Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)


Duuh🙄
 

And we count on them to take us off the hook🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nina imani na hii Tume kwasababu baadhi ya wajumbe wake nawafahamu kwa karibu ni watu niliofanya nao kazi, naelewa uwezo wao, uimara wao na uadilifu wao, watu wa type hii, ndio wanamsaidia Samia kwa kumwambia ukweli na sio wasaidizi wake uchumi wakiongozwa na msaidizi mkuu wa uchumi, the chancellor of exchequer ambaye ni chawa, atamsaidia nini Samia na kuisaidia nchi!
Juzi kati niliandika humu na magazetini Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..? hiki kikosi kazi kitamsaidia ila Mama nae akubali kuambiwa ukweli na afuate ushauri.

Kile kikosi kazi cha siasa jilijazwa machawa na badala ya kumsaidia ndio kwanza kimeyarudia Madudu yale yale!.
Nina imani sana na Prof. Assad, nimeisha zungunza nae sana na haya ni baadhi ya kauli zake
Huyu ataisaidia sana hii Tume na atamsaidia sana Samia kwa kumweleza ukweli.
P
 

Tume haina wahusika ambao ni wafanye biashara. Hao hawana tofauti na waziri na wabunge. Nani mfanya biashara mzoefu kwenye hayo majina. Wakati hizo kodi zinapitishwa baadhi yao walikuwepo serikalini. Ngoja muda utaamua.
 
Tume haina wahusika ambao ni wafanye biashara. Hao hawana tofauti na wazuri na wabunge. Nani mfanya biashara mzoefu kwenye hayo majina. Wakati hizo kodi zinapitishwa baadhi yao walikuwepo serikalini. Ngoja muda utaamua.
Sahihi yaani tume imejaa waajiriwa tu hawajui sector binafsi huko ilivyo sababu maisha Yao yote ni kwenye ajira tu
 
Utoto punguza ,kwa hiyo prof assad ni mtu wa kuvizia mlo? Kwenye hiyo list kuna mwenye mali chini ya bil 5?miafrika wote tuuawe mjinga sana
Sio wa kuvizia mlo wala hawana njaa hao na pia wana elimu zao kubwa tu na watu wazito sana
Ila unatarajia kodi itashuka?
Wewe ndio umekuwa mtoto kwa hasira
Tujadili tu humu kwani ukiwa na jazba utatoka kila mada umefura
 
Ni hatua nzuri lakini naona wote ni wasomi wanufaika na serikali kwanini tume isingekuwa na mfanyabiashara wa kariakoo mkubwa asiyekuwa kada wa chama ili wajue kwa kina matatizo ya kikodi na yule muhindi wa nida aliyeongea siku ile mwenye kiwanda changamoto wanazopata wazalishaji wa nguo toka kwa importers.
 
Good move lakini HAKUNA muathirika wa madhara ya kodi kandamizi katika Tume hii.
Ni wastaafu na watu wa nadharia tu.
Mfano Prof Luoga na kodi, wapi na wapi?
 
Hii tume haitaweza kuleta kile ambacho watanzania wa hitaji. Hakuna representation ya kisekta kabisa. Hao wenye vyeo hao wastaafu sina hakika kama wanafahamu mazingira halisi ya biashara.
 
Sana
 
Fursa zaidi zimetolewa kwa waliokuwa na fursa tayari.

Teuzi tunaambiwa ila budget ya hiyo tume ni siri. Ila ikija kujulikana utasikia mabilioni.
Hiyo ndo njia nzuri ya kuzungusha hela. Bila serikali kutumia pesa kwa njia mbalimbali mzunguko unakuwa mdogo. Ukiona serikali inabana sana ujue tunaoumia ni sisi. Heko mchumi Samia siyo lile lililokuwa linafikiria kubana tu tunaoumia ni sisi
 
If you think you have better ideas bring them forward, stop writing nonsense, stupid!
 
Huyu bibi ni bingwa wa kuunda tume na vikosi kazi lkn vyote havina matokeo chanya. Hata hii tume ni ulaji tu.
Mtasema sana mwaka huu, Mama yupo yupo sana huyu....mpaka 2030! CCM HOYEEEE! nani kama mama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…