katisha watu weee kuhusu nyuklia mpaka kachoka mwisho kaishia kubadili. Doctrine watu wanapiga hivyo hivyo mpaka Moscow

 
Kwani kuna ubaya kusaidiwa na washirika wake kwani US Libya,Iraq si alisadiwa na washirika wake wa NATO? Ina maana aliishiwa US?
 
Kwani kuna ubaya kusaidiwa na washirika wake kwani US Libya,Iraq si alisadiwa na washirika wake wa NATO? Ina maana aliishiwa US?
Alipigana vita na washirika toka mwanzo, hii ni tofauti na Putin baada ya kuona silaha na wanajeshi wanakwisha ndio kaenda kutafuta msaada, tena kama Iran anasema aliuza Drone mwezi kabla wala hakujua kuwa Urusi anataka kuanzisha vita
 
Alipigana vita na washirika toka mwanzo, hii ni tofauti na Putin baada ya kuona silaha na wanajeshi wanakwisha ndio kaenda kutafuta msaada, tena kama Iran anasema aliuza Drone mwezi kabla wala hakujua kuwa Urusi anataka kuanzisha vita
Kwa hiyo ukisaidiwa tokea mwanzo ni tofauti ukisaidiwa mwishoni?
 
Kwa hiyo ukisaidiwa tokea mwanzo ni tofauti akisaidiwa mwishoni?
Tofautisha msaada na ushirika, Us alipigana vita na washirika kuanzia maamuzi mpaka kuingia vitani, ILA Urusi kapanga vita vyake vina muelemea sasa kaenda kuomba msaada
 
Tofautisha msaada na ushirika, Us alipigana vita na washirika kuanzia maamuzi mpaka kuingia vitani, ILA Urusi kapanga vita vyake vina muelemea sasa kaenda kuomba msaada
Kwa hiyo US alijijua ni dhaifu na akahisi vita itamuelemea ndio maana kaomba msaada kwa washirika wake tokea mwanzo?
 
Anaokoteza kama vile marekani alivyookoteza askari UK, German na ufaransa kuivani Iraq.
 
Kwa hiyo US alijijua ni dhaifu na akahisi vita itamuelemea ndio maana kaomba msaada kwa washirika wake tokea mwanzo?
Hapana waliamua kumpiga kwa pamoja ili iwe jambo la wote, ila Urusi jambo la Ukraine lilikuwa lake binafsi kwahiyo baada ya unga kuzidi maji katoka mbio kwa KIM kuomba salama
 
Hapana waliamua kumpiga kwa pamoja ili iwe jambo la wote, ila Urusi jambo la Ukraine lilikuwa lake binafsi kwahiyo baada ya unga kuzidi maji katoka mbio kwa KIM kuomba salama
Sasa kwani Russia kuamua mwisho kumpiga pamoja Ukraine kwa kushirikia na NK kuna ubaya? Sasa huyo ambaye unasema maji yalizidi unga,ndiye US alimuomba akawarudishe wanaanga wake waliokwamba angani. Nikakuuliza why NASA na Mask waishindwa,wakati NASA bajeti yao ni kubwa na Mask ni tajiri namba moja.
Ila around mwezi wa kumi mwaka jana,kwa kutumia resources na bajeti yake akawarudisha hao wananga,halafu taifa kama hili maji yazidi unga, mbona unajicontradict mwenyewe.
 
Nimekwambia usichanganye ushirikiano na msaada, Unarudia yale yale , Kushirikiana maana yake ni kuanzia mipango yote mpaka mnakwenda vitani na ndio kitu US alifanya na washirika wake, PUTIN alipigana vita mwenyewe baada ya kuona amepoteza watu na silaha nyingi ndio anakwenda KUOMBA msaada kufidia alichopoteza , maji yamezidi unga hii ndio maana yake, sasa unarudi kule kule kwa NASA wakita nilishajibu
 
Walimu wanakazi so ushirikiano ni tofauti na msaada? Kwa hiyo mkishirikiana hamna kuasaidiana? Haisee kiswahili kigumu..... kwani hili la Ukraine,US na NATO si walipanga tokea mwanzo na wakakubaliana,kufunga silaha za maangamizi Ukraine, mbona NATO na US wanatoa msaada kwa Ukraine na Trump katishia kusitisha au huu unaotolewa na NATO pamoja na US sio msaada sababu mwanzo walishiriki kupanga wote hii vita kwa pamoja?

Nimekuuliza mtu ambaye maji yamezidi unga ndiye US alimuomba akawarudishe wana anga wake ,halafu unasema maji yamezidi unga.Lazima nirudi kwa NASA sababu huelewi unacho kizungumza,nimemtumia NASA na MUSK kuonyesha capability ya Rusia kitech na kiuchumi, kwani huwezi fanya hivi vitu kama kiuchumi haupo vizuri.
 
Nimesha kupa maana una uliza tena swali lile ushirikiano sio msaada , kila moja ina hatua zake mbona nimesha eleza juu uko, sasa kuambiwa kurudisha wanaanga ndio kunakufanya wewe usitafute msaada kwa Korea ya kaskazini? mbona unalinganisha vitu hata havina uhusiano? mambo ya anga na wewe vita kuwa ngumu vina uhusiano gani? namna hii lazima waalimu wapate tabu
 
Kwani kwenye vita kwa nini kuna kikosi cha anga? Kama anga na vita ni tofauti? Yaani unajicontradict.........

Okay dhumuni la msingi la NATO au BRICS ni nini? unaweza Google naamini kupitia hizo taasisi ndipo utaelewa dhumuni ya hizo taasisi ni kushirikiana na KUSAIDIANA.

Halafu unasema maji yamezidi unga huku washirika wa NATO na US hawataki kutoa msaada wa kuisaidia Ukraine ,hivi ushajiuliza kwa nini hawataki kumsaidia Ukraine kwa sasa?
 
Mkuu ebu fatilia jeshi la anga la Urusi na wana anga wa kawaida, usichanganye mambo aiseee, NATO iliundwa kwa ajili ya kumzuia Sovieti asijitanue Ulaya yote , NATO ipo kwa ajili ya usalama wa wanachama, BRICS ni kitu kingine kabisaa kwa ajili ya mambo tofauti na NATO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…