EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Kila ushaelimika najua.Nakuelimisha na kukupa taarifa ili uzinduke na usiwe mjinga tena!
Karibu tena[emoji1756][emoji1756]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila ushaelimika najua.Nakuelimisha na kukupa taarifa ili uzinduke na usiwe mjinga tena!
Mwajiri ataombwa kujibu vielelezo na kujibu hoja za mrufani tu.halafu mfumo wao wa kushughulikia rufaa hauna mantiki nzuri; wanawasiliana na mwajiri ila mwajiriwa haitwi ktk kikao chochote.
Ni wazi kuwa kuna changamoto ktk maamuzi
Asante kwa compliment.
Pole kwa majibu mabaya ila si ulipewa nafasi ya kukata rufaa kwa Mh. Rais ulifanya hivyo ukashinda kama Tume ilikuonea?
Pole ila amini haki itatendekaNdiko shauri liliko right now
Hiki ndicho kinachotakiwa kufanywa. Watoe cause list (mkeka) ya kuonesha rufaa zipi zinasikilizwa katika kikao husika na zipi zitasikilizwa kikao kijacho.Tume itafute mbinu ya kupunguza msongamano wa kesi mfano kesi ambazo zimewasilishwa tmTume nje ya mda, management iwe inaandaa paper na kupeleka kwa makamishna kupitishwa kwa circular resolution. badala ya kuanza kumuandiki mwajiri, kufanya uchambuzi nk huku ni kupoteza mda tuu badala ya kutoa maamuzi mapema within a month say halafu baada ya hapo mlalamikaji achukue hatua zingine stahiki mfano kwenda CMA nk.
Pili tume hebu wafundisheni staff wenu wawe na customer care nzuri wanatoa majibu makavu short na dry hii sio sawa . Simu hawapokei. Kuna siku nilipiga simu nikawapa identity ya uongo wakasena oh shauri lako lipo ktk uchambuzi. Nikagundua kuwa hawa wapokea simu hawana muda wa kufanya kazi kwa wekedi bali wanatia majibu ya uongo. Tabia hii inasababisha malalamiko yasiyo ya lazima.
Tume kwa nini hamtoi taarifa sahihi? mtu akiuliza shauri lake mtalimaliza lini hamsemi ni kumzungusha tuu mtu bila sababu mbona hata Court of appeal hapako hivyo wapo wazi kabisa hamna usiri usiri usio na maana ukienda CA unakuta list ya cases na tarehe gani kuna tukio gari. Tume hebu badilikikeni, mkiona kuna malalamiko msijitetee badala yake rekebisheni kasoro.
Kanuni ya 62 (2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za 2003, ambayo inaeleza kuwa TUME inatakiwa kuhitimisha Rufaa (kuitolea uamuzi rufaa) ndani ya siku 90 (miezi 3 tu) toka Mwajiri alipowasilisha utetezi wake.Naomba Kanuni inayotoa muda wa rufaa kutolewa uamuzi
Aya ya 3 na ya 4, tume imepata wapi mamlaka ya kusikiliza malalamiko??Huu ndio tunaita "upotoshaji"
Tume ina maafisa wasiozidi 35
Wanashughulikia rufaa za watumishi wooote wa umma ukiondoa walimu, polisi, magereza, na wanajeshi
Unajua workload ya rufaa au unalalama tu.
===
Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma
NA MWANDISHI MAALUM-PSC
Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma (Sura ya 298 marejeo ya mwaka 2019), pamoja na majukumu mengine Tume ina jukumu la kupokea na kushughulikia rufaa kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Nidhamu ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao, kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (1) cha Sheria hii na Kanuni ya 60 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.
Tume ya Utumishi wa Umma inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” tarehe 12 Agosti 2021 kama ifuatavyo:-
1. Kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume inaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe 6 ambao huteuliwa na Rais ambao pamoja na majukumu mengine wana jukumu la kisheria la kutolea uamuzi rufaa na malalamiko yanayowasilishwa mbele ya Tume. Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 14(1) na (2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume ina Katibu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu. Katibu na Wasaidizi wake (Sekretarieti) ndio watendaji wa kazi za kila siku katika Tume ya Utumishi wa Umma ambao wameteuliwa baada ya kukidhi sifa na vigezo katika nafasi walizo nazo.
2. Pamoja na Sheria zilizopo, Tume inashughulikia rufaa kwa mujibu wa Mwongozo Kuhusu Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2009 ambapo rufaa hupokelewa, husajiliwa, huchambuliwa na kupitiwa na Kikao cha Menejimenti na hatimaye kuwasilishwa mbele ya Tume kwa uamuzi. Hatua ya mwisho ni Mrufani na Mrufaniwa kujulishwa kwa barua juu ya uamuzi unaotolewa na Tume. Utaratibu huu umewekwa ili kuimarisha utendaji kazi, kudhibiti upendeleo, rushwa na kuimarisha utoaji wa haki. Aidha, elimu kuhusiana na utaratibu huu imekuwa ikitolewa kwa wadau kupitia majukwaa mbalimbali.
3. Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko haitoi uamuzi kwa shinikizo au ushawishi wa Mwajiri au Mamlaka ya Nidhamu yoyote ili kuwakandamiza watumishi wasipate haki zao. Tafsiri kuwa Tume ni chombo cha kulinda maslahi ya Waajiri na Serikali. Tume inapenda kuufahamisha umma kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.
4. Rufaa na malalamiko yanayopokelewa Tume yenye vielelezo vilivyokamilika ndio yanayoshughulikiwa na kutolewa uamuzi kwa kadri yalivyopokelewa (First in, First Out).
5. Tume ya Utumishi wa Umma, inaomba umma kuupuuza upotoshwaji huu uliotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” na inatoa wito kwa umma na wadau wote kuwasiliana na Tume kwa ufafanuzi, maoni au suala lolote kuhusu Tume kupitia simu namba 0738166703, 0733 005 974 na barua pepe, secretary@psc.go.tz.
Imetolewa na:
John C. Mbisso
KAIMU KATIBU
TUME YA UTUMISHI WA UMMA
DAR ES SALAAM
13 AGOSTI, 2021
![]()
Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma
www.diramakini.co.tz
Unaposema unakula mishahara yote unaonesha kama ni faida hivi wakati mishahara ilitakiwa kulipwa hivyo kama ingelipwa wakati ule mtu aliotakiwa kufanya kazi. Sasa kwa vile inalipwa nje ya utaratibu lazima iwe na fidia maana huyo mfanyakazi kwa ajili ya survival alilazimika kutafuta fedha mahali kwingine (sio mshahara).We ni boonge la kilaza ukishinda tufaa yako unakula mishahara yako toka umefukuzwa kazi.kwanza ukute hata ajira huna
Muda wa mwajiri kuwasilisha vielelezo vyake na majibu ya Rufaa ni siku 14, na anatakiwa kumpa nakala ya vielelezo hivyo mrufani (mwajiri).Hii Tume ni hovyo kabisa! Wanachezea haki za wafanyakazi kirahisirahisi tu. Sheri zinawekwa halafu wanakuwa wa kwanza kuzikiuka....pumbavu kabisa.
Afisa Mwandamizi mzima eti anajibu very simple kwamba wana workload kubwa, kwani hiyo workload inamsaidia nini mtumishi?, kwani umuhimu umuhimu wa kuweka Sheria na Kanuni ni upi?
Unàchanganya, hiyo unayoizungumzia ni Sekretarieti ya Ajira, lakini huu uzi ni kuhusu tume ya utumishi wa ummaSijui ni nani alileta wazo la kuanzishwa kwa hii kitu.
Bora utaratibu wa awali wa taasisi zenyewe kuajiri zirejeshwe.
Mfano wengine walikuwa wanatumia wakufunzi wa vyuo udsm/MU kuwa interview na kupeleka majina ya walioshinda kwenye taasisi husika.
Kama lilivyo shirika la Posta Tanzania. Wazee wengi mno na hawaendani na kasi ya teknolojia.Ni kweli Rushwa imekithiri pale kuna jamaa yangu alitoa milioni tatu ili issue yake iweze kukimbizwa.
Management imejaa wazee wenye speed ya konokono na mawazo ya kizamani waliorudisha miaka nyuma na wengine wamestaafu lakini bado Katibu Mkuu UTUMISHI anawaongezea ajira za mkataba wakati vijana wapo tu mtaani.
Ushauri wangu kwa UTUMISHI na Katibu Mkuu Kiongozi badilisheni Management nzima ya TUME mlete watu wengine tena wawe vijana wachapa kazi wenye speed ya kukimbiza mashauri ya wakata rufaa. Au kama kuna vijana hapo TUME wachapa kazi wapewe madaraka wapeleke mambo kwa kasi.
Unàchanganya, hiyo unayoizungumzia ni Sekretarieti ya Ajira, lakini huu uzi ni kuhusu tume ya utumishi wa umma