Utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia umedhoofisha upinzani Tanzania

Jamaa unamajibu ya kiserikali mno! ebu tumia akili kidogo hapa tunakwambia hilo ulilokuwa nalo sio jibu pekee, fikiria wengine wanafanyaje katika kutatua changamoto. Majibu matamu ya serikali yanachelewesha kuwa open minded haPA upate mawazo mbadala.
Tunataka mikakati isiyokuwa ya kibajet, tunakwambia huku kwetu maeneo ya kulima ni makubwa ila ni sehemu ndogo tu watu ndio wanaweza kuyalima, huko nyuma sababu ilikuwa soko na post harvest handling. kama maghala yapo watu wahamasishwe na kulima zaidi ya walivyolima msimu uliopita. Pembejeo hapa isiwe mbolea tu tuzungumzie tunalima kwa majembe au tunaengage wadau waweke tractors serikali ni guarantees tu inatosha.
Serikali wala isitenge maenea mapya tutafute productivity kwa haya tuliyonayo. Access ya mbegu bora, ni kufacilitate suppliers wafike mpaka grass roots, serikali ijifunze kwa mabodi ya tumbaku.
Serikali inazungumzia Macro wewe sasa zungumzia Micro, nyie wasemaji wa serikali mmekuwa wengi mno, badilikeni kuwasemea wananchi ili tabu zao ndio ziwe fursa kwa serikali. sasa kama mtang'ang'ana kusifia serikali tu basi wengi wataendelea kuwa maskini. ndio mana tunataka upinzani na setor binafsi zaidi.
 
Ndio Kazi ambazo Rais Samia na Waziri wa Kilimo wanazifanyia Kazi..

Kwani hujui kwamba soko la soya limefunguliwa China? Hujui kwamba China imetoa clearance ya Kampuni za Tanzania 52 ku export mazao mbalimbali zikiwemo nyama?

Usipofuatilia hutojua kitu..Safari yetu ya Ajenda 1030 inatakiwa kitufikisha hapa come 2025πŸ‘‡
 

Attachments

  • Screenshot_20220810-220410.png
    161.8 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220810-220528.png
    38.3 KB · Views: 6
Soya upeleke china wakati tunatumia soya nyingi kutoka Malawi na Zambia, soya inayozalishwa haitoshi, epuka taarifa za kusaign mikataba na kufungulia makongamano. wenzio tuko site. Soya tunaagiza kutoka zambia na malawi. Ebu acheni hizi politike na kudanganya watu, safari ya ajenda 1030 ilianza na kilimo kwanza sie tunataka urudi kuyatumia ya kilimo kwanza 1030 bado kidogo mno bado mnambwela.
Sasa wewe unalipwa humu kuandika propaganda, sema ukweli tunufaike wote
 

This is how is happening πŸ‘‡
Hakika mama yupo kazini hapoi Wala hapumziki, Anahitaji kuona kazi inafanyika na matokeo Bora yanapatikana kwa manufaa ya watanzania
 
Hakika mama yupo kazini hapoi Wala hapumziki, Anahitaji kuona kazi inafanyika na matokeo Bora yanapatikana kwa manufaa ya watanzania
Hii ataipata vizuri kama mtampa na dawa chungu pia, hatujawakatalia ila tunawaambia nyie mataga na changamoto pia mziseme na muwaache wengine wanaona tofauti nao waseme. Mmetughalimu sana wakati wa jiwe sasa mama nae aone tofauti akiyarekebisha sasa atafanikiwa sana.
 
Mijizi ya kura bana, yaani umejiunga hapa jukwaani mwezi uliopita, ili kuleta propaganda ukidhani ndio utaokota watu vibaya sana.

Tindo vumilia Nyundo ifanye kazi yake
 
Changamoto zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi mkuu, Ndio maana unaona mawaziri wakiongozwa na mh Rais wapo bize kushughulikia na kutoa majibu kwa Kero za wananchi

Ndio maana unaona Rais yupo huku makamu wa Rais pale Waziri mkuu kule mawaziri huku na huko, huku wote ajenda ikiwa Ni kuwatumikia wananchi kwa kufika katika maeneo yao

Nawakiondoka huko site wanaacha maagizo kwa ma RC,RAS,DC,DAS Na ma DED, na wanajuwa wanafuatilia utekelezaji wa maagizo yao, kwa ufupi Ni kuwa mama na Serikali yake yupo kazini muda wote
 
Endelea kubwabwaja ujinga utaishia hivyo hivyo..

Kinachoamua wapi zao liende ni Bei ya zao husika..

Kwa taarifa yako ,Wachina wanalima soya ya exports zaidi ya hekta laki 200 kule Chunya na Songwe..

Kaa usichangamkie fursa subiria utaletewa nyumbani kwako, endelea kuita propaganda.
 
Soya inatoka zambia na Malawi unafikiri ni uwongo, inayozalishwa haitoshi we umri huu nani anamletea mwenzie???
 
Sawa Mwanaccm mwenzangu.
Unaweza kunitajikiwanda kimoja tu ambacho chama chetu au serikali kilichojengwa na kinazalisha ktk hii miaka mitano.
Kwani unavyokuja na hoja na sisi kama chama tawala tuwe na pa kujibanza sio kuja kuja za kuamsha watu ili wapate hoja za kuhoji ndani ya chama na serikali kwani tutazidi kuonyesha udhaifu wa chama.
Ndo maana Mzee wetu Msuya ametuasa kwani tujijue tuko wapi kisiasa.
Asante
 
Sifa ni kwake eeh Yesu kristu. Uliotukuka πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ au basi huu uzi wako ndo umenifanya nikujue n mtu wa namn gan
 
Kazi ya serikali siyo kujenga viwanda Bali Ni kuweka mazingira mazuri yatakayo vutia wawekezaji watakao Jenga viwanda hapa nchini na kutoa ajira kwa watanzania

Ukitaka kujuwa wawekezaji wangapi wamewekeza katika viwanda hapa nchini embu fuatilia taarifa za TIC,
Siyo
 
Mijizi ya kura bana, yaani umejiunga hapa jukwaani mwezi uliopita, ili kuleta propaganda ukidhani ndio utaokota watu vibaya sana.
Ukiandaliwa uchaguzi huru Kama Kenya, yaani Polisi wasionekane kwenye vituo vya kupigia kura, mawakala wasizuiliwe, majina ya wagombea yasikatwe, kura zihesabiwe hadharani huku zilipigwa picha.....loo, mbona CCM mapema tu asubuhi hawapo.
 
Ukiandaliwa uchaguzi huru Kama Kenya, yaani Polisi wasionekane kwenye vituo vya kupigia kura, mawakala wasizuiliwe, majina ya wagombea yasikatwe, kura zihesabiwe hadharani huku zilipigwa picha.....loo, mbona CCM mapema tu asubuhi hawapo.
Hakuna chama chenye uwezo wa kuitikisa CCM kwa Sasa hapa Tanzania kisera hata kiajenda,
 
Stupidly sense you have said.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…