Utendaji Mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma; Rais Samia tupia jicho lako hapo

Utendaji Mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma; Rais Samia tupia jicho lako hapo

Angalia sasa, mnampa kazi bure Mh. Rais kwa utopolo wenu na ucheleweshaji wa bure wa haki ya Mtumishi....Shame on you!!
Sio anapewa kazi ndio mchakato wa kupata haki ulivyo.

Na kwa taarifa yako waliowahi kushinda maamuzi ya TUME kwa RAIS na MAHAKAMA KUU hawafiki 2%

Hii inaonesha jinsi TUME ilivyo makini
 
Kumbe unaongelea usichokijua utendaji wake karibuni. Basi ndio ujue kwa sasa TUME ni uozo mtupu.
Hakuna kitu sikijui we lalama hapa.

Ungesoma sio unaajiriwa kwa vyeti vya wengine[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
We ni pimbi sana rushwa utatoa kwa watu wangapi??

1.Ofisa
2.Idara
3.Mngmt Tume

Nani atakayepindisha haki yako

Process ndefu inahusisha watu wengi sana.
Hiyo approach yako na lugha isiyo ya staha inaonyesha rangi halisi za huko ulipo. TUME kwa sasa ni UOZO kwa rushwa na ndio maana inatakiwa imulikwe na mamlaka husika. Kama watendaji wenyewe ndio kama wewe ni dhairia shairi mmejichokea.
 
Hakuna kitu sikijui we lalama hapa.

Ungesoma sio unaajiriwa kwa vyeti vya wengine[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Pole sana ndugu. Kama ndio wewe TUME wamekutuma uwatetea mbona unawaharibia zaidi?
 
Hiyo approach yako na lugha isiyo ya staha inaonyesha rangi halisi za huko ulipo. TUME kwa sasa ni UOZO kwa rushwa na ndio maana inatakiwa imulikwe na mamlaka husika. Kama watendaji wenyewe ndio kama wewe ni dhairia shairi mmejichokea.
Umewahi kutoa rushwa?? Kwanini usimshikishe pesa za TAKUKURU?
 
Mchakato nimekueleza

Ningekuwa "mweupe kichani" ningeshafukuzwa kazi ila bado nadunda

We uliye "mweusi" kichwani wamekula kichwa
Ni bahati tu kama uko kwenye ajira ila inaonekana huna kitu kichwani kutokana kuongelea usichokijua. Muda wako hauko mbali wtakugundua tu. Walifukuzwa wengi hawana wa kuwalinda kama unavyolindwa wewe pamoja na uwezo wako mdogo.
 
Kwanini unahisi hawana wa kuwalinda ili hali wanakata rufaa kwa RAIS wasiporidhika wanakata rufaa MAHAKAMA KUU?
 
Umewahi kutoa rushwa?? Kwanini usimshikishe pesa za TAKUKURU?
Hayo maswali yataulizwa na serikali ikiwamulika TUME iliyooza kwa rushwa. Wewe unauliza kama nani wakati umeshaonyesha upande unaoutetea.
 
Huu ndio tunaita "upotoshaji"

Tume ina maafisa wasiozidi 35

Wanashughulikia rufaa za watumishi wooote wa umma ukiondoa walimu, polisi, magereza, na wanajeshi

Unajua workload ya rufaa au unalalama tu.
===

Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma

NA MWANDISHI MAALUM-PSC

Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma (Sura ya 298 marejeo ya mwaka 2019), pamoja na majukumu mengine Tume ina jukumu la kupokea na kushughulikia rufaa kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Nidhamu ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao, kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (1) cha Sheria hii na Kanuni ya 60 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.

Tume ya Utumishi wa Umma inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” tarehe 12 Agosti 2021 kama ifuatavyo:-

1. Kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume inaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe 6 ambao huteuliwa na Rais ambao pamoja na majukumu mengine wana jukumu la kisheria la kutolea uamuzi rufaa na malalamiko yanayowasilishwa mbele ya Tume. Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 14(1) na (2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume ina Katibu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu. Katibu na Wasaidizi wake (Sekretarieti) ndio watendaji wa kazi za kila siku katika Tume ya Utumishi wa Umma ambao wameteuliwa baada ya kukidhi sifa na vigezo katika nafasi walizo nazo.

2. Pamoja na Sheria zilizopo, Tume inashughulikia rufaa kwa mujibu wa Mwongozo Kuhusu Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2009 ambapo rufaa hupokelewa, husajiliwa, huchambuliwa na kupitiwa na Kikao cha Menejimenti na hatimaye kuwasilishwa mbele ya Tume kwa uamuzi. Hatua ya mwisho ni Mrufani na Mrufaniwa kujulishwa kwa barua juu ya uamuzi unaotolewa na Tume. Utaratibu huu umewekwa ili kuimarisha utendaji kazi, kudhibiti upendeleo, rushwa na kuimarisha utoaji wa haki. Aidha, elimu kuhusiana na utaratibu huu imekuwa ikitolewa kwa wadau kupitia majukwaa mbalimbali.

3. Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko haitoi uamuzi kwa shinikizo au ushawishi wa Mwajiri au Mamlaka ya Nidhamu yoyote ili kuwakandamiza watumishi wasipate haki zao. Tafsiri kuwa Tume ni chombo cha kulinda maslahi ya Waajiri na Serikali. Tume inapenda kuufahamisha umma kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.

4. Rufaa na malalamiko yanayopokelewa Tume yenye vielelezo vilivyokamilika ndio yanayoshughulikiwa na kutolewa uamuzi kwa kadri yalivyopokelewa (First in, First Out).

5. Tume ya Utumishi wa Umma, inaomba umma kuupuuza upotoshwaji huu uliotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” na inatoa wito kwa umma na wadau wote kuwasiliana na Tume kwa ufafanuzi, maoni au suala lolote kuhusu Tume kupitia simu namba 0738166703, 0733 005 974 na barua pepe, secretary@psc.go.tz.

Imetolewa na:

John C. Mbisso

KAIMU KATIBU

TUME YA UTUMISHI WA UMMA

DAR ES SALAAM

13 AGOSTI, 2021

Hili liutopolo kabisa ndio limejibu nini?
 
Kwanini unahisi hawana wa kuwalinda ili hali wanakata rufaa kwa RAIS wasiporidhika wanakata rufaa MAHAKAMA KUU?
Hapa tuchoongelea ni UDHAIFU wa TUME. Ingefanya kazi yake vema ingempunguzia kazi Mh Rais na Mahakama. Sasa kama TUME ni uchochoro wa kupitia ili uendelee mbele wa kazi gani?
 
Hapa tuchoongelea ni UDHAIFU wa TUME. Ingefanya kazi yake vema ingempunguzia kazi Mh Rais na Mahakama. Sasa kama TUME ni uchochoro wa kupitia ili uendelee mbele wa kazi gani?
Ndio.maana nikakuambia only 2% ya mashauri ya Tume yamewahi kubatilishwa.

Hata mahakamani kuna mahakama kuu ya rufaa
 
Back
Top Bottom