Utendaji Mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma; Rais Samia tupia jicho lako hapo

hakuna cha tume wala babake nani serikali yote pamoja na vyombo vyake ni uharo mtupu.
 
Hii TUME inayofanya mambo ya hovyo ndio iliyoaminiwa na Rais kuwa hategemei kubadilisha uamuzi wao. Kwa maana hiyo Rais amewaamini watu wa TUME wasiowasafi kimaadili na kimaamuzi. Huu ni wakati wa Rais kuifutilia mbali TUME hii ili kuondokana na uozo wake.
 
Lisemwalo lipo,Kama hakipo linanyemelea.Haki inayocheleweshwa ndiyo haki inayonyimwa.Tume ijitafakari na iondoshe malalamiko au upungufu uliopo hivi sasa,waadhirika wanateseka.Kama kazi zimewaelemea ombeni kibali Cha ku review ikams(establishment) ya taasisi yenu na kuomba kuongeza watumishi ili kuleta ufanisi.
 
Na sio kitu cha kweli (halisia) kuwa wana rufaa nyingi sana, watumishi wanaofukuzwa kazi serikalini ni wachache sana kwa mwaka. Mfano, mahakama, unakuta mwaka mzima hakuna hakimu aliyefukuzwa kazi Tanzania nzima. Halmashauri ya Wilaya yenye watumishi 2500, mwaka mzima wanaweza kufukuzwa kazi watumishi wasozidi 3 kwa mwaka. Halmashauri zipo 152 kama sikosei, kwa hiyo ni rufaa chini ya 600 zinazokwenda TUME kwa mwaka, ukijumlisha na za taasisi nyingine za umma unakuta no rufaa labda 1000 kwa mwaka. Ukigawa kwa wafanyakazi 35 wa Tume unakuta kila mmoja atafanyia kazi rufaa 29 kwa mwaka mzima wenye siku 365 wakati hakimu mmoja wa mahakama ya mwanzo ana jukumu la kusikiliza kesi 70 sijui kwa mwaka na kesi zinaenda. Sasa hao tume huo mzigo wanautoa wapi?

Wanataka kutuaminisha kuwa taasisi za umma zinafukuza sana watumishi kiasi rufaa ni nyingi sana?
 
Mpigie simu kabisa maana naona unateseka sana.

Unahisi.kwa mfano bado ningekuwa Tume ningekaa natafakari rufaa yako tu kati ya rufaa za watu maelfu ambao tayari wana vielelezo.

Sikia nshakuambia sio.msemaji wa Tume so usinikoti pambana na hali yako
kama mrufani akichelewa kupeleka rufaa yake ndani ya siku 45 inatupiliwa nje kwanini mwajiri nae akichelewa ndani ya siku 14 rufaa isiamuliwe kutumia vielelezo vya upande mmoja? kama huo muda upo kisheria?
 
kama mrufani akichelewa kupeleka rufaa yake ndani ya siku 45 inatupiliwa nje kwanini mwajiri nae akichelewa ndani ya siku 14 rufaa isiamuliwe kutumia vielelezo vya upande mmoja? kama huo muda upo kisheria?
Sio lazima mrufani akichelewa kupeleka rufaa yake inatupiliwa mbali soma Reg.61(4). Mamlaka ya Nidhamu sio kila mara wanachelewa kuleta vielelezo. Ukisoma ufafanuzi wa Kaim Katibu amesema "FIRST IN FIRST OUT"

Pia kumbuka vikao vya TUME vinakaa kila robo mwaka kisheria maana yake baada ya miezi3. kwa mfano rufaa imemalizika kuchambuliwa leo na kikao kimeisha jana, itasubiri next kikao. Kulikuwa na mrundikano mwingi wa kesi lilipoisha zoezi la uhakiki wa vyeti.
 
Kwanza kubalini customer care yenu hasa kwenye upande wa simu ni mbaya mnoo halafu pili mnatakiwa mbadilike badala ya kutumia posta muendane na technology inavyoenda mtumie email badala ya kumsumbua mrufani kutembelea posta kuangalia barua au aweze kupata alert kuna barua imepelekwa posta kupitia e-mail halafu kutokana na mabadiliko makubwa kwenye TEHAMA tume wanatakiwa wawe na mfumo ambao kila mrufani atapewa id yake ili aweze kulogin na kuangalia status ya rufaa yake hii itadumu mpaka rufaa yake itakapofikia mwisho. kama idara ya Tehama imeshindwa kulifanyia kazi nendeni e-government kwa msaada zaidi au njoo huku private sector tuwasaidie acheni kuwapeleka watu kizamani kwenye zama hizi ambazo taarifa inapatikana kwenye vidole
 
Mkuu e-goverment 90% ya Serikali na ASASI zake bado hawajaingia, anyway ni wazo zuri kama ukilifikisha kwa wahusika.

Email kila mtumishi anayo ila tatizo hairuhusiwi kwa namna yoyote MCHAMBUZI KUWASILIANA NA MRUFANI DIRECT.

EMAIL YA KATIBU ANAFUNGUA PS WAKE unadhani atajibu ngapi TZ nzima? tuongee reality.

Barua IM SURE UKIANDIKA LAZIMA UJIBIWE
 
Huyu Msemaji wao humu anasema rufaa nyingi ziliongezeka baada ya wale wenye vyeti feki kutimuliwa kwahiyo nina imani kwa sasa hivi idadi ya wanaokata rufaa itakuwa imepungua sana
 
Mimi sizungumzii kutuma rufaa kupitia e-mail hapana !!! ila muwe mnatoa majibu ya rufaa kupitia e-mail badala ya barua au mtumie vyote viwili kumrahishia mrufani badala ya kumaktisha tamaa ya kwenda posta mara kwa mara kwenda kuangalia majibu ya rufaa yake

Halafu wewe ndiye unatakiwa kuyafikisha kwa wahusika
 
They operate like an old school!!πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Wanazungumzia FIRST IN FIRST OUT badala ya kuagalia Sheria na Kanuni vinasemaje kuhusu suala la muda, halafu anaeongea hilo eti ni Kaimu Katibu, bure kabisa!!!. Hawa Tume wanacheza na haki za watumishi!!!
 
Hilo hata kama sifanyi kazi pale tena ila naona HALIWEZEKANI.
GOVERNMENT WORKS ON PAPER.


KUHUSU BARUA KUCHELEWA KUMFIKIA MRUFANI HATA BAADA YA KIKAO IPO HIVI:-
NAKALA ZA RUFAA ZINAENDA OFISI KAMA 6
1.MRUFANI
2 MAMLAKA YA NIDHAMU
3. RAIS/IKULU
4 UTUMISHU
5. TAMISEMI
6. RAS
HIZI ZOTE ZINATAKIWA KUSAINIWA ORIGINAL NA PIA LAZIMA ASAINI MTENDAJI MKUU PEKE YAKE.

IMAGINE KIKAO KIMEAMUA RUFAA 100 NA KILA RUFAA MTU MMOJA ASAINI NAKALA 6 MAANA YAKE ATASAINI BARUA 600 BAADA YA KUHAKIKI MAUDHUI YAKE KAMA YAPO KAMA YALIVYOAMULIWA (KUJIRIDHISHA)

KUMBUKA HAPO BADO ANA DAY TO DAY ACTIVITIES

VUTA SUBIRA HAKI YAKO INAKUJA TU
 
Waache uvivu kuhakiki barua 600 shida ni nini kama wanaona ni kazi waachie ngazi wapo watu wachapa kazi.
 
Waache uvivu kuhakiki barua 600 shida ni nini kama wanaona ni kazi waachie ngazi wapo watu wachapa kazi.
Huwezi kuelewa kwa kuwa we ni muhanga. Toka kidogo kwenye lindi la hasira zako halafu weka mbele wako kitabu chenye kurasa 600+ halafu usome kila page na kusaini. Hapo bado una majukumu chungu mzima utaelewa.

NB. sikulazimishi kuelewa na kama nlivokuambia mwanzoni kama una maswali nenda pale Kivukoni, Luthuli st. Kiwanja Na.10 kamuone Katibu uzuri haitaji Apointment kuonana na mteja. atakufafanulia. Uzi uliletwa ili Rais auone nadhani ameshauona, usiniulize mimi maswali zaidi nlijitolea kuelewesha baadhi ya mambokutokana na uelewa wangu wa kufanya kazi pale matokeo mmenigeuza mimi TUME.
 
Kwa nini usaini barua 100 kwa siku? kwa siku zinaweza kuwa drafted barua za watu 30 unaedit zikiwa vizuri una wa- cc wahusika unaprint 30 x 6 = 180 shida nini hapa baada ya wiki imemaliza. kwani anadraft mwenyewe? kuna wakuu wa idara na vitengo. Kwa nini mambo rahisi mnataka kuyafanya magumu. Huo ni UKILAZA!!!
 
Lingekuwa rahisi Ungekuwa kazini saivi pimbi wewe.

Ufukuzwe kazi kwa upumbavu wako halafu ufundishe kazi waliopo kazini pathetic!!

Nakuelekeza kwa adabu ila unaonekana kichwa maji.

Print uzi huu ukakabidhi pale geti la ikulu au peleka platforms zingine liende viral [emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
 
Kama wewe sio mhusika wa Tume kwa nini unakuwa kimbelembele hapa kila kinachotumwa unajibu. Nyamaza basi.
 
Mbona matusi ndugu kuwa mstaarabu. Tujadili kwa hoja na sio matusi au hasira, wewe kila mtu hapa unamtukana kwa nini uko hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…