Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Status
Not open for further replies.
toauti ni kubwa sana,enzi za mwalimu TISS ilikuwa inafanya kazi kwa kuzingatia weledi na katiba na sharia za nchi bila kusahau ETHICS za kazi zao ambazo zinahitajiconfidentiality ya hali ya juu!na msingi wa kazi yao ni kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa dhidi ya yeyote anayetaka kuhujumu!na pia target kubwa ya TISS ya mwalimu ilikuwa kuhakikisha viongozi wetu wa ngazi za juu mawaziri,wakuu wa mikoa na vigogo wote kwy mashirika ya umma na tahasisi mbalimbali wanazingatia ETHICS kweney utendaji wao hivyo TISS ilikuwa inawafuatalia kwa karibibu viongozi waliokuwa wanakiuka MIIKO ya uongozi kama ilivyoanishwa kwenye AZIMIO LA ARUSHA.TISS ya JK Kazi ni mabingwa wa kungoa meno na kucha bila GANZI, kutesa na kutelekeza watu kwenye msitu wa PANDE kama vile Dr.Ulimboka,Kibanda.
 
Hiyo TISS ni idara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba, wewe kwa nini unadhani shughuli au wajibu wake hautakiwi kujulikana?

Inaonekana wewe ni muelewa. Hebu nipatie mfano wa nchi moja tu duniani ambayo idara yake ya usalama inaanika targets zake na goals zake. Just one country on earth!
 

Wewe akili yako ni usiku wa giza. Nape anihonge mimi??? Ananijua mimi??? I am independent and I have the right to freely express my feelings here just like you do. You would not put words into my mouth so as to say what you want to hear or read. All those allegations you are referring to are mere gossip with no truth at all. Do you believe everything reported in Newspapers? Do you? Unless the culprits are arraigned in court and dealt with according to the law, no one really knows who the real culprits are...
 

Big Up. Una uzalendo wa kweli kwa nchi japo mapenzi ya chama yanaweza kuwapo kwenye akili yako. Nchi kwanza. Napenda unavyochambua issue in a positive and crically withou any bias. Tungekuwa wote kama Bw. Kiroba JF inegkuwa ni jamvi la manufaa hasa kuliko ambavyo wengi wetu tumekuwa negatively moved only on political affiliations and supportive fans without looking on issues critically and analytically.
 
usalama wa taifa wapambane na mafisadi. watusaidie katika uchumi wa taifa. vipi kama kuna vyama au vikundi vinaanzishwa kuvunja umoja/utaifa uliopo? wafanyeje? usalama wa taifa wasaidie kuhakikisha kuwa wana vishughulikia vyama na vikundi hivi. usalama wetu si kulinda tusiibiwe tu. usalama wetu ni pamoja na kulinda taifa hili linaloitwa tanzania.
 


Ahaaaa, kwa hiyo unakuja hapa JF kutoa matusi hayo bila hata kujadili hoja objectively. Ukitafutwa ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema??????
 

Pole. tatizo letu watz tunapenda saana kusahau historia kwa kudandia yaliyopo sasa. Nani kasema wakati wa mwalimu TISS haikutesa watu na hata kupoteza kabisa? TISS ndo kilikuwa chombo kama mungu mtu hapa TZ, nani alikuwa na uhuru wa kukijadili kama hivi inavyofanyika sasa? Au ndo tunapenda kujitia upofu kwa sababu sasa ni kikwete dhidi ya nyerere? Kwani huyu kikwete karithi kutoka kwa nani kama siyo huyo mnaemdhania kuwa hakukosea (nyerere)? Tuache kufikiri kwa mrengo wa nyuma, tufikiri kwa kutumia akili. Ingekuwa uhuru na wingi wa vyombo vya habari kwa sasa ni sawa na wakati ule wa nyerere mbona kila mtu angemkataa asiwe rais wa nchi hii. amefanya mabaya makubwa yenye uovu na uonevu mkubwa kwa wa TZ ambayo hayafikiriki? Let us leave biasness and be analytical criticisers
 
Ahaaaa, kwa hiyo unakuja hapa JF kutoa matusi hayo bila hata kujadili hoja objectively. Ukitafutwa ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema??????
GO TO HELL!! huna wa kumtisha!!
 
on a curious note mkuu, huyo jamaa kwenye avatar yako ungempatia hata meno ya bandia tu, manake yatakuwa yalishamkuta!

noted mkuu, tamaduni zinaruhusu mkuu, hiyo ni njia maalum ya tiba, kwa magonjwa kama tetenus, na mengine mkuu, huyu yupo salama kabisa anafurahia maisha mkuu, kama unavyoona, smile kubwa linamananisha mambo poa kabisa,
 
Ahaaaa, kwa hiyo unakuja hapa JF kutoa matusi hayo bila hata kujadili hoja objectively. Ukitafutwa ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema??????

Kwa nini usimtafute bila ya kumwambia? Au sheria inasema mhalifu anapigiwa simu kabla ya kutuma kikosi cha kumkamata....Yaani kama mitaa ya kwetu kila mtu anatoa haya mabiti loooooooooooooooooh!!!!!! TZ kiboku.
 
Kwa nini usimtafute bila ya kumwambia? Au sheria inasema mhalifu anapigiwa simu kabla ya kutuma kikosi cha kumkamata....Yaani kama mitaa ya kwetu kila mtu anatoa haya mabiti loooooooooooooooooh!!!!!! TZ kiboku.

Naona hujanielewa. Mimi sina mamlaka wala uwezo wa kumkamata. Bali nilimuuliza, je iwapo ukatafutwa na ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema???
 
It was a beacon of our nation. Leo hii mhhh!

Ukweli TISS ya leo inatia aibu sana, nawahurumia zaidi wale waliokuwa vijana ndani ya TISS ya Nyerere ambao nasikia kuwa siku hizi wametengwa kiaina fulani vile..yaani wapowapo tu ili wapate mshahara mwisho wa mwezi

Kweli ilikuwa vigumu kuwajua lakini kwa wale kama wa Ubungo flats pale tulikuwa tunawajua kwa uchache na si kwa undani sana kama hawa wa leo wanojianika utafikiri mitumba ipo Gulioni
 
Unamjua IGHONDU wewe au unashabikia tu taarifa za kutunga za magazeti?

Wewe una kila sababu ya kumjua kwavile nyie wote ni majasusi; mimi sina hata haja ya kuona uso wake kwani ni muuaji!!
 
Naona hujanielewa. Mimi sina mamlaka wala uwezo wa kumkamata. Bali nilimuuliza, je iwapo ukatafutwa na ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema???

Mkuu lazima tukubali kuna tatizo huko TISS kwani hii idara inatumika vibaya na lazima wawe wakali kutoruhusu wahuni wachache ambao ni watendaji wanaotumika ili kuharibu maana na malengo yao.
 
Inaonekana wewe ni muelewa. Hebu nipatie mfano wa nchi moja tu duniani ambayo idara yake ya usalama inaanika targets zake na goals zake. Just one country on earth!
Simaanishi kwamba waseme Metsada leo tumechunguza na kugundua ujangili, namaanisha kwamba shughuli na wajibu wa idara hiyo unajulikana na mambo kama kushamiri kwa ufisadi, biashara za magendo, utoroshwaji wa wanyama wakiwa hai, udini, usafirishwaji wa meno ya tembo,kutekwa kwa watu mara kwa mara na kunyofolewa kucha, meno na macho, mauaji ya albino, mauaji ya viongozi wa dini, kuzagaa hadharani kwa kanda zinachochea mauaji hayo n.k, ni ishara kuwa ama idara hiyo ni dhaifu sana katika kutekeleza majukumu yake au inashiriki moja kwa moja kutekeleza mambo hayo.
 


Tunapojadili tusiifishe fikra kwa vitu complex ambavyo hata hatuna ushahidi navyo. Bila kujua sana majukumu ya TISS tujiulize matukio ya hivi karibuni na jitihada za TISS kuzuia yasitokee. Benki kuu yetu mwaka 2005-2006 ilivunjwa kweupe na Watanzania katika jua la utosi bilioni 150 zikachotwa na kuishia mifukoni mwa watu. Tukaambiwa kati ya wezi hao ni Kagoda ambayo tuliambiwa fedha zilienda kwa mambo ya usalama kabla Zakia Meghji hajabanwa naye kumsakizia aliyekufa na hali akijua hawezi kuwa shahidi.

Kuna Meremeta, Buzwagi, Richmond, Twiga na wanyama wengine kutoroshwa kweupe na ndege za kitapeli toka nje. Nijuavyo viwanja vya ndege vya kimataifa kuna mtu wa TISS anayetakiwa kukagua kila ndege ya nje inayofika hapa na kutoka. Naambiwa twiga hawa walitoroshwa na ndege za kijeshi za Qatar. Hivi bado viko kwenye kumbukumbu zetu. Riporti za CAG na mengineyo.

Tujiulize hivi kweli chombo hiki ni mahili and ethical wakati mambo haya yametokea na kulitia Taifa letu doa kiasi hicho? Kinastahili kuenziwa na kisiojiwe? Ndugu yangu nafikiri matukio haya na majibu mepesi toka serikalini na idara zake yanaleta opportunity of doubt.
 

Ningependa kuiamini TISS kama Taasisi kwa sababu hata tukibadili Wapangaji wa Ikulu TISS itafanya kazi na yeyote atakayeingia madarakani. Hili liko Kisheria/Kikatiba.
Hao Individuals wanaotajwa tajwa kuhusika na matukio ya utesaji hawawezi kusababisha tufike mahala tuione TISS kuwa haifai hata kuwepo. Ndiyo maana nilisema taasisi zenye majukumu ya kuisimamia TISS ZIWAJIBIKE. Lakini katika huo uwajibikaji tusijikute tuna-broadcast our weakness.
 

tofauti ni kuwa enzi za nyerere, idara hii haikuwepo kisheria. hivyo ilikuwa inaendeshwa kutokana na utashi wa rais. baada ya vyama vingi, kukawa na ulazima wa chombo hiki kuwa rasmi ndipo bunge lilipotunga sheria ya idara ya usalama wa taifa mwaka 1996. kwa sasa haifanyi tena kazi kwa matakwa ya mtu mmoja tu. idara inajitahidi kuaccomodate watu wote japo wengine hatuoni hilo
 
utajie hao watu ambao TISS ya mwalimu iliwatesa na hata kupoteza kabisa na kasha tufanye comparison na hawa wanaoteswa ha JK tuone kama kuna uwiano,awa wakina kibanda na Ulimboka Nyerere angewaona na hatia angekamata na kuweka ndani(detention) na hiyo ingelikuwa ni kazi ya POLISI tu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…