Utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia umedhoofisha upinzani Tanzania

Duh! Bado mnamsingizia Marehemu hadi leo!!? Mi nilikua najua baada ya JPM kuondoka,saa hizi CDM mngekua Ikulu ya Chamwino iliyojengwa na JPM!!!??
Ndo hapo Sasa hata nami nimemshangaa kana kwamba haoni juhudi za mh Rais, mh Mbowe mwenyewe alimpongeza Rais na kusema kuwa Mh Rais Anastahili pongezi
 
Ndugu zangu Kuna kipindi fulani ilikuwa ukisikia kuwa kesho katibu mkuu wa Chadema Mh. Dr Slaa atakuwa na mazungumzo muda fulani, ni kama nchi ilikuwa inasimama. Vyombo vyote vya habari vilikuwa vinafika hata kabla ya muda husika, kila mtanzania alikuwa anatega sikio kusikia nini kitakacho zungumzwa.

Kila Kona ya nchi ilikuwa inakuwa ni gumzo lisilo pimika, ilikuwa ni kana kwamba Rais wa marekani anakuja kutolea tamko Tanzania juu ya kuuwawa kwa Osama bin laden. Watu walikuwa hawatulii walipokaa, wasio na TV walikwenda hata vibanda umiza kuchungulia ilimradi tu asijesubili kusimuliwa.

Hoja nzito nzito zilishushwa huku zikinogeshwa na vijana wa Redbriged waliokuwa wanakaa nyuma ya viongozi wao. Sisi vijana wa CCM wakati mwingine tulikuwa hatuelewi tutajibu nini juu ya nondo zinazokuwa zimeshushwa, hivyo tulibaki tukirusha rusha miguu wakati tukisubili akina Mh. Nape walete silaha za hoja kujibu vijana wenzetu wa upinzani huku site.

Hata mikutano tu ilikuwa ukisikia Dr slaa anakuja Mbeya mjini kwenye uwanja wa Rwanda Nzovwe maarufu kama CCM, jiji lote lilikuwa linasimama, shughuli zote zilikuwa zinasimama. Mimi nilikuwa nikitoka shule Sekondari ya Ivumwe, nilikuwa hata sipiki chakula zaidi ya kwenda mkutanoni ili nijuwe wanasema nini hawa watani zangu.

Alikuwa akija anapokelewa kama Rais wa nchi, shangwe kubwa hata uwe mwanjelwa unasikia. Ilikuwa ni Kama nchi inakwenda kupinduliwa kwa maandano. Ilikuwa ni kama wananchi wote wapo upinzani japo wa CCM tuliogopa hata kuvaa sare kuepuka kupigwa. Ilikuwa ukisikia "PIPOZ" watu walikuwa wanaitikia utazan wanataka kulia jinsi walivyo na hasira!

CCM fundiii bwana, CCM chama kubwa, CCM Ina mbinu hadi za reserve, CCM ndio chama kiongozi, CCM ndio mkombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, CCM ndio chama Cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Unajua nini kilifanyika upinzani wakapewa Mh. nguli wa mikakati ya kisiasa Mh. Edward Lowasa waliyemtukana kwa miaka takribani nane kuwa ni fisadi? Ilikuwa ni kwa ajili ya kumsafisha na kumpaka mafuta hadi apendeze.

Hapo ndioo tukaanza kuona mvurugano ndani kwa ndani. Mara Dr slaa akatimka kwa kusema hawezi kazi hiyo, mara Mnyika akazira, mara sijui Mh Sanaa havai makombati yao, Mara huku Askofu Gwajima akasema alikuwa mshenga, mara sijuw nini yaani ikawa furu michanganyo.

Baada ya hapo akaingia Dr John Pombe Magufuli kama Rais wa nchi. Aliwakaba hadi vivuli vyao wakawa wanavikimbia. Hapo ndio ikajulikana pia nani ni mpinzani na nani ni mpinzani njaa. watu waliunga mkono juhudi kama hawana akili nzuri.

Baada ya hapo ndio akaja mama yetu kipenzi cha watanzania, mzalendo wa kweli, mwenye maneno ya upendo na faraja, mwenye tbasamu la upendo na ukarimu, aliyejaa hekima na busara katika kifua chake, mwenye moyo wa huruma na upendo akaanza kusuka serikali yake hatua kwa hatua. Watu wakaanza kushituka maana hawakutegemea jinsi anavyoendesha nchi kwa weledi na utumishi uliotukuka.

Hapa ndio ikawa mwisho na hitimisho la upinzani hapa nchini, kwa sasa hakuna mwananchi atakuelewa juu ya upinzani. Kwa sasa wananchi wapo na mama, kwa sababu mama yetu amewafanya watu wawe na iman naye. Anaendesha nchi kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na utawala bora.

Utawaambia nini wakulima juu ya mama Samia wakati wanaona juhudi za mama katika kilimo hasa baada ya kutoa ruzuku kwenye Wizara ya Kilimo takilibani billion mia hamsini na kumkabidhi kijana wake Mh. Hussein Bashe ili asimamie? Utawaambia nini wananchi wakati wanaona mama sasa ameweka elimu bure hadi kidato cha sita? Utawambia nini watu wakati wanaona vyumba vya madarasa, vituo vya afya, zahanati na maji vikisambazwa kila kona ya nchi?

Hakuna anayeweza kukuelewa ukimsema vibaya mama yetu kipenzi mama Samia Suluhu Hassani kwa utendaji wake bora wa kazi. Huku Songwe ni mama anaupiga mwingi na wala huwaambii na wakakuelewa habari za upinzani.

Nakupenda CCM na nitaendelea kuwa mwana CCM. Hapa ni Tanzania na siyo Kenya, hata tuwape upinzani wasimamie uchaguzi bado CCM itashinda tu. CCM ndio tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo. Upinzaani asante sana kwa kumuunga mkono mama yetu na msisite kushirikiana zaidi na zaidi na mama yetu kuijenga nchi yetu maana upinzani siyo uadui.

Kazi iendelee, sote tumuunge mkono Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassani katika kuijenga Tanzania mpya.​
Hizi ndio tabia za ovyo zinazorudisha hii nchi nyuma, hawa ndio wale Msigwa wameajiriwa wengi kwenye mitandao kusifu na kutukuza. Humu JF sio mahala pake hili jukwaa lilianza kutengeneza fikra mbadala nyie wa kusifu mnazo platforms nyingi mno mngetuachia critical thinkers. Hatujakataa Mama anafanya kazi ila punguzeni sifa humu tumulike yale yasiyotimia. Rushwa kwa askari polisi na utendaji mbovu wa jeshi la polisi hili uwezi sema kumuondoa Sirro haitoshi. We endelea kuwa CCM lakini gharama za maisha ziko juu mno na uzalishaji wetu bado uko chini. Excuse ya kusema kuna vita Ukraine haitoshi kukabiliana na mfumuko unaoendelea. Sie huku tunayo natural gas hatuoni jitihada zozote za serikali katika kuchukua hatua mbadala, magari yabadilishwe kutumia natural gas tena kwa mkopo wa serikali. Kuna shida kubwa mno katika teuzi na raisi anafanya recycling ya watu wale wale wasio na tija, nakupa mfano wa ferry kigamboni warasimu na ndio wafanya maamuzi wanataka Pantoni kuubwa la kuingiza gari nyingi na linahitaji matirioni, Azam wao wamekuja na Taxii za baharini ni mamilioni unanunua na uwezi amini zinapiga kazi kwa gharama nafuu. Point yangu wapo watanzania wanaakili nyingi na wanaamua kutoka sekta binafsi Mama inaonekana kapewa list ya wenzetu ambao lazima wawepo na hawana tija yeyote ni kuhamishwa ofisi tu kila teuzi wamo tu. Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ndio ngao zetu ona danadana na sarakasi na mipango mizuri ya katika makaratasi, tuliambiwa kuna Bank ya Kilimo we acha tu hamtaki watu wanaouliza maswali magumu. Huko bungeni angalia quality ya so called watunga sera na wafanyamaamuzi hapa kuna shida. Wanachaguliwa watu hawapewi malengo ya kazi matokeo yake sasa wa ilala na Temeke utafikiri india na china. Uhuru wa kuchagua na kufanya siasa upo bado mikononi mwa polisi, watu ambao wenyewe hawajitambui. Tusiendelee kupongeza mtu kwa kutembelea miguu miwili, tunataka kuona mtu anatumia mguu mmoja au anatembele kichwa ndio tupige makofi.
 
Changia mada hayo ya usajiri hayana nafasi hiyo, Na sizani Kama wewe uliisajiilwa hapa na mtu ili uje umpambe, Kama ulifanya hivyo Basi Mimi sijasajiliwa na mtu kuja kumpamba bali kutoa mawazo yangu Kama mtu huru
Kama haya uliyoyaandika ni mada,basi pole sana kwa kuwa na tatizo la ufahamu.
 
Hizi ndio tabia za ovyo zinazorudisha hii nchi nyuma, hawa ndio wale Msigwa wameajiriwa wengi kwenye mitandao kusifu na kutukuza. Humu JF sio mahala pake hili jukwaa lilianza kutengeneza fikra mbadala nyie wa kusifu mnazo platforms nyingi mno mngetuachia critical thinkers. Hatujakataa Mama anafanya kazi ila punguzeni sifa humu tumulike yale yasiyotimia. Rushwa kwa askari polisi na utendaji mbovu wa jeshi la polisi hili uwezi sema kumuondoa Sirro haitoshi. We endelea kuwa CCM lakini gharama za maisha ziko juu mno na uzalishaji wetu bado uko chini. Excuse ya kusema kuna vita Ukraine haitoshi kukabiliana na mfumuko unaoendelea. Sie huku tunayo natural gas hatuoni jitihada zozote za serikali katika kuchukua hatua mbadala, magari yabadilishwe kutumia natural gas tena kwa mkopo wa serikali. Kuna shida kubwa mno katika teuzi na raisi anafanya recycling ya watu wale wale wasio na tija, nakupa mfano wa ferry kigamboni warasimu na ndio wafanya maamuzi wanataka Pantoni kuubwa la kuingiza gari nyingi na linahitaji matirioni, Azam wao wamekuja na Taxii za baharini ni mamilioni unanunua na uwezi amini zinapiga kazi kwa gharama nafuu. Point yangu wapo watanzania wanaakili nyingi na wanaamua kutoka sekta binafsi Mama inaonekana kapewa list ya wenzetu ambao lazima wawepo na hawana tija yeyote ni kuhamishwa ofisi tu kila teuzi wamo tu. Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ndio ngao zetu ona danadana na sarakasi na mipango mizuri ya katika makaratasi, tuliambiwa kuna Bank ya Kilimo we acha tu hamtaki watu wanaouliza maswali magumu. Huko bungeni angalia quality ya so called watunga sera na wafanyamaamuzi hapa kuna shida. Wanachaguliwa watu hawapewi malengo ya kazi matokeo yake sasa wa ilala na Temeke utafikiri india na china. Uhuru wa kuchagua na kufanya siasa upo bado mikononi mwa polisi, watu ambao wenyewe hawajitambui. Tusiendelee kupongeza mtu kwa kutembelea miguu miwili, tunataka kuona mtu anatumia mguu mmoja au anatembele kichwa ndio tupige makofi.
Nashukuru kuwa umekubali kuwa mh Rais anafanya kazi njema na nzuri, hayo mengina mfano ya rushwa Hakuna mahali ambako mh Rais anayafumbia macho, pia wewe ukiombwa rushwa ndio inatakiwa uwe wa kwanza kutoa taarifa

Kuhusu mfumuko wa Bei Ni suala la Dunia nzima kwa Sasa, hata hivyo Rais wetu anaendelea kupambana nalo kupunguza makali kwa mwananchi, Ndio maana unaona ametoa na kuweka Ruzuku ya billion Mia moja katika mafuta na billioni Mia hamsini katika mbolea,

Pia serikali yake kupitia Wizara ya Fedha amekuwa akiondoa au kupunguza tozo zisizo na alazima, juhudi zote hizi Ni katika kukabiliana na mfumuko wa Bei
 
Duh! Bado mnamsingizia Marehemu hadi leo!!? Mi nilikua najua baada ya JPM kuondoka,saa hizi CDM mngekua Ikulu ya Chamwino iliyojengwa na JPM!!!??
Shujaa kaacha madhara mengi.
Itachukua muda kurudi katika mstari wa haki.
 
Vitu kama hivyo vinaendelea kumalizwa kisheria kwa utaratibu mzuri hatua kwa hatua ili tuijenge Tanzania Yetu kwa Hali ya umoja na mshikamano, hujasikia wale walioachiwa kule katavi, Geita, songwe na hata kule Njombe, wote hao wameachiwa katika utaratibu mmoja

Hata hivyo siyo wote wataachiwa tu kwa namna Kama hiyo, wengine watalazimika kujibu mashitaka yao, maana wapo walioharibu na kujeruhi wengine kwa kimvuli Cha kupambania vyama vyao, hao watawajibishwa kwa mujibu wa Sheria

Tuendelee kushikamana na Tuvumiliane katika siasa zetu, tutangulize mbele utanzania wetu na tubishane kwa hoja na panapobidi tukubaliane na kupongezana, Tukosoane kwa staha na heshima kwa kulinda utu wetu bila kuvunjiana heshima

Mbona wanaccm hawako ndani na wao waliendesha ukatali wa wazi na ushahidi upo?
 
Utendaji kazi nzuri wa mh Rais una uhusiano mkubwa Sana tuu, maana mfano labda ingekuwa Rushwa imetawala, wananchi wakienda hospitalini hakuna huduma Bora Wala kusikilizwa, mitaani maji shida halafu hakuna juhudi zinazofanyika, unazani wananchi wangempenda Rais wao, unazani wangeipenda serikali?

Lakini wananchi wanamuunga mkono Rais na serikali yake kwa kuwa wanaona juhudi kubwa anazofanya kuwatumikia wananchi, namna anavyotatua kero na changamoto na namna anavyogusa maisha yao
Sawa Mama anajitahidi.Lakini haina uhusiano wowote na ukimya wa vyama vya upinzani.
Kumbuka kuwa mpaka leo ni marufuku vyama vya upinzani kufanya mikutano.
Pia kumbuka wizi wa kura uliofanyika 2019 & 2020 uliopelekea shujaa kunyakua wabunge wote na serikali zote za mitaa kwa asilimia 100
 
Chama Cha siasa kazi yake Ni kuwa midomoni na mioyoni mwa watu muda wote, Na ili ufanikiwe katika Hilo unapaswa kuwa na ajenda za msingi zinazogusa maisha ya watu hasa wale wa chini ambao ndio kundi kubwa

Kwa sasa ajenda za msingi zimeshikwa na mh Rais ndio maana unaona akipata uungwaji mkono mkubwa Sana toka kwa watu tofauti tofauti bila kujali mlengo wao wa kisiasa,

Kwa kuwa Amedhamilia kuijenga Tanzania mpya kwa kushirikiana na mtu yoyote ambaye yupo tayari, Ndio maana unaona pia akiwakaribisha na kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya upinzani Ikulu,

Nawakitoka hapo unaona wote wakizungumza kauli za kuwaunganisha watu na kuijenga nchi yetu kwa pamoja kwa kuhubiri Amani upendo mshikamano na Utendekaji wa Haki

Tumuunge mkono Rais wetu, Tukosoane kwa heshima, vyama hivi visiwe vikubwa kuliko nchi yetu na visitufanye tukaigawa vipande vipande nchi yetu nzuri ambayo hata majirani zetu wanaiangalia kwa jicho la wivu kwa namna tulivyo wamoja, licha ya kuwa tuna makabila Zaid ya Mia ishilini
 
Nashukuru kuwa umekubali kuwa mh Rais anafanya kazi njema na nzuri, hayo mengina mfano ya rushwa Hakuna mahali ambako mh Rais anayafumbia macho, pia wewe ukiombwa rushwa ndio inatakiwa uwe wa kwanza kutoa taarifa

Kuhusu mfumuko wa Bei Ni suala la Dunia nzima kwa Sasa, hata hivyo Rais wetu anaendelea kupambana nalo kupunguza makali kwa mwananchi, Ndio maana unaona ametoa na kuweka Ruzuku ya billion Mia moja katika mafuta na billioni Mia hamsini katika mbolea,

Pia serikali yake kupitia Wizara ya Fedha amekuwa akiondoa au kupunguza tozo zisizo na alazima, juhudi zote hizi Ni katika kukabiliana na mfumuko wa Bei
Juhudi hazitoshi ndio tunakwambia nyie warasimu njia zenu za kuondosha matatizo ya wananchi ni ndeefu mno jifunzeni wa sector binafsi, kwa majibu mazuri mbona mko vizuri dunia nzima. Rushwa katika jeshi la polisi mbona ni yeye amir jeshi kukubari ipo kwanza ndio tatizo linapoanzia.

Mfumuko wa bei ni kuongeza uzalishaji katika kilimo, Mzee Magu alizuia mfumuko kwa kufunga mipaka, mama amefungua tunakubali ila uzalishaji ndio utiliwe mkazo bei zitashuka achaneni na hizo siasa za vita ya ukraine ambayo imeathiri bei ya ngano nyie wamatumbi na ngano wapi na wapi, mahindi ndio kila kitu tuongeze ackrage, na tractors za kulima bei zitashuka zenyewe.

Tozo hilo ndio chaka mnalojifichia kupata kodi kiubwete, ongezeni uzalishaji serikali itapata kodi nyingi zaidi kuliko tozo
 
Nashukuru mkuu Wala usijari maana ndio lengo la serikali kuhakikisha uzalishaji katika kilimo unaongezeka Zaid na zaidi, Ndio maana ya kauli mbiu ya mwaka huu kuwa kilimo Ni biashara, hivyo huwezi kufanya biashara pasipo kuwa na uzalishaji wa kutosha na bidhàa za kutosha,

Katika kufanya na kufanikisha Hilo serikali imeamua kuweka Ruzuku katika pembejeo ili mkulima awe na uwezo wa kununua pembejeo kukuza kipato, kwa kupata kipato kikubwa na Bora zaidi

Lakini pia serikali inafanya kazi ya kuimalisha taasisi za utafiti ili kuweza kupata mbegu Bora kulingana na eneo husika na Hali ya hewa yaani mvua katika ukanda husika

Pia serikali inajitahidi kuongeza wataalamu watakao kwenda vijijini na kuwa karibu na wakulima kwa ajiri ya kutoa ushauri kwa wakulima juu ya mbinu Bora na za kisasa za kilimo, yote hii Ni dhamila njema ya mh Rais kuona kuwa kilimo kinamnufaisha mkulima

Mwisho tuna kila sababu ya kumpongeza mh Hussein Bashe Waziri wa kilimo kwa namna anavyojituma kutekeleza majukumu yake ndani ya Wizara hii, Amekuwa Chachu ya maendeleo ya Wizara ya kilimo
 
Ebu achana na hizi mambo huu ndio upotezaji wa pesa, angalia watu binafsi wanalima na kufuga jifunzeni kutoka kwao kwanza zipo quick win, haya mengine ni siasa zisizo na tija miaka nenda miaka rudi.
Arable land zipo na unakuta kijijini ardhi inayotumika kwa kilimo ni 20% tu, kila kata iwe na tractor hata kama halimilikiwi na serikali, yapo maeneo mengi kilimo chao kinahitaji best practices zaidi kuliko mbolea. ebu anzeni na kuongeza only 30% ya arable. serikali isifanye kila kitu na ijipunguzie mambo ya uzalishaji iachie watu binafsi.
 
Arable land zipo na unakuta kijijini ardhi inayotumika kwa kilimo ni 20% tu, kila kata iwe na tractor hata kama halimilikiwi na serikali, yapo maeneo mengi kilimo chao kinahitaji best practices zaidi kuliko mbolea. ebu anzeni na kuongeza only 30% ya arable. serikali isifanye kila kitu na ijipunguzie mambo ya uzalishaji iachie watu binafsil

Ebu achana na hizi mambo huu ndio upotezaji wa pesa, angalia watu binafsi wanalima na kufuga jifunzeni kutoka kwao kwanza zipo quick win, haya mengine ni siasa zisizo na tija miaka nenda miaka rudi.
Arable land zipo na unakuta kijijini ardhi inayotumika kwa kilimo ni 20% tu, kila kata iwe na tractor hata kama halimilikiwi na serikali, yapo maeneo mengi kilimo chao kinahitaji best practices zaidi kuliko mbolea. ebu anzeni na kuongeza only 30% ya arable. serikali isifanye kila kitu na ijipunguzie mambo ya uzalishaji iachie watu binafsi.
Lazima uliangalie kwa jicho la kipekeee kundi kubwa la wakulima wadogo wadogo ambao nao unapaswa uwasaidie kuwainuib,kwa kuhakikisha kuwa pembejeo za kilimo hasa mbolea zinapatikana kwa Bei nzuri

Ndio maana Sasa unaona serikali ikifanya juhudi za kulikwamua kundi hili huku pia ikiweka mikakati ya kibajeti

Katika kilimo Cha umwagiliaji, Nazani uliona katika bajeti ya kilimo kuwa serikali inataka kutenga maeneo kwa ajiri ya shughuli hiyo

Serikali yetu imedhamilia kuona kilimo kinakuwa Ni biashara itakayo mnufaisha mkulima, uchumi mzuri Ni ule unaogusa maisha ya waliowengi, Na kilimo ndio secta iliyobeba watu wengi, Hivyo kwa kuigusa na kuinua inakuwa umegusa na kuinua maisha ya watanzania walio wengi
 
Ndugu zangu Kuna kipindi fulani ilikuwa ukisikia kuwa kesho katibu mkuu wa Chadema Mh. Dr Slaa atakuwa na mazungumzo muda fulani, ni kama nchi ilikuwa inasimama. Vyombo vyote vya habari vilikuwa vinafika hata kabla ya muda husika, kila mtanzania alikuwa anatega sikio kusikia nini kitakacho zungumzwa.

Kila Kona ya nchi ilikuwa inakuwa ni gumzo lisilo pimika, ilikuwa ni kana kwamba Rais wa marekani anakuja kutolea tamko Tanzania juu ya kuuwawa kwa Osama bin laden. Watu walikuwa hawatulii walipokaa, wasio na TV walikwenda hata vibanda umiza kuchungulia ilimradi tu asijesubili kusimuliwa.

Hoja nzito nzito zilishushwa huku zikinogeshwa na vijana wa Redbriged waliokuwa wanakaa nyuma ya viongozi wao. Sisi vijana wa CCM wakati mwingine tulikuwa hatuelewi tutajibu nini juu ya nondo zinazokuwa zimeshushwa, hivyo tulibaki tukirusha rusha miguu wakati tukisubili akina Mh. Nape walete silaha za hoja kujibu vijana wenzetu wa upinzani huku site.

Hata mikutano tu ilikuwa ukisikia Dr slaa anakuja Mbeya mjini kwenye uwanja wa Rwanda Nzovwe maarufu kama CCM, jiji lote lilikuwa linasimama, shughuli zote zilikuwa zinasimama. Mimi nilikuwa nikitoka shule Sekondari ya Ivumwe, nilikuwa hata sipiki chakula zaidi ya kwenda mkutanoni ili nijuwe wanasema nini hawa watani zangu.

Alikuwa akija anapokelewa kama Rais wa nchi, shangwe kubwa hata uwe mwanjelwa unasikia. Ilikuwa ni Kama nchi inakwenda kupinduliwa kwa maandano. Ilikuwa ni kama wananchi wote wapo upinzani japo wa CCM tuliogopa hata kuvaa sare kuepuka kupigwa. Ilikuwa ukisikia "PIPOZ" watu walikuwa wanaitikia utazan wanataka kulia jinsi walivyo na hasira!

CCM fundiii bwana, CCM chama kubwa, CCM Ina mbinu hadi za reserve, CCM ndio chama kiongozi, CCM ndio mkombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, CCM ndio chama Cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Unajua nini kilifanyika upinzani wakapewa Mh. nguli wa mikakati ya kisiasa Mh. Edward Lowasa waliyemtukana kwa miaka takribani nane kuwa ni fisadi? Ilikuwa ni kwa ajili ya kumsafisha na kumpaka mafuta hadi apendeze.

Hapo ndioo tukaanza kuona mvurugano ndani kwa ndani. Mara Dr slaa akatimka kwa kusema hawezi kazi hiyo, mara Mnyika akazira, mara sijui Mh Sanaa havai makombati yao, Mara huku Askofu Gwajima akasema alikuwa mshenga, mara sijuw nini yaani ikawa furu michanganyo.

Baada ya hapo akaingia Dr John Pombe Magufuli kama Rais wa nchi. Aliwakaba hadi vivuli vyao wakawa wanavikimbia. Hapo ndio ikajulikana pia nani ni mpinzani na nani ni mpinzani njaa. watu waliunga mkono juhudi kama hawana akili nzuri.

Baada ya hapo ndio akaja mama yetu kipenzi cha watanzania, mzalendo wa kweli, mwenye maneno ya upendo na faraja, mwenye tbasamu la upendo na ukarimu, aliyejaa hekima na busara katika kifua chake, mwenye moyo wa huruma na upendo akaanza kusuka serikali yake hatua kwa hatua. Watu wakaanza kushituka maana hawakutegemea jinsi anavyoendesha nchi kwa weledi na utumishi uliotukuka.

Hapa ndio ikawa mwisho na hitimisho la upinzani hapa nchini, kwa sasa hakuna mwananchi atakuelewa juu ya upinzani. Kwa sasa wananchi wapo na mama, kwa sababu mama yetu amewafanya watu wawe na iman naye. Anaendesha nchi kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na utawala bora.

Utawaambia nini wakulima juu ya mama Samia wakati wanaona juhudi za mama katika kilimo hasa baada ya kutoa ruzuku kwenye Wizara ya Kilimo takilibani billion mia hamsini na kumkabidhi kijana wake Mh. Hussein Bashe ili asimamie? Utawaambia nini wananchi wakati wanaona mama sasa ameweka elimu bure hadi kidato cha sita? Utawambia nini watu wakati wanaona vyumba vya madarasa, vituo vya afya, zahanati na maji vikisambazwa kila kona ya nchi?

Hakuna anayeweza kukuelewa ukimsema vibaya mama yetu kipenzi mama Samia Suluhu Hassani kwa utendaji wake bora wa kazi. Huku Songwe ni mama anaupiga mwingi na wala huwaambii na wakakuelewa habari za upinzani.

Nakupenda CCM na nitaendelea kuwa mwana CCM. Hapa ni Tanzania na siyo Kenya, hata tuwape upinzani wasimamie uchaguzi bado CCM itashinda tu. CCM ndio tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo. Upinzaani asante sana kwa kumuunga mkono mama yetu na msisite kushirikiana zaidi na zaidi na mama yetu kuijenga nchi yetu maana upinzani siyo uadui.

Kazi iendelee, sote tumuunge mkono Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassani katika kuijenga Tanzania mpya.​
Anaitwa Rais wa Ma bii,yaani kamwaga mabilioni kwa mabilioni haijapata kutokea..

Kila sekta na watu wanaona.
 
Kabisa kila eneo kaligusa na kuliwezesha
By 2025,Nchi hii itakuwa mbali Sana maana seems SSH anajua kwamba bila pesa Nchi haisogei na anajua kuweka mipango ya kupata pesa na wapi pa kuzitumia..

Pesa zinazotumika kwenye Mikoa ni nyingi sio mchezo across sectors japo kwenye michezo amekacha ujenzi wa viwanja vikubwa.

Tutakuwa mbali Sanaa kiuchumi chini ya mh Rais mama Samia suluhu Hassani maana Amedhamilia kuijenga nchi hii bila kumuacha mtu nyuma

Anajenga uchumi jumuishi unaomgusa kila mtu, Uongozi wake utaacha Alama kila eneo na Atakumbukwa Sana na watanzania maana amekaa katika mioyo yao,
 
This is how is happening 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220811-125758.png
    Screenshot_20220811-125758.png
    133.8 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220811-125427.png
    Screenshot_20220811-125427.png
    114.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom