Uteuzi Julai 2, 2024: Kidata aondolewa TRA, Jafo na Ashatu wabadilishana Wizara

Nchi zote zenye sheria kali za ubadhirifu, rushwa na wizi wa mali za Serikali na umma zina maendeleo yanayoonekana. Mfano mmoja mzuri ni China.

Tanzania tutabadilishana mpaka kufa, bila sheria kali za kuuwa wabadhirifu, wala na watowa rushwa, maendeleo ya haraka tuyaone kwenye TV tu.
 
Kariakoo si issue iliyomuondoa. Mambo ya Kariakoo mbona yashazoeleka?

Issue iliyomuondoa ni barua ya mabalozi wakilalamikia kodi.
Mabalozi hawatakiwi kulipa kodi? Walitozwa kodi zilizo nje ya mfumo wa sheria?
 
Hapana, ujinga upo naturally tu hauhitaji kupewa story hata kama haya matukio yasingetokea bado wajinga wasingejadili mambo serious.
 
Mwigulu na bashe bado wapo upuuzi mtupu!
 
Mna uhakika mama yupo humu jamiiforum?
Mbona mpaka sasa Lucas wangu hajatajwa🤔
Lucas yupo kamati ya mapambio na usifiaji inayofanya kazi moja kwa moja na kamati ya tiba asili na kafara.

Siku ikihitajika kafara ya mtu kwa mizimu ya kipemba, watampeleka Lucas. Hivyo usihofu yupo kitengo salama.

Tusubiri uzi mrefu tu wa machozi ya furaha ya raia kwa teuzi na tenguzi alizofanya mama.
 
Mwenda ni mtoza ushuru aka Zakayo.
Kazi za akina Zakayo tokea enzi na enzi ni za lawama,licha ya kuwa ni muhimu kukusanya fedha za kuendesha nchi.
Na ni vigumu akina Zakayo kuwa na mikono safi may be one in thousands
Labda washuke chini kutoka juu ya mkuyu kitu ambacho sio rahisi ni kigumu sababu vishawishi,matamanio
ni vingi mno.
 
Hili si tatizo; kila Mzanzibari ni Mtanzania japo siyo kila Mtanzania ni Mzanzibari. Hivyo, Mzanzibari kama Mtanzania mwingine ana haki sawa na Mnyakyusa toka Katumba Songwe.
Halikuwa tatizo lakini siku hizi limekuwa tatizo!

Wazanzibar tena Wabunge walioapa kwa katiba ya Tanzania wanapokana Utanzania ni tatizo.
Watu wanaoweza kuukana Utanzania kwasababu ni Wazanzibar wakatuacha na Utanzania wetu unawezaje kuwaamini katika masilahi ya Tanzania wakiwa wameubeba Uzanzibar Bora kwanza! uchungu wa Tanzania wanaupata wapi!

Kisheria si tatizo, lakini kwavile kuna Uzanzibar hatuwezi kukwepa kama tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…