Utenguzi: Rais Samia atengua nafasi za Viongozi wafuatao

Utenguzi: Rais Samia atengua nafasi za Viongozi wafuatao

Toka maktaba :

Ruangwa, Lindi

MKUU WA WIILAYA YA MBARALI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI


Video toka maktaba : Mkuu wa wilaya wa Mbarali Mheshimiwa Reuben Mfune

TAKUKURU imemfikisha Mkuu wa wilaya wa Mbarali Mheshimiwa Reuben Mfune (58) mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi namba 1 ya mwaka 2023.

Baada ya kusomewa mashtaka, mtuhumiwa alikana tuhuma za makosa na amepewa dhamana. Na kesi hiyo kusikilizwa tena mwezi February 2023 mbele ya Mahakama ya Wilaya.


TOKA MAKTABA :
30 Oktoba 2013
1674576273041.png

DC Ruangwa kusaka mchawi anayekwamisha maendeleo ya ...

30 Oct 2013 — Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Reuben Mfune aliahidi kufanyia kazi malalamiko hayo ya watumishi .....

TOKA MAKTABA :
18 May 2016
KESI YA DAVID KAFULILA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI 2015

Aidha katika kipengele cha pili ambacho Kafulila alikuwa anamlalamikia Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo, Reuben Mfune; aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kuwa alishinikizwa kumtangaza Mwillima kuwa mshindi wakati msimamizi huyo akijua kwamba yeye Kafulila ndiye.

Kafulila alikuwa anamlalamikia Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo, Reuben Mfune; aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kuwa alishinikizwa kumtangaza Mwillima kuwa mshindi wakati msimamizi huyo akijua kwamba yeye Kafulila ndiye ......
 
Mh
Tunaweka dini yetu. Hao wote ni makafir.
Tunaweka dini yetu. Hao wote ni makafir.

Najiuliza tuu hivi kafiri na wale wazee wa kwampalange wepi wataingia kwa pepo?

Mbali nasisi ma Jah man mbingu yetu Ina eleweka
Wewe ni mpumbavu! Hakuna hata mmoja anayepewa madaraka kwenda kuwatumikia wanadini wenzake badala ya Watanzania

Dini dini hizi' ziishie kwenye milango ya kuabudia tuu' mitaani wote ni Watanzania" dini zinachelewesha saana na zina magomvi kibao na sio za kubembeleza hizi! Mtu akileta fyoko akihusisha dini, tafahari afyekwe haraka sana! Dini ni kama mafuta ya petrol!


Duh! njiapanda mkuu🥺🥺
 
Reuben Mfune anakesi Ruangwa alipokua DED anadaiwa kupiga 200 Mil. Kinyume na utaratibu, hao wengine pia wana vimeo TAKUKURU
TAKUKURU inafanya kazi sana msimu huu. Wakikudaka huchomoki kirahisi, wameondoa ule uzembe.
Ila kazi waifanyayo TAKUKURU ni 1/10 ya kazi wanayotakiwa fanya.
Bado halmashauri na taasisi nyingi za serikali zina ubadhirifu.

Takukuru iongezewe nguvu zaidi kifedha, vifaa.
 
Watu wanamdharau mama eti siyo mkali. Wanasahau kuwa alishaweka wazi kwamba makuzi na Imani yake havimuruhusu kumfokea mtu mzima, na kwamba yeye anatumia kalamu. Huwezi kufanya Kazi za utawala majukwaani, huko ni kutafuta political popularity ambayo Rais wa nchi haiitaji kwa sababu tayari ni popular kwa nafasi yake. Mama yuko kazini wanaobisha wataendelea kuumia tu.
Hivyo ni vidagaa tu!
 
TAKUKURU inafanya kazi sana msimu huu. Wakikudaka huchomoki kirahisi, wameondoa ule uzembe.
Ila kazi waifanyayo TAKUKURU ni 1/10 ya kazi wanayotakiwa fanya.
Bado halmashauri na taasisi nyingi za serikali zina ubadhirifu.

Takukuru iongezewe nguvu zaidi kifedha, vifaa.
Hiyo moja ya kumi umewapa kubwa sana mkuu
 
Back
Top Bottom