EINSTEIN112 ngoja nikufundishe kidogo namna ya kusoma sheria (Act), itakusaidia kuelewa mambo na sio kubisha bisha bali kama utabisha basi itakuwa ni kwa hoja. Kama bado unafanya TUME ya Utumishi utaitumia fursa hii kuwaambia makamishna na watumishi wenzako kuwa Tafsiri sahihi ya sheria ni hii na sio hivyo mnavyoelewa. Darasa linaweza kuwa refu lakini SOMA uelewe maana ni muhimu kwako na kwa wenzako mnaoamua hatima za maisha ya watu kwa nguvu za kisheria mlizopewa (ingawa mnazitumia vibaya).
IPO HIVI
CMA ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kusuluhisha migogoro itokanayo au ihusianayo na ajira mwajiri na mfanyakazi). Mamlaka hayo CMA imeyapata kupitia kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Mahakama/Taasisi za Kazi (The Labour Institutions Act Cap 366 RE 2019)
View attachment 1905293
Hapo unaona kabisa kuwa
CMA ina mamlaka ya
kusuluhisha mgogoro wowote wa kikazi unaowasilishwa mbele yake kwa Sheria yoyote ya mambo ya ajira (
Sheria ya utumishi wa Umma ikiwa ni mojawapo ya sheria za kazi).
Sheria ya Ajira na mahusiano kazini (the
Employment and Labour Relations Act CAP 366 R.E 2019) kupitia
kifungu cha 2 (1) inaeleza vyema kuwa
ITATUMIKA kwa wafanyakazi wote wa
sekta binafsi na
wa Serikali isipokuwa wachache wa serikali ambao wameainishwa. Wakati kifungu cha
34A cha
Sheria ya Utumishi wa Umma kimeeleza kuwa unpotokea mkanganyiko kati ya Sheria ya Utumishi wa Umma na Sheria nyingine inayohusu utumishi wa Umma ( Sio ELRA), basi Sheria ya utumishi wa Umma (
CAP 298 R.E 2019) itakuwa na nguvu dhidi ya nyingine (ya serikali). Kwa lugha rahisi ni kwamba, Sheria ya Utumishi wa Umma haina nguvu kuzidi Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (hata kwa watumishi wa Umma).
View attachment 1905296
RUFAA ZA WATUMISHI WA UMMA
Pale ambapo mamlaka ya nidhamu inakuwa imetoa adhabu (maamuzi) dhidi ya mtumishi wa umma kutokana na nguvu iliyopewa na sheria basi mtumishi huyo anaelekezwa kupitia
Kifungu cha 25 (1) (b) cha
Sheria ya utumishi wa umma kukata
Rufaa kwenye
TUME ya UTUMISHI WA UMMA.
Msisitizo,
Ni pale tu mamlaka ya nidhamu inapokuwa imetekeleza mamlaka yake kisheria kwa kutoa adhabu kwa mtumishi kama kumshusha cheo, kumshusha mshahara au kumfukuza kazi ndio mtumishi anaweza kukata Rufaa, kama hakuna adhabu iliyotolewa mtumishi hawezi kukata Rufaa.
View attachment 1905301
TUME KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WATUMISHI WA UMMA
Tume ya Utumishi wa Umma
haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza na kutoa maamuzi ya Malalamiko ya Watumishi wa Umma. TUME haina uhalali wa kusikiliza migogoro mibichi (
original jurisdiction) isipokuwa inaweza kusikiliza migogoro katika hatua ya Rufaa tu (
Appellate Jurisdiction) kama ilivyoelezwa katika
Kifungu cha 10 (1) (d) cha
Sheria ya utumishi wa Umma. Kwa hiyo kinachofanyika sasa TUME kusikiliza Malalamiko ya watu pale ambapo mwajiri anakuwa
amemkosea au
anamuonea mtumishi. Mamlaka haya yapo CMA tu kama nilivyoeleza awali na TUME imeyapora kutoka CMA kwa kisingizo cha mabadiliko ya Sheria ya utumishi wa Umma, kitu ambacho sio kweli, tutakisoma kifungu hicho wanachotumia TUME na ambacho hakiwapi mamlaka hayo. Kazi za TUME ni hizi hapa;
View attachment 1905302
JE NI LAZIMA KISHERIA KWA MTUMISHI WA UMMA KUEXHAUST LOCAL REMEDIES KABLA YA KWENDA CMA?
Jibu ni inategemea na aina ya mgogoro.
Kama kinacholalamikiwa ni
maamuzi ya mamlaka ya nidhamu basi mtumishi wa Umma anapaswa kukata Rufaa TUME na baadae kama hajaridhika kukata rufaa kwa Rais na kisha kama hajaridhika na maamuzi ya rais kurudi Mahakama Kuu kwa Judicial Review, hii ndio inaitwa exhaustion of local remedy. Lakini kama mgogoro ni malalamiko juu ya uonevu wa mwajiri basi mtumishi anaruhusiwa kwenda moja kwa moja CMA bila kupita popote sababu CMA ndicho chombo pekee chenye mamala ya kusikiliza migogoro ya kazi/ ajira. Hana local remedy anayotakiwa kuexhaust.
JE, MABADILIKO YA SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA MWAKA 2016 YALIHUSU WATUMISHI WOTE?
Jibu ni HAPANA, mabadiliko hayo ya kuwataka watumishi waexhaust local remedies yaliwahusu watumishi wa umma walio katika ngazi ya OPERATIONAL SERVICE, yaani watumishi wasio na digrii. Ili uelewe vyema jambo hili, unatakiwa kusoma Sub Heading ya Kifungu cha 32 na 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma, kimeandikwa (c) Operational Service. Kwa hiyo Mabadiliko ya Sheria mwaka 2016 yaliongeza
Kifungu 32A kuwahusu Watumishi wa Umma ambao wapo katka kundi la
Operational Service tu na sio wengineo.
BAHATI mbaya, Mawakili wa Serikali wamekuwa
wakiipotosha Mahakama kwa kuwaambia kifungu hicho
kinahusu waumishi wote wa Umma jambo ambalo
sio kweli. Wamekuwa wakiweka Mapingamizi ya Kisheria kila mara mtumishi wa umma anapofungua CMA mgogoro usiohusu adhabu za mamlaka ya nidhamu wakimtaa aexhaust local remedies. Majaji na Waamuzi wa CMA nao wamekuwa wakiingia mtego huu wa mawakili wa serikali, labda kwa kutokusoma kifungu husika au kwa kukisoma vibaya. Maofisa ambao sheria ya utumishi wa Umma imewatambulishakuwa ni wale walioajiriwa kwa digrii (shahada) kama ngazi ya mwanzo kabisa ya ajira zao mfano maafisa kilimo, maafisa watendaji wa Kata, maafisa ugavi nk wanaitwa
AFISA. Msingi wa kuongeza Kifungu hiki cha 32A ilikuwa ni kuwazuia watumishi wa Operational Service kwenda CMA moja kwa moja kwa kuwa
Sheria ya Utumishi wa Umma hiyohiyo kupitia
Kifungu cha 32 iliwaelekeza kuwa watumishi hao wanatawaliwa ama wanaongozwa na Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini.
View attachment 1905307
Kwa hiyo, TUME ya Utumishi wa Umma imekwa ikitekeleza jambo amabalo haina mamalaka nalo la kusikiliza malalamiko na kuyatolea uamuzi.
Natumai
EINSTEIN112 na wenzako mtakuwa mmenielwa vyema na mmejifunza.
View attachment 1905300