Utawala wa Trump wafuta misaada yote ya silaha kwa Ukraine na uchunguzi unafuata

......
Trump ana mpango wa kujitoa NATO, unaelewa kuwa US kujitoa NATO ni kuikabidhi Ulaya nzima at mercy of Russia?

Nguvu pekee dhidi ya Russia ni NATO, US kujitoa na kuivunja NATO, Huoni kuwa ni kumfanya Russia superpower?
Mkuu unamaanisha nin kusema Ulaya nzima itakuwa at mercy ya mrusi?

Pili, kwani Russia akiwa superpower kuna ubaya?

Nachojua ni kwamba Trump hataki kodi za wamarekani ziende kusiko na maslahi ya marekani.
 
Pravda ni chombo cha habari cha Urusi. Wapo Urusi na taarifa za wazi za Marekani wamezipataje bila wao kuwa na source iliyopo serikali ya Marekani.

TBC inawezaje kutoa taarifa ya kauli au uamuzi wa wazi wa serikali ya Nigeria, bila serikali ya Nigeria kutoa taarifa?
 
Ujinga wa nani? Putin mvamizi mme wa Trump au Ukraine wanaopigana kulinda nchi Yao?
Ama uelewa wako mdogo au unafata mkumbo. Chanzo cha vita kinajulikana, kwanini wakati wa vita baridi na mpaka Sasa marekani hawakutaka Urusi aweke mitambo yake ya nyukilia Cuba .
 
Naelewa namna unavyojisikia mkuu, ndio maana ukaandika kwa herufi kubwa, but ka suspend.

Nadhani sasa ndio muda wa EU, kuonesha uwezo wao, maana walisema wametenga budget ya kuendelea na vita bila U.S support na wame allocate kama 300B US dollar, Tuone walikuwa serious au zilikuwa tishia nyau.
 
Mkuu kote nilikuwa nakubaliliana na wewe, ila ulipoanza kutoa povu la US kujitoa kwenye hayo mashirika nikakushangaa kidogo, kama aliingia kwa hiyari hata kutoka ni hiyari, na sielewi kwanini third party wanaumia kuliko wahusika.
Yeye kaangalia faida na hasara.
kama anajitoa alafu uchumi wake unakuwa na anaendelea ku maintain military base, ushawishiki wake hautapungua kama mnavyodhani
 
Je CNN na Washington Post wanapotoa habari za Russia mbona mnaziamini bila kutia shaka?
 
Natafuta hii habari niisome au kama ni video nitazame. Unaweza kunisaidia mkuu kama hutojali.
 
Wakubaliane na Ukraine, vinginevyo Trump akigundua shida ni Urusi basi vikwazo vinakuja, kama shida ni Ukraine anakata misaada yote ya kijeshi, Trump akili kubwa
Urusi keshamwambia kama anataka mazungumzo aje kwa heshima.....hio mikwara yake itamshtua Zelensky tu,,,,vikwazo kwa Urusi kwa sasa sio tatizo
 
Urusi keshamwambia kama anataka mazungumzo aje kwa heshima.....hio mikwara yake itamshtua Zelensky tu,,,,vikwazo kwa Urusi kwa sasa sio tatizo
Hili ni jambo la Urusi na Ukraine, yeye Trump ni kaka mkubwa, anataka wamalizane ila atakae leta utata anashuka nae
 
Ila ilianzishwa na US wenyewe kwa faida zao, sasa wameona matumizi yake yamepungua na imekuwa mzigo ndio maana wanajitoa, au pia haiendani na sera za serikali yake
Hata kwenye mkata wa hali ya hewa pia wanajitoa, sababu haiendani na sera za serikali yake, sasa sioni tatizo.

Yaani hii sawa tajiri kujitoa kwenye umoja wa kusaidia wasiojiweza, sasa wasiojiweza wanaanza kumtisha tajiri kuwa usipotusaidia unapoteza umaarufuku wako kwwnye jamii, wanasahau tajiri anachojali ni kutokufilisika na kuongeza utajiri wake ujitoa kwenye umoja flani kwa manufaa yako, alafu watu kuku
 
Ni ilani yake ya uchaguzi ndio maana wa Marekani wamemchagua, wameona ana mashiko kwenye hoja zake, hata Mchina ushawishi anao lakini hatoi pesa nyingi kama yeye , ndio maana Trump katumia mwanya huo kufyeka kichaka
 
Umeongea vzr Beira Boy ,kuna watu sijui walilelewa vipi na mitaa ipi...Yani heshima kwao ni kitu cha anasa sana,unaanzaje kudhihaki mtu mzima kama Trump,mwenye familia?
 
Hili ni jambo la Urusi na Ukraine, yeye Trump ni kaka mkubwa, anataka wamalizane ila atakae leta utata anashuka nae
Hio position anayokaa mmarekani ndi mrusi haitaki ndo maana kamwambia aje kwa heshima vikwazo vyake sio jambo geni na hatishiki
 
Tutajua tuwape muda kama katishika au lah
Sio walamba miguu wa wamagharibi hao.......na jamaa wanajua mrusi na china wameingia Africa kutibua mipango yao (Global South) chaguzi nyingi kwa sasa Afrika zina mikono ya pande 2 kwa sasa global north (wamagharibi/mabepari) na global south (wengi wao ni zile nchi zilizokua za kijamaa) hata huu mwaka uchaguzi una elements za hizo pande 2 na anajulikana atakaeshinda,,,.......,,kwahio wakijifanya kuleta ubabe wao wa enzi hizo na wao wanajua pakuwatetemesha. ..AFRICA IS THE NEW FRONTIER
 
Mrusi ameingia Africa kuservive hali ni mbaya, vita ni gharama sana, kwahiyo amekuja Africa kukwepa vikwazo, pesa ambazo alikuwa anapata Ulaya ni nyingi, ndio yupo Africa kwa ajili ya mali halafu anawapa ulinzi na wanajeshi wale wa Wagner ili kukwepa vikwazo, huyu Urusi wa sasa sio yule wa kabla ya vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…