Kimsingi, Tume ya Utumishi wa Umma katika kusikiliza Rufaa haiafuati wala kusimamia sheria ya utumishi wa umma.
Waajiri wanafurahia sana rufaa kuja tume (na ndio wanakomaa na kutafsiri vibaya kifungu cha 32A cha Sura ya 298 (Rejeo la 2019) ya sheria za Tanzania. Waajiri haohao na kwa kesi (mgogoro) hiyohiyo hawapo tayari kabisa kuiona ikipelekwa CMA, wanaihofia CMA ambayo ina mamlaka kisheria na wao wanalazimisha iende tume ambao hawana mamlaka kisheria.
Tume inaendeshwa kizamani sana na hawataki kubadilika. Watu wameshauri iwe inaweka cause list basi watu wajue rufaa zao zinasikilizwa lini lakini hawataki, UWAZI unakuwa haupo, kuaminika kutatoka wapi? Kuna gharama gani kuweka cause list? Mahakama ya Rufaa baadhi ya mikoa inakaa vikao mara 2 tu kwa mwaka lakini wanatoa cause list na rufaa zinasikilizwa kwa uwazi, TCRA wanaposikiliza mgogoro wanatoa cause list na unasikilizwa kwa uwazi, Vivyo hivyo Fair Competition Tribunal, EWURA nk, hawa tume nini hasa kinawazuia kuwa wawazi?
Kulalamikiwa sio sifa nzuri, inapaswa wajitafakari na wabadilike.