EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Sio kweli ukishindwa TUME unakata RUFAA kwa RAIS ukiona umeonewa unakata rufaa MAHAKAMA KUU.Majibu yanayotolewa na Tume kwa rufaa ya Mtumishi ukiangalia ni kama wameandaliwa na Mwajiri husika wao ni kusaini na kupiga mhuri tu. Kugundua hujuma hii iko wazi sana sema tu wamejipanga kiasi kwamba bahasha zinatembea kwa wahusika wote.
We KIlaza Subiri POsho tu huna unachowaambia watu waliodhulumiwa haki zao kwa taarifa yako Customer care yenu ingekua nzuri hata mngekua mnatoa majibu ya uongo wangeridhika, you dont have a single point kuwaaminisha waathirika huo utendaji wenu fake, nasema kwa ujumla nyie ni Crap, waambie waliokutuma kuna jamaa yuko ughaibuni huko hataki kabisa kuelewa TUME YA UTUMISHI WA UMMA NI JANGA KWA WATUMISHI TANZANIA. mara uwatukane badala ya kuwaelimisha , yaani nyie watu mliopata kazi kimagumashi mnashida sana , narudia tena wewe ni masikini tu kama watumishi wenzio period.Huko juu nimetoa ufafanuzi wa PROCESS ya rufaa kuchambuliwa.
Labda nirudie
Ofisa atachambua rufaa kwa kujibu HOJA zako vs majibu ya mamlaka ya nidhamu vs sheria, kanuni, nyaraka, taratibu, miongozo, nk
Akimaliza uchambuzi wake unapitiwa na kikao cha IDARA wanasoma kila HOJA ilivyochambuliwa, watarekebisha kama kuna MAKOSA.
Baadae huo uchambuzi utapitiwa na kikao cha MENEJIMENTI ya TUME ambayo ina wabobezi za sheria za kazi watarekebisha kama kuna makosa.
Mwishoni ndio inaenda TUME.
NADHANI UMEELEWA ILIVYO NGUMU OFISA KULA RUSHWA AU WEWE KUONEWA
CHECK AND BALANCE ni kubwa mno
So huwezi kuonewa wala kupendelewa
Majibu ya kinadharia tu uhalisia wa utendaji wa TUME ni aibu. Serikali ikiamua kuichunguza mengi sana na ya kustaajabisha yatagundulika. Kwa utendaji huo ni bora ivunjwe maana inatumia fedha za umma bila ufanisi na kuendekeza rushwa kwa kushirikia na Waajiri ili kudhulumu haki za wafanyakazi/watumishi.Huu ndio tunaita "upotoshaji"
Tume ina maafisa wasiozidi 35
Wanashughulikia rufaa za watumishi wooote wa umma ukiondoa walimu, polisi, magereza, na wanajeshi
Unajua workload ya rufaa au unalalama tu.
===
Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma
NA MWANDISHI MAALUM-PSC
Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma (Sura ya 298 marejeo ya mwaka 2019), pamoja na majukumu mengine Tume ina jukumu la kupokea na kushughulikia rufaa kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Nidhamu ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao, kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (1) cha Sheria hii na Kanuni ya 60 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.
Tume ya Utumishi wa Umma inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” tarehe 12 Agosti 2021 kama ifuatavyo:-
1. Kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume inaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe 6 ambao huteuliwa na Rais ambao pamoja na majukumu mengine wana jukumu la kisheria la kutolea uamuzi rufaa na malalamiko yanayowasilishwa mbele ya Tume. Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 14(1) na (2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume ina Katibu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu. Katibu na Wasaidizi wake (Sekretarieti) ndio watendaji wa kazi za kila siku katika Tume ya Utumishi wa Umma ambao wameteuliwa baada ya kukidhi sifa na vigezo katika nafasi walizo nazo.
2. Pamoja na Sheria zilizopo, Tume inashughulikia rufaa kwa mujibu wa Mwongozo Kuhusu Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2009 ambapo rufaa hupokelewa, husajiliwa, huchambuliwa na kupitiwa na Kikao cha Menejimenti na hatimaye kuwasilishwa mbele ya Tume kwa uamuzi. Hatua ya mwisho ni Mrufani na Mrufaniwa kujulishwa kwa barua juu ya uamuzi unaotolewa na Tume. Utaratibu huu umewekwa ili kuimarisha utendaji kazi, kudhibiti upendeleo, rushwa na kuimarisha utoaji wa haki. Aidha, elimu kuhusiana na utaratibu huu imekuwa ikitolewa kwa wadau kupitia majukwaa mbalimbali.
3. Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko haitoi uamuzi kwa shinikizo au ushawishi wa Mwajiri au Mamlaka ya Nidhamu yoyote ili kuwakandamiza watumishi wasipate haki zao. Tafsiri kuwa Tume ni chombo cha kulinda maslahi ya Waajiri na Serikali. Tume inapenda kuufahamisha umma kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.
4. Rufaa na malalamiko yanayopokelewa Tume yenye vielelezo vilivyokamilika ndio yanayoshughulikiwa na kutolewa uamuzi kwa kadri yalivyopokelewa (First in, First Out).
5. Tume ya Utumishi wa Umma, inaomba umma kuupuuza upotoshwaji huu uliotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” na inatoa wito kwa umma na wadau wote kuwasiliana na Tume kwa ufafanuzi, maoni au suala lolote kuhusu Tume kupitia simu namba 0738166703, 0733 005 974 na barua pepe, secretary@psc.go.tz.
Imetolewa na:
John C. Mbisso
KAIMU KATIBU
TUME YA UTUMISHI WA UMMA
DAR ES SALAAM
13 AGOSTI, 2021
Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma
www.diramakini.co.tz
Punguza MIHEMKO utaelewa nlichoandikaWe KIlaza Subiri POsho tu huna unachowaambia watu waliodhulumiwa haki zao kwa taarifa yako Customer care yenu ingekua nzuri hata mngekua mnatoa majibu ya uongo wangeridhika, you dont have a single point kuwaaminisha waathirika huo utendaji wenu fake, nasema kwa ujumla nyie ni Crap, waambie waliokutuma kuna jamaa yuko ughaibuni huko hataki kabisa kuelewa TUME YA UTUMISHI WA UMMA NI JANGA KWA WATUMISHI TANZANIA. mara uwatukane badala ya kuwaelimisha , yaani nyie watu mliopata kazi kimagumashi mnashida sana , narudia tena wewe ni masikini tu kama watumishi wenzio period.
Fuatilia post za chini utaelewaMajibu ya kinadharia tu uhalisia wa utendaji wa TUME ni aibu. Serikali ikiamua kuichunguza mengi sana na ya kustaajabisha yatagundulika. Kwa utendaji huo ni bora ivunjwe maana inatumia fedha za umma bila ufanisi na kuendekeza rushwa kwa kushirikia na Waajiri ili kudhulumu haki za wafanyakazi/watumishi.
Hopeless kabisa Tume!!Huko juu nimetoa ufafanuzi wa PROCESS ya rufaa kuchambuliwa.
Labda nirudie
Ofisa atachambua rufaa kwa kujibu HOJA zako vs majibu ya mamlaka ya nidhamu vs sheria, kanuni, nyaraka, taratibu, miongozo, nk
Akimaliza uchambuzi wake unapitiwa na kikao cha IDARA wanasoma kila HOJA ilivyochambuliwa, watarekebisha kama kuna MAKOSA.
Baadae huo uchambuzi utapitiwa na kikao cha MENEJIMENTI ya TUME ambayo ina wabobezi za sheria za kazi watarekebisha kama kuna makosa.
Mwishoni ndio inaenda TUME.
NADHANI UMEELEWA ILIVYO NGUMU OFISA KULA RUSHWA AU WEWE KUONEWA
CHECK AND BALANCE ni kubwa mno
So huwezi kuonewa wala kupendelewa
Hapa tunaongelea uozo wa TUME ambao uko wazi kabisa ukifuatiliwa. Kukata rufaa ni suala lingine. Kwa hiyo TUME wanakula rushwa kumhujumu mtumishi kwa kushirikiana na mwajiri ili Mtumishi akate rufaa kwa Rais? Kwa hiyo TUME ni uchochoro wa kupitia kukata rufaa?Sio kweli ukishindwa TUME unakata RUFAA kwa RAIS ukiona umeonewa unakata rufaa MAHAKAMA KUU.
wote wakuonee kwa lipi hasa ulilonalo?
Kama hufahamu UTARATIBU uliza na so kulalama
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pumbavu fata SHERIA ZA KAZIHopeless kabisa Tume!!
Cha msingi ni kuwa ujumbe umefika kwa Mh. Rais, najua wewe unatetea ugali wako hapo Tume bila kujua kuwa na wewe ni mhanga mtarajiwa, na ndio maana tumesema kuwa hapo Tume wamejaa vilaza na corrupted staff to the maximum!
Koma wewe! unajua namna mkwe alivyomtamuMama apige chini uongozi wote
Huko juu nimeeleza.vizuri sana juu ya CHECK AND BALANCE.Hapa tunaongelea uozo wa TUME ambao uko wazi kabisa ukifuatiliwa. Kukata rufaa ni suala lingine. Kwa hiyo TUME wanakula rushwa kumhujumu mtumishi kwa kushirikiana na mwajiri ili Mtumishi akate rufaa kwa Rais? Kwa hiyo TUME ni uchochoro wa kupitia kukata rufaa?
Ulivyo mweupe kichwani unadhani mahitaji na matumizi yatasubiri ushinde rufaa yako? Chakula nyumbani, ada za shule, kodi ya pango nk yote haya yatasubiri ushinde rufaa yako?We ni boonge la kilaza ukishinda tufaa yako unakula mishahara yako toka umefukuzwa kazi.kwanza ukute hata ajira huna
Suala si utaratibu bali ni uozo wa TUME imekidhiri kwa rushwa. Sijui hawalipwi mishahara hadi wana njaa kiasi hicho. Naamini serikali imepata ujumbe na itaimulika TUME hii inayoiabisha kwa rushwa.Fuatilia post za chini utaelewa
UTARATIBU
Mimi sijawahi kuajiriwa na vilaza wewe , hivi unaongozwa na watu wenye low IQ unajiona unajua , hujui kitu tulia wewe hoja ya msingi hamtakiwi kuendelea kuwepo Serikalini mfutwe tu hamna mnachofanya full stop, nitakupinga usiku na mchana TUME YENU MBOVU, utaratibu gani mpaka wenzenu wafe bila madai yao kushughulikiwa, unashupaza misuli bure kutetea UPUUZI ni sawa na Jitu lianze kutaka kuisafisha Tume ya UCHAGUZI litakua zuzu tu kama wewePunguza MIHEMKO utaelewa nlichoandika
Vinginevyo we ndio unaonekana MPUUZI ndio maana UKAFUKUZWA KAZI mbona wenzako bado wapo kazini we una USPESHELI gani?
Nshakudharau kabisa
Angalia sasa, mnampa kazi bure Mh. Rais kwa utopolo wenu na ucheleweshaji wa bure wa haki ya Mtumishi....Shame on you!!Sio kweli ukishindwa TUME unakata RUFAA kwa RAIS ukiona umeonewa unakata rufaa MAHAKAMA KUU.
wote wakuonee kwa lipi hasa ulilonalo?
Kama hufahamu UTARATIBU uliza na so kulalama
Wewe unatetea ugali ila ukweli unaujua. Mawasiliano ya wajumbe wa TUME na waajiri yanafanyika na hupanga matokeo pamoja. Hiyo ni dhambi kabisa, endelea kujitetea ila mwisho wenu wa dhuluma unakuja.Huko juu nimeeleza.vizuri sana juu ya CHECK AND BALANCE.
UKIAMUA KUBISHANA NAKUACHA
Sikiliza mkuu nshaondoka huko miaka4 iliyopita napajua vemaWewe unatetea ugali ila ukweli unaujua. Mawasiliano ya wajumbe wa TUME na waajiri yanafanyika na hupanga matokeo pamoja. Hiyo ni dhambi kabisa, endelea kujitetea ila mwisho wenu wa dhuluma unakuja.
Mchakato nimekuelezaUlivyo mweupe kichwani unadhani mahitaji na matumizi yatasubiri ushinde rufaa yako? Chakula nyumbani, ada za shule, kodi ya pango nk yote haya yatasubiri ushinde rufaa yako?
Chipime mwenyewe ukilaza wako!
We ni pimbi sana rushwa utatoa kwa watu wangapi??Suala si utaratibu bali ni uozo wa TUME imekidhiri kwa rushwa. Sijui hawalipwi mishahara hadi wana njaa kiasi hicho. Naamini serikali imepata ujumbe na itaimulika TUME hii inayoiabisha kwa rushwa.
Kumbe unaongelea usichokijua utendaji wake karibuni. Basi ndio ujue kwa sasa TUME ni uozo mtupu.Sikiliza mkuu nshaondoka huko miaka4 iliyopita napajua vema
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kama hujawahi kuajiriwa UNALALAMA niniMimi sijawahi kuajiriwa na vilaza wewe , hivi unaongozwa na watu wenye low IQ unajiona unajua , hujui kitu tulia wewe hoja ya msingi hamtakiwi kuendelea kuwepo Serikalini mfutwe tu hamna mnachofanya full stop, nitakupinga usiku na mchana TUME YENU MBOVU, utaratibu gani mpaka wenzenu wafe bila madai yao kushughulikiwa, unashupaza misuli bure kutetea UPUUZI ni sawa na Jitu lianze kutaka kuisafisha Tume ya UCHAGUZI litakua zuzu tu kama wewe