Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Huu uzi ufutwe umekaa kichonganishi sana,tafadhali nchi yetu msituletee mambo ya ukand nchi hii ni yetu sote
 
Bila kumtoa yule mpuuzi mvaa mabendera bado hakuna kilichofanyika

Kosa lake nini mnamchukia hivyo? Kuwaambia mlipe kodi ? Mnataka Nchi iendeshwe kwa kuomba omba kwa mabeberu until when?
 
As long as Mwigulu bado yupo kwenye Baraza, naweza kusema hii haitoshi-alituambie tuhamie Burundi.

Halafu hawa kina Makamba ndio watu pekee wa kuwa Mawaziri? Ni kweli wanawazidi wenzao uwezo au ni influence tu za wazazi wao ndio zinawafanya wapate kipaumbele?

Kama si hivyo, basi ni wazi CCM kuna ombwe kubwa la watu wanaofaa kuwa viongozi katika hii nchi.

Watanzania tuendelee kudai Katiba mpya tupate watu wapya kuongoza hii nchi kwani hata hawa walioenguliwa bado kesho wanaweza kurudi tena katika Baraza la Mawaziri.

Chama kilekile, Watu walewale (wanaachiana tu viti) na matokeo yake maisha ya watanzania yanabaki kuwa yale yale miaka nenda, miaka rudi.

Pathetic!

Problems can not be solved by the same level of thinking that created them-Mchungaji Msigwa.
Naomba kujuzwa tu kwani Dr.Faustine Ndugulile kakosea wapi? Pengine mimi sijui Naomba munijuze wana JF, nawasilisha
 
Mshana ishu so coastal Union tatizo Pamba ya kule kwa wasukuma walileta ushamba wakadhani wanaweza sana mchezo Kumbe master wapo

Katika vitu Sukuma gang walikosea ni ishu ya Lodilofa wakadhani wako stronger enough kusimama wenyewe….

Soon Membe anarudi mjini ndipo watajua hawajui…

Then nimenusa nusa mahali ule utatu mtakatifu umeinuka tena… wameamua kusameheana!!
 
Siyo kweli, kamemanii alianza kupiga sana, angalia kwenye gas na mafuta mpska aliundiwa tume ya kuchunguza.
Lakini pia walipanga kupora mgodi wa wachimbaji wadogo wadogo huko Nyang'hware geita.
 
Watanzania wote ni kitu kimoja. Tusikuze ukabila, ukanda wala udini. Kiongozi mkuu tunakuomba uzidi kuwa conscious. Corrections unazofanya awamu ya 6 ni kwa sababu awamu ya 5 ama kwa makusudi au bahati mbaya haikujali hatari katika mambo haya. Lakini muhimu zaidi, tukubali katiba ya Warioba ifanyiwe kazi na kuzaa katiba mpya yetu sote kungali na amani Tanzania. Wah.Waryoba, Polepole, Kabudi na HE Samia hawakuwa wapinzani walipoipokea katiba ya wananchi kwa sherehe. Wako wanaotaka watu tuamini dai la Katiba mpya ni la upinzani. Mnawapa sifa wao peke yao kimakosa. Ni sifa ya watanzania wote. Vinginevyo tukubali "UNAFIKI" uwe tunu mpya ya Taifa letu. Turuhusu wapinzani kwenye bunge letu ili liwe bunge hasa sio hili la sasa la hovyo kabisa. Anaeshinda kihalali ndiye watanzania wanaemtaka. Hapo tutakuwa "level" automatically.

Na jf inalea vitu kama hivi.Tusiendekeze mambo ya ukanda na ukabila kila mtu ana haki ya kuchaguliwa bila kuconsider kanda yake
 
I think we are missing back ups, alivyofariki Mh Kuandikwa imeshindikana kureplace kutoka kundi la wabunge waliopo mpaka akatafutwa nje yao. Nashauri watu mbadala wawe wanaandaliwa katika hizi nafasi kubwa.
Ifike mahali nafasi hizi zisiwe za kisiasa. Waziri atoke kwenye poll ya wataalamu nasio wanasiasa(wabunge).
 
Back
Top Bottom