Utendaji wa bangili ya Kupumbaza nyoka na Jiwe la nyoka

Utendaji wa bangili ya Kupumbaza nyoka na Jiwe la nyoka

Mi nakubali sijasoma, ila mi sio kama wewe... siwachukii waliofika chuo..... Kwahyo kwa hicho kimombo ndo unantishia nawewe umesoma?
Hapana... Hata kidogo. Hii lugha ni kama kiswahili tu kwangu.so haihusiani na elimu....mi nawachukia ambao wamesoma halafu hawajaelimika. Napenda walioelimika.😁
 
Nyoka washamstudy na kujua tabia zake kipi apendi kipi apatani nacho mfano zipo device zinazuia uwepo wa nyoka mita 50 kwa degree 360.
Zipo zinazotoa mawimbi ya sauti zisizopatana na nyoka.
Ipo mimea isiyopatana na nyoka
 
Pana mti mmoja unaitwa mnyokanyoka upo kama muhogo ukipanda kama fence unafukuza nyoka. Pia waya wa shaba haupatani na nyoka unazuia nyoka
 
Na vipi kuhusu kung'atwa na nge na shilingi mia moja maana hiyo nishaweka hiyo nina ushahidi mwenyewe na wengine pia wanajua.
Sumu ni kemikali na shilingi mia ni madini.So zile metali zilizopo kwenye shilingi mia zina nguvu ya kuivuta ile sumu ya ng'e
 
Nachojua hili jiwe linakusaidia kupunguza madhara lakini ni lazima ufike hospital pia
 
Hata unga wa mkaa huu wa kawaida unayo uwezo wa kufyonza sumu ya nyoka au mdudu. Ni kama ilivyo kitunguu saumu kinazuia kuvimba uking'atwa na nyuki, au mdudu yeyeto we ponda paka kinafyonza sumu
 
Nimekuwa nikijiuliza sayansi iliyoko katika lile jiwe ambalo watu hutumia mara waumwapo na Nyoka. Unaliweka sehemu husika na linanyonya sumu mpaka linapodondoka. Ni sayansi gani hapo inayofanya kazi? Wenye uzoefu please.

Lakini pia ile bangili ambayo husemekana inampumbaza nyoka. Inafanyaje kazi? Tunaomba kupeana darasa katika mambo haya please.
Jiwe
Screenshot_20220908-073315.jpg
Screenshot_20220908-073415.jpg


Mawe haya sijui yanapatikana wali
 
Sijui umri wako,sijui umekulia wapi..Ila Mimi kwetu tabora nimeona tiba nyingi za kushangaza...ikiwemo ile dawa ya kuunga mfupa uliovunjika kwa tabibu kuchezesha viganja vya mikono pembezoni mwa mguu/mkono uliovunjika,Kuna ngariba umakondeni huko alikua hashiki kisu kukata govi,anaweka mhogo kwenye ungo,anakwambia chukua,menya nchani kwa kuvua,ukimaliza na govi lako halipo,anakupaka dawa ndo ushatahiriwa
Walikufa na elimu zao.
Hawa wangetusaidia Sana MOI pale kuunga mifupa ya bodaboda
 
Broo wangu alishawai kugongwa (kung'atwa na nyoko)
Walimchanja kidogo karibu na eneo alilohongwa.
Walimuwekea hilo jiwe la sumu, likaganda na kweli lilikua linavuta sumu

Baada ya muda linadondoka, inabidi mlichemshe
Then mnaliweka tena
Hiyo process inajirudi hadi unafika muda ukiliweka linaanguka muda huo huo

Alipona, na hakupelekwa hospital

TIBA ZA ASILI ZIPO, TENA KONKI SANA
 
Tukae nayo kama hakiba...ila baada ya kumuweka jiwe umfunge, na awahishwe hospital
Broo wangu alishawai kugongwa (kung'atwa na nyoko)
Walimchanja kidogo karibu na eneo alilohongwa.
Walimuwekea hilo jiwe la sumu, likaganda na kweli lilikua linavuta sumu

Baada ya muda linadondoka, inabidi mlichemshe
Then mnaliweka tena
Hiyo process inajirudi hadi unafika muda ukiliweka linaanguka muda huo huo

Alipona, na hakupelekwa hospital

TIBA ZA ASILI ZIPO, TENA KONKI SANA
 
Nikikutana na wanaouza hayo mawe ntayanunua

Ukikaa nayo kama akiba ni muhimu sana
Stand ya mabasi ya Msamvu Morogoro kuna Mzee anauza hayo mawe, nilishanunuwaga wakati Nina field za porini.
 
Pana mti mmoja unaitwa mnyokanyoka upo kama muhogo ukipanda kama fence unafukuza nyoka. Pia waya wa shaba haupatani na nyoka unazuia nyoka
Njia rahisi ya kufukuza nyoka ni kuchoma matairi ile harufu watakimbia mbali kabisa.

Njia ya kuikinga nyumba na nyoka mwaga majivu kuzunguka nyumba au ukiwa na oil chafu Fanya hivyo.
 
Habari
Ninalo hilo jiwe naliambiwa kuwa ili kulifahamu kulifahamu jiwe hilo unalijaribu kwa kuliweka kwenye ulimi linanata. Seems hata sisi wanadamu kwenye mate yetu kuna kiwango fulani cha sumu dhidi ya viumbe wengine. Jiwe lipo kama mkaa lakini lina manufaa makubwa

Naweka picha
Inawezekana,umeshajiuliza inakuwaje mdudu akiingia kwenye jicho au sikio akikutana na yale maji maji anakufa,ngoja nifanye research,siku nikikutana na Nyoka nimtemee mate nione nini kitatokea,halafu ntaleta mrejesho...
 
Back
Top Bottom