Kila mtu yupo Kwa ajili ya maslahi yake .
Ukiona wajinga watakupa maslahi yako basi watumie.
Kwa katiba hii iliyopo hata vichaa wanaweza wakapitia CCM na wakatwala nchi na Dola likawalinda mana itakua pia ni fursa Kwa wakubwa kwenye vyombo hivyo kujichukulia vyao kama nyumba inazimwa taa .
Wakati tukiwa tunasoma SHULE ZA SERIKALI ZA BODING KULIKUA NA UBABE MWINGI SANA WAKATI WA KULA CHAKULA AU MENYU. Ikitikea ghafla umeme ukakatika wakati wa kugawa chakula basi nusu au robo tatu ya Darasa watalala njaa. Mana chakula kitagombaniwa na hata kumwagikia chini na watu watatawanyika na kukimbilia mabwenini na viwanjana bila kujulikana. Wenye nguvu na wakorofi ,wavuta bhangi siku hiyo watahifadhi vyakula kwenye makabati hasa siku ya wali au nyama.
Ukiona sehemu yenye SHERIA na taratibu lakini mambo yanakwenda hovyo hovyo basi ujue taa imezimwa. Ni fursa kwa wahuni kugombania chakula na wastarabu watalala njaa.
Wapinzani wakiweza kuyasemea mahitaji ya watanzania wote CCM itatoka ipende isipende.
Mfano : Kuyasemea matatizo ya Wakulima,wafanyakazi,wavuvi,wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wanafunzi wa sekondari na vyuo , Mapolisi, wanajeshi, migambo, wenyeviti wa serikali za mitaa,madiwani, wajumbe wa mitaa , madereva n.k.
Kuwasemea watanzania bila maneno ya dharau na kuwatukana au kudhalilisha Hakika watu watachagua kati ya ufisadi na uadilifu.
Mtu akijitikeza kukemea ubaya tumuunge mkono bila kujali Chama .