UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

bado katika hii thread sijaona mwanasheria wa kumtetea lulu...!
you are really a viper.......................nani kakwambia lengo ni kumtetea lulu?.................kazi yetu ni kuutafuta ukweli tu mambo ya utetezi ni ya wengineo.....................lakini ni rahisi kuongea ulichoongea bila ya kujibu ya maswali ya kwa nini......
 
Kweli utetezi umesimama vema!

Uncle jey jey...............wawe waungwana wasalimu amri na yaishe kwa kumwachia binti mdogo aende kujenga nchi yake.......na wao waendelee na majukumu yao.........
 
9. Alishawahi kupatikana na makosa mahakamani na kuhukumiwa kwa mwenendo mbaya na matusi

hiyo point je???

kwa hiyo matusi sasa ni ni muuaji wajamini......let us be serious at least fro a moment...........
 
mbwa mzee anafundishwa kuzurura majalalani? Hakuna cha kutaka kubakwa wala nini haka katoto kazinzi na kauaji jela ndo mahala pake
 
mbwa mzee anafundishwa kuzurura majalalani? Hakuna cha kutaka kubakwa wala nini haka katoto kazinzi na kauaji jela ndo mahala pake

kwa mzaha mzaha wa aina hii sote tunapswa kuwa lupango......kwa maana soe ni wahuni na tuna mafaulo yetu kibao..........acha kumnyanyapaa dogodogo...anahitaji sisi wakubwa zake tumwelekeze lipi litamfaa maishani mwake........
 
poleni wana sheria wetu, kazi mnayo kwa huyu binti yenu.
 
Guys stop speculating, the high court will collect all evidence and come up with unbiased ruling, ninyi sio watabiri kama marehemu shekh, let wait and see what gonna be, this is for Ruta and allied
 
Simu yangu haina sauti kubwa, hv umesema kanumba alikuwa anatumia ARV?? hebu rudia tena sijasikia vizuri mkuu
 
Guys stop speculating, the high court will collect all evidence and come up with unbiased ruling, ninyi sio watabiri kama marehemu shekh, let wait and see what gonna be, this is for Ruta and allied

yaani ningelikuwa ni wewe ningelijinyamazia maana hata huelewi yakuwa mahakama siyo kazi yake kukusanya ushahidi hiyo ni kazi ya DCI...........manumba........................na DPP kuamua kama kuna ushahidi wa kutosha kufungua jarida la kesi ya jinai kama hii ya mauaji.......sometimes a little silence is a sign of erudite.........
 
Simu yangu haina sauti kubwa, hv umesema kanumba alikuwa anatumia ARV?? hebu rudia tena sijasikia vizuri mkuu

kwa zaidi ya mwaka mmoja................alianza kuzitumia baada ya kucheza filamu ya From Dar to lagos.....................kainiangalie ile picha halafu utaniambia kama hakuwa alibaki mifupa mitupu.......the guy was a dead man walking sijui kwa nini hamlioni hilo...........we are a nation on denial when it comes hiv and aids.............kila siku taarifa za uongo ni kuwa maambukizi ya vvu yanapungua kumbe ukweli yamechachamaa......
 
poleni wana sheria wetu, kazi mnayo kwa huyu binti yenu.

hatuwezi kupoa kwa nini kazi siyo ya lulu tu bali kulikomboa taifa lote kutoka kwenye minyororo ya ukandamizaji wa dhuluma..........
 
Friday, April 13, 2012
Michuzi Blog Exclusive: Baba mzazi wa lulu afunguka, aomba haki itendeke katika kesi ya binti yake




[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Bw. Michael Edward Kimemeta - Baba Lulu




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Picha na Habari na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii, Moshi

Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.

Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.

Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya Marehemu
Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo.

Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Midway mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.

Bw Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba.

Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.

“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa
katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu.

“Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”alisema.

Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.

“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa” alisema Kimemeta.

Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria mazishi marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema mazingira yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole.

Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.
Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla. Friday, April 13, 2012 ~ Copyright: Michuzi Blog ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0
 
Ni picha halisi ni kipande cha movie ya marehemu imetoka muda kidogo inaitwa family tears

lakini si alikuwa anamlea mtoto wa watu kwa mikwaju ya hapa na pale tangia kakiwa kadogo sana?
 
Back
Top Bottom