Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Kuna kipindi fulani ilikuwa ukisikia kuwa kesho katibu mkuu wa Chadema Mh. Dr Slaa atakuwa na mazungumzo muda fulani, ni kama nchi ilikuwa inasimama. Vyombo vyote vya habari vilikuwa vinafika hata kabla ya muda husika, kila mtanzania alikuwa anatega sikio kusikia nini kitakacho zungumzwa.
Kila Kona ya nchi ilikuwa inakuwa ni gumzo lisilo pimika, ilikuwa ni kana kwamba Rais wa marekani anakuja kutolea tamko Tanzania juu ya kuuwawa kwa Osama bin laden. Watu walikuwa hawatulii walipokaa, wasio na TV walikwenda hata vibanda umiza kuchungulia ilimradi tu asijesubili kusimuliwa.
Hoja nzito nzito zilishushwa huku zikinogeshwa na vijana wa Redbriged waliokuwa wanakaa nyuma ya viongozi wao. Sisi vijana wa CCM wakati mwingine tulikuwa hatuelewi tutajibu nini juu ya nondo zinazokuwa zimeshushwa, hivyo tulibaki tukirusha rusha miguu wakati tukisubili akina Mh. Nape walete silaha za hoja kujibu vijana wenzetu wa upinzani huku site.
Hata mikutano tu ilikuwa ukisikia Dr slaa anakuja Mbeya mjini kwenye uwanja wa Rwanda Nzovwe maarufu kama CCM, jiji lote lilikuwa linasimama, shughuli zote zilikuwa zinasimama. Mimi nilikuwa nikitoka shule Sekondari ya Ivumwe, nilikuwa hata sipiki chakula zaidi ya kwenda mkutanoni ili nijuwe wanasema nini hawa watani zangu.
Alikuwa akija anapokelewa kama Rais wa nchi, shangwe kubwa hata uwe mwanjelwa unasikia. Ilikuwa ni Kama nchi inakwenda kupinduliwa kwa maandano. Ilikuwa ni kama wananchi wote wapo upinzani japo wa CCM tuliogopa hata kuvaa sare kuepuka kupigwa. Ilikuwa ukisikia "PIPOZ" watu walikuwa wanaitikia utazan wanataka kulia jinsi walivyo na hasira!
CCM fundiii bwana, CCM chama kubwa, CCM Ina mbinu hadi za reserve, CCM ndio chama kiongozi, CCM ndio mkombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, CCM ndio chama Cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Unajua nini kilifanyika upinzani wakapewa Mh. nguli wa mikakati ya kisiasa Mh. Edward Lowasa waliyemtukana kwa miaka takribani nane kuwa ni fisadi? Ilikuwa ni kwa ajili ya kumsafisha na kumpaka mafuta hadi apendeze.
Hapo ndioo tukaanza kuona mvurugano ndani kwa ndani. Mara Dr slaa akatimka kwa kusema hawezi kazi hiyo, mara Mnyika akazira, mara sijui Mh Sanaa havai makombati yao, Mara huku Askofu Gwajima akasema alikuwa mshenga, mara sijuw nini yaani ikawa furu michanganyo.
Baada ya hapo akaingia Dr John Pombe Magufuli kama Rais wa nchi. Aliwakaba hadi vivuli vyao wakawa wanavikimbia. Hapo ndio ikajulikana pia nani ni mpinzani na nani ni mpinzani njaa. watu waliunga mkono juhudi kama hawana akili nzuri.
Baada ya hapo ndio akaja mama yetu kipenzi cha watanzania, mzalendo wa kweli, mwenye maneno ya upendo na faraja, mwenye tbasamu la upendo na ukarimu, aliyejaa hekima na busara katika kifua chake, mwenye moyo wa huruma na upendo akaanza kusuka serikali yake hatua kwa hatua. Watu wakaanza kushituka maana hawakutegemea jinsi anavyoendesha nchi kwa weledi na utumishi uliotukuka.
Hapa ndio ikawa mwisho na hitimisho la upinzani hapa nchini, kwa sasa hakuna mwananchi atakuelewa juu ya upinzani. Kwa sasa wananchi wapo na mama, kwa sababu mama yetu amewafanya watu wawe na iman naye. Anaendesha nchi kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na utawala bora.
Utawaambia nini wakulima juu ya mama Samia wakati wanaona juhudi za mama katika kilimo hasa baada ya kutoa ruzuku kwenye Wizara ya Kilimo takilibani billion mia hamsini na kumkabidhi kijana wake Mh. Hussein Bashe ili asimamie? Utawaambia nini wananchi wakati wanaona mama sasa ameweka elimu bure hadi kidato cha sita? Utawambia nini watu wakati wanaona vyumba vya madarasa, vituo vya afya, zahanati na maji vikisambazwa kila kona ya nchi?
Hakuna anayeweza kukuelewa ukimsema vibaya mama yetu kipenzi mama Samia Suluhu Hassani kwa utendaji wake bora wa kazi. Huku Songwe ni mama anaupiga mwingi na wala huwaambii na wakakuelewa habari za upinzani.
Nakupenda CCM na nitaendelea kuwa mwana CCM. Hapa ni Tanzania na siyo Kenya, hata tuwape upinzani wasimamie uchaguzi bado CCM itashinda tu. CCM ndio tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo. Upinzaani asante sana kwa kumuunga mkono mama yetu na msisite kushirikiana zaidi na zaidi na mama yetu kuijenga nchi yetu maana upinzani siyo uadui.
Kazi iendelee, sote tumuunge mkono Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassani katika kuijenga Tanzania mpya.