Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa tenguzi hizi mbili, naona mwisho mbaya wa Mh. Samia 2025
Hawa watataftiwa kazi nyengineo, mama kashtuka na wao wanautaka urais angali yeye nae keshanogewa nao, anaona awapumzishe kwanza wasije kumpiku 2025, ila pia asipo wapa kitengo ndo mwanzo wa uhasama na watu hawa wawili, na watamvuruga sana kichwa mpaka kufika ,2025
 
Ni ngumu sana wao kufanya kama walivyofanya kwa Magu. Mbinu zao zinajulikana zote. Hawawezi kumvuruga mtu yoyote akili. Zaidi kama wanabusara, watulizane tu. Wasitumie mitandao kumchafua yoyote, wala wasifanye mbinu chafu kwenye chama. Hapa wanaweza kulainisha watu.

Wananishangaza kweli hawa wakaka.. mitaani kwa vijana waliowengi, hawakubaliki! Kama hapa mama kajizolea point za kutosha kutoka kwa watu waliokuwa hawamkubali, kisa hawa vijana. Kazi wanayo kubwa wao kurudi tena kwenye uWaziri. Na nje ya uWaziri, maisha yao huwa hayana relevance yoyote.
 
Mzee malope alipo fariki JPM ghafla alikua na furaha sasa naona leo atakua hajalala haamini kilicho tokea.Ila Maza ni noma kapiga pale pale kwenye mshono.Bado wawili yule somalia boy na mzee wa tozo hao wakitinduliwa kweli mama atakua kaamua kufanya kazi.
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Kweli siasa hazina rafiki wa kudumu. Lakini acha watoane manundu, watasaidia kujenga upinzani wa kweli kama baadhi yao wataamua kuondoka CCM.

Wakati wakiandamwa na Magufuli, Samia alikuwa anashinda kutwa nzima na January akilewa na kuvuta sigara zake.

Samia alikuwa na hali ngumu mpaka akafanya aliyoyafanya na Makonda. Magufuli alijua kuwa kuwa January ndiye alikuwa mtunza siri mkubwa wa Samia na ndo sababu ya kumtoa kwenye baraza wakati huo.

Chuki anayoijenga dhidi ya January kwa kuogopa uchaguzi wa 2025 itamtengeneza Magufuli mwingine. Hakuna mtu yoyote ndani ya CCM aliyeamini kuwa Magufuli angekuwa rais 2015 mbali na mtandao wa Kikwete na Lowassa kutumia mabilioni kumuandama toka 2005.

Siasa ni kuvumilia hata wale usiokubaliana nao kama Mkapa alivyofanya kwa Kikwete na Kikwete akafanya kwa Magufuli. Ikitokea January akiupata urais siku moja, sina hakika watoto wa Samia wataendelea kuishi nchi ukizingatia wizi walioufanya.

Tujifunze namna Magufuli alivyomtendea Kikwete na watu wengine kutokana na hasira yake kwa waliomsulubu. Tusubiri, tuone.
 
Serikali kumbe sometmes haina dhamira ya dhati,au tuseme uchawi upo, Jery silaa unamtoaje wizara ya ardhi wakati alikuwa anafanya vizuri zaidi!!? Au ndio matapeli wameenda kuroga ahamishwe wizara au atenguliwe!!! Kweli uchawi upooooo
Slaa ametolewa dhahiri ni wenye pesa wamefanya yao,sio bure.

Kwa mwendo wa slaaa waliona ataenda fukua fukua kila mahali
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Mzee wa goli la mkono alijisahau sana kamponza Byabato, eti "Nitakufundisha jinsi ya kuiba kura" 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom