Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Hata hivyo kajitahidi kuwaacha mawaziri,mimi ningewafyeka wote hadi Igp!🏑🏒🏑
 
Unatutisha mkuu, maana haya unayoyasema hapa ni kama kweli!

1. Bomba la gesi kwenda Kenya bila shaka sasa litapewa kipaumbele zaidi.

2. Makampuni binafsi ya kutuuzia umeme, hasa kutoka Marekani, bila shaka sasa yatapigana vibega kuwekeza ili watutoe kamasi kupitia kwenye mikataba yao ya kuuza umeme.
Wewe unataka upuuzi wa TANESCO uendelee? Nilihonga hela nyingi sana kuletewa umeme home kwangu enzi hizo, kama kuna mabadiliko na yafanyike sasa
 
Sawa, Ndungulile tulimlaani.

Bado @Mwiguru Mwiguru nchemba naye ninamlaani.

Hii nchi ni ya hao hao kina januari tu akisema jakaya imepita, kwani ni lini watoto wetu wataonja keki ya taifa?

Mungu anawaona.
 
As long as Mwigulu bado yupo kwenye Baraza, naweza kusema hii haitoshi-alituambie tuhamie Burundi.

Halafu hawa kina Makamba ndio watu pekee wa kuwa Mawaziri? Ni kweli wanawazidi wenzao uwezo au ni influence tu za wazazi wao ndio zinawafanya wapate kipaumbele?

Kama si hivyo, basi ni wazi CCM kuna ombwe kubwa la watu wanaofaa kuwa viongozi katika hii nchi.

Watanzania tuendelee kudai Katiba mpya tupate watu wapya kuongoza hii nchi kwani hata hawa walioenguliwa bado kesho wanaweza kurudi tena katika Baraza la Mawaziri.

Chama kilekile, Watu walewale (wanaachiana tu viti) na matokeo yake maisha ya watanzania yanabaki kuwa yale yale miaka nenda, miaka rudi.

Pathetic!

Problems can not be solved by the same level of thinking that created them-Mchungaji Msigwa.
bahat ya wenzo silalie malango waz.
 
...
Halafu hawa kina Makamba ndio watu pekee wa kuwa Mawaziri? Ni kweli wanawazidi wenzao uwezo au ni influence tu za wazazi wao ndio zinawafanya wapate kipaumbele?

Kama si hivyo, basi ni wazi CCM kuna ombwe kubwa la watu wanaofaa kuwa viongozi katika hii nchi.
...
Japo alikuwa na mapungufu yake late Legendary Pombe alikuwa kiboko na alifaa kwa haya madudu yanayojirudia.
 
Back
Top Bottom