Utetezi wangu wa wazi wa William Ngeleja - The use of Emergency Powers Act 1986

Jana maeneo ya Mwenge kuna mzee mmoja anasema bila Kikwete simu za mchina tusingekuwa tunatumia anasema cmu kwa 30000 unapata nilichoka akapigilia hayo ndo maisha bora

Yaani imenibidi nicheke kicheko cha masikitiko.
 
NN naomba kupingana na wewe!
Katika watu ambao nimekuwa nawapenda kimawazo ni pamoja na wewe...ila leo umenishangaza sana!Ukiangalia kiundani jinsi Mwanakijiji alivyoelezea utaona ni jinsi gani Ngeleja alivyo mzembe pamoja na watendaji wengine(sio wote) pale wizarani hasa katika kurugenzi ya Nishati.

Ninauhakika kabisa haya aliyoyasema Mwanakijiji yapo ktk makabrasha ya wizara na kama Ngeleja angelikuwa na nia ya dhati ya kuondoa matatizo ya umeme angelikuwa kashafanya hivyo kitambo sana.Chukua mfano wa mtu kama Magufuli jinsi alivyoikomalia wizara ya Ujenzi ambayo watu kama akina Sitta waliipitia na kuiacha mbovu na yenye uvundo wa rushwa na kuendeleza kale katabia ka "business as usual"!

Kimsingi na kiukweli huyu jamaa hafai na anatakiwa ama ajiuzulu au afukuzwe,PERIOD!!!
Mkuu NN,heshima yako!Hili moja halitanifanya niache kujali na kuheshimu michango yako iliyonifanya ni-fall in love na ideas zako za zamani kabla ya hii ya leo ambayo imenifanya nihisi labda kuna mtu kaiba password yako na kutuma hii "kitu".

Nawasilisha...
 

Hapo penye nyekundu mzee umenikumbusha walivyotukosakosa na mvua za Thailland...dili ambalo Lowasa alikuwa kesha liweka kwenye pipeline natumshukuru mungu kwani alijajiuzulu kabla dili halijatick, saa zingine mungu hutuonea huruma na kutusaidia kinamna kwani bila yeye saa hizi tungekuwa tumeshaumia zamaaaaani
 

Kwenye red: Aliyemuweka kwenye uwaziri ni JK ili aweze kilinda maslahi yao, nikisema maslahi yao naamanisha ni JK, EL, RA na mafisadi wengine.
 
MKJJ
Ni kweli kama ulivyofafanua kwamba matatizo ni ya siku nyingi,Lakini Ngeleja ndiyo amepewa kazi ya kuishauri na kutenda kwa niaba yetu sote,lazima abebe lawama,kama anajua hayo yote kwa nini asiwapishe wengine amabao wanaweza kutusaidia?

Kitu gani kinamshinda achukue hatua ambazo umezifafanua?ni lazima atende au atoke
 
Nakubaliana na M'kijiji kwamba chanzo cha tatizo ni Ngereja peke yake... Japo ninasisitiza kwamba, yeye ndiye wa kulaumiwa sana angalau kwa sasa. Yaani baada ya miaka mingi ya tatizo, na historia ndefu alikuwa amepata upendeleo wa kulisoma na kulielewa tatizo vizuri na kutumia mapungufu ya viongozi waliopita kufanya mabadiriko. Mfano ni kansa, inapoanza, daktari asipogundua dalili kweny chuchu tutamsamehe, lakini mpaka inapofikia ziwa zima linapotakiwa kukatwa, huyo hasamehewi hata kidogo!! Ngereja ametufikisha sehemu ambayo ziwa linatakiwa likatwe ili kuinusuru nchi kwenye giza.

Lakini, kwa nyongeza zaidi, achana na uwekezaji katika sekta ya viwanda kama ilivyopendekezwa na M'kijiji. Idadi ya watu Tanzania imeongezeka sana. Sidhani kama nalo hili linahitaji kwenda darasani ili ujue tatizo! Watu wengi, matumizi makubwa, miundombinu ileile aliyoiacha mkoloni enzi za watu M 20,000.

Lawama kubwa ni kwetu watanzania wo00te, nilazima tukione cha moto kama matokeo ya uchaguzi wetu huru wa bila kushurutishwa. Tumeichagua wenyewe, sasa tunapiga kelele nini... aah yote ubatili mtupu>>>!!!
 
kwa wale wanaotaka 2cmwajibshe ngereja wa2ambie amefanya nn tangu aanze kula kodi zetu km mshahara wa uwaziri,only when there genuine evidence ya alichokfanya kwa miaka 6 wizaran kitatutoa kwnye mawazo ya kumwajibsha.kusiwe na utetezi usio na sababu wala manufaa kwe2
 
I still maintain that there is no one, absolutely no one that knows what to do. If there is one out there, then he or she should prove me wrong.

You can prove yourself wrong, yes you can!

PS. Acha kubeba maboksi huku ulete umeme!
 
Makala nzuri lakini sijaona ni mahali gani pa kuthibitisha kwamba Ngeleja hahusiki na tatizo au kuonyesha kama yeye binafsi siyo tatizo.
Ngeleja kukuta tatizo la Nishati kutoka katika serikali zilizopita siyo hoja, hoja ni kwamba kwa muda mrefu amekuwepo katika wizara hiyo kiasi cha kumfanya awe amefanya kitu fulani cha kuondoa/kupunguza tatizo. Kiufupi Ngeleja ndiye Waziri mwenye dhamana, na anatakiwa awoconvice Watanzania kwamba anafanya jambo na matunda yanaonekana, lakini so far kwa muda aliokaa katika hiyo wizara nyimbo ni zilezile kila siku na tatizo la umeme liko palepale.

Wewe MKJJ umejaribu kuliona hilo tatizo, mbona hujiulizi kama Ngeleja kaliona?, Kama kaliona amefanya nini?, kama amefanya kitu mbona tatizo liko palepale?.

So far Ngeleja Must go.
 

Ngereja atupishe kwanza ameziba nafasi ya mtu ambaye anaweza kulitatuwa
 
Well, labda Ngeleja kaliona lakini anaogopa asije gombezwa hadharani na wakubwa zake kama Magufuli alivyofanyiwa 🙁Hapa ni president na PM wafanye haya maamuzi ya ukweli alau tuone kama Ngeleja atashindwa kutekeleza.
 
Watu wanasema ati kuna "hali ya dharura"; kwa miaka yote hii karibu ishirini hawajawahi kutangaza rasmi hali ya dharura. Wanachofanya ni kuliingiza taifa kwenye "mikataba ya dharura" bila kutangaza hali ya dharura. Huu ulikuwa ugomvi wangu na Lowassa alipounda ile tume ya dharura wakati wa Richmond. Hakuwa na madaraka hayo - isipokuwa Rais tu.

Hata leo hii, badala ya kumtaka Rais atangaze hali ya hatari ili ajirudishie madaraka aliyonayo kisheria na kuweza kuliondoa tatizo hili watu wamekubali kuahirisha mjadala ilii waje baadaye wazungumzeeeeee na Watanzania wafurahia " wabunge walikuwa wakali kweli". Ukweli uliopo mbele yetu ni kuwa hawataki kutangaza hali ya dharura kwa sababu wakifanya hivyo wanajifunga kisheria kutatua tatizo kwa haraka zaidi!

Mtu pekee anayeweza kufanya hivi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye akitaka na akilazimishwa na wabunge anaweza kutangaza hali ya hatari kesho, keshokutwa akaigiza mitambo ya dharura, paid, owned and operated by the Tanzanin Government! Aidha kuna hali ya dharura kweli au hakuna - kama hakuna mnaweza kujivuta vuta taratibu na kukaa chini na vikamati, kuzungumza hadi mtondogoo kwani siku 21 ni kupoteza muda mwingi sana kwenye uchumi.

Kama ipo - basi ni lazima itangazwe rasmi. Ninachokiona ni kuwa vyovyote vile wanataka kuwa na uwezo wa kununua au kuagiza mitambo kwa njia zile zile zilizotufikisha hapa. Mipango yoyote itakayokuja itakuwa ni kwa kutekeleza miezi sita ijayo. Pendekezo langu litaondoa tatizo hili ndani ya miezi miwili tu. Jamani, Nyerere alipotangaza hali ya hatari wakati tunaenda vitani kila kitu nchini kilielekezwa huko, na Taifa likaingia vitani kama moja na kushinda kwa mbwembwe. Bila kutangaza hali ya hatari rasmi na kuchukua hatua zinazoendana na tangazo hilo. Tutarudi tena hapa.

Ngeleja anaweza kuwajibishwa lakini atawajibishwa kwa kosa gani? Sera zinatokana na CCM, uongozi mzima unatokana na CCM, Bajeti yote inapitishwa na Bunge la CCM. Mimi binafsi ningeamini kuwa kweli wanataka kutatua tatizo kama wabunge wote wangejiuzulu warudi wote kwa wananchi. Nyerere aliwahi kuwaleta huko - na Kikwete ameonesha woga tu. Kama aliamini bajeti hiyo ni nzuri angeisimamia na kuwaambia wabunge wake msipoiipitisha turudi kwa wananchi - Bunge livunjwe warudi kwa wananchi. Na kutoka hapo ndani ya siku tisini tuna uchaguzi mkuu mpya!

Mapendekezo yako wazi:

a. Tangaza hali ya hatari (chini ya EPA 1986)
b. Suspend section za PPA hasa vipengele vyake kadhaa
c. Unda timu ya kitalaamu - siyo wanasiasa - ya kumshauri Rais ya aina ya majenereta yanayohitajika
d. Zungumza moja kwa moja na Kawasaki, GE, Siemens, na nk kuona ipi inaweza kuleta mitambo nchini kwa haraka zaidi, kwa bei nafuu
e. Agiza na lipia.

Simple.

Kuhusu Ngeleja:

Ngeleja ana kosa moja ambalo amelifanya ambalo atalilipia (kati ya mengine) nalo linahusiana na Kiwira. Kwenye Kiwira hawatomsamehe hasa kwa kuwapa Wachina waendeshe. Japo ni uamuzi wa baraza la mawaziri ni wazi wengine yaweza kuwa umeonekana ni uamuzi wake binafsi.
 
Ngeleja anaweza kuwajibishwa lakini atawajibishwa kwa kosa gani?
Hivi sasa hivi tuna umeme?
Hivi ni nani waziri wa nishati?
Hivi Ngeleja is he doing the job perfectly?
Mkuu labda ungesema Ngeleja na wenzake wengi wanapaswa kuwajibika..., na sio kwamba wengine ndio wawajibike apart from Ngeleja (it should be including Ngeleja)

When things go wrong the man in charge is answerable, and if am not mistaken Ngeleja is incharge
 
Hivi sasa hivi tuna umeme?

Lini tumewahi kuwa na umeme wa kutosha?

Hivi ni nani waziri wa nishati?
Ni yeye lakini yeye anatekeleza tu sera za chama chake zilivyo na anaweza kufanya tu yale ambayo Wabunge wake wanampatia fedha kuyafanya na madaraka kuyafanya.

Hivi Ngeleja is he doing the job perfectly?

Nani mwingine anafanya kazi yake perfectly, Rais, Wabunge?
Mkuu labda ungesema Ngeleja na wenzake wengi wanapaswa kuwajibika..., na sio kwamba wengine ndio wawajibike apart from Ngeleja (it should be including Ngeleja)

Hilo ndilo nimelisema lakini mimi sisemi "na wenzake wengi" nasema CCM na serikali yake yote.

[/quote]
When things go wrong the man in charge is answerable, and if am not mistaken Ngeleja is incharge[/QUOTE]

Ninachosema - na ndio hoja yangu - the man in Charge is CCM. Chama kizima Rais na wabunge wake wawajibishwe. Kama kweli watu wanataka mtu awajibike basi ni kujiuzulu mara moja kwa serikali nzima ya CCM - hadi Rais na kurudi kwa wananchi kupata mandate mpya ya uongozi. Ngeleja peke yake haitatui tatizo - au tumesahau kuwa Msabaha na Karamagi walikuwa mawaziri nao walijiuzulu na bado tupo pale pale?
 
nakala ndefu kama mashati ya ccm na manguo yao hatutaaki ila cc ni kwamba tunataka umeme na wanasema kuna upungufu wa mega 230 wakati kwa waziri wangu ni mega 570 sasa wanataka nin kama co nguvu ya umma
 
hilo linaturudisha kwa Kikwete.

Hivi kama kweli unaingia pahala ukakuta hupawezi lazima ung'ang'ane tu na likitu lisilo bebeka? Kama Ngeleja angekuwa kijana mzalendo kabisa na nchi hii, muda alokaa pale angetoa mapendekezo yake na ikibidi achukue hatua za makusudi kabisa angalao kuonyesha dhamira ya kweli kuwa hali hii ya umeme nchi hii inamkera sio kukaa na kucheka cheka tu! Unapopewa mke hakikisha unamweza la sivyo achana naye kuliko kukubali aibu. Ngeleja alitakiwa yeye na wataalamu wake watoe mapendekezo yao, serekali ikikataa anaachia ngazi! Sio lazima ukubali kuitwa mweshimiwa waziri huku unakuja kupata aibu. Ni kwa mara ya kwanza kwa uelewa wangu au tangu nipate akili hali kama inatokea. Kwa kusema ukweli nimemwonea huruma sana ila lazima mtu ajifunze na kwa hili wengi wamejifunza. Enzi za kuwadanganya watoto kuwa mtoto ananunuliwa! sijui anadondoshwa na ndege umepitwa na wakati! Tuelezane ukweli hii ni mimba na miezi tisa imepita na uzao ndo huu! Ngeleja alikubali kulinda na kuendeleza ya watangulizi wake. Haya ndiyo yanayomkuta! He deserve it! Kwani kule kwa Magufuli madudu si yalikuwepo pia ingawa na yeye baada ya kufungwa gavana alitakiwa ajiuzulu! Watau wanajali zaidi kuitwa Mheshimiwa Waziri! SHAME!
 
Lini tumewahi kuwa na umeme wa kutosha?

Mkuu ni kweli kwamba hatujawahi kuwa na umeme wa kutosha na bado majority of tanzanians umeme haufiki kabisa kwao..,lakini it is undisputed kwamba sasa hivi tatizo is even worse, yaani hata sisi wachache ambao tumeunganishwa na grid hatupati umeme.., Yeah its true inabidi wawajibike wengi ila thats will never happen they will find a scape goat na kumtoa kafara (as we have seen it happening today kwa katibu wa wizara)

Kwahiyo sababu Commander mwenyewe hawezi kuwajibika ni bora tuondoke na hata huyu waziri wa nishati and maybe.., just maybe the other person who steps in Ngeleja shoes will be more serious na kuacha kupiga watu changa la macho na kutufanya hatuna akili kwa ahadi hewa na miradi mingi ambayo yote haifanyiki... Maybe Just Maybe atakuwa more realistic na kuja na one mradi at a time na kuangalia hii issue in long term. Pia mbona mawaziri wengine wa CCM kama Magufuli they are more serious na wanachokifanya kinaonekana..
 

mzee kamanda mzima anaweza kuwajibika. Rais anaweza kujiuzulu na Bunge kama linaona hana uwezo wa kuongoza linaweza kumuondoa madarakkanin na makamu wake akaingia bila kulazimisha uchaguzi mkuu. Kama wana CCM wanataka kuwa wakweli wamuondoe Rais madarakani ili aingie RAis mwingiine mwenye uwezo wa kuwafuatilia mawaziri wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…