Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Ajabu sana watu kufurahia hizi teua tengua, zina impact gani hasa kwenye maendeleo yetu, zaidi sana zinaturudisha nyuma.

Badala ya kufanyia kazi issues muhimu kama ripoti ya cag, tupo busy kufurahia teua, tunaamini kabisa 99% hati zilikuwa safi while the govt kumejaa madudu kuanzia local government hadi central.

Tutazidi kuhadaiwa na mambo yasiyo ya msingi hadi kizazi chetu kipite.
 
Watu wanabahati sana Dr Mhede amefeli TRA akafeli DART tena kapewa kazi?
Dr Mhede hajawahi kufeli, kwanza ni mzalendo haswa na pili ni mchapa kazi. Kumbuka yeye ndiye mwenyekiti wa bodi ya benki ya NMB ambayo ndiyo taasisi ya umma yenye mafanikio makubwa kuliko taasisi nyingine yoyote nchini. Mwaka jana kufikia robo ya tatu ilikuwa ishatengeneza faida ya bil 569 faida ambayo haijawahi kutengenezwa na taasisi yoyote nchini na bado Rais wetu alimuongezea miaka mingine mitano na mwaka huu tunategemea makubwa zaidi. Kwa wanaomjua Dr Mhede, ni zaidi ya hazina.
 
Maisha yanaendelea mganga wa kipara mkali sana!
 
Naona kabisa kwa tabia yake makonda hatamaliza mwaka arusha kama ambavyo
Uenezi amekaaa miezi michache…..
Wanamtafutia kufanyiziwa
 
Kweli mkuu hii iko wazi, ni km umepata mke anakupenda na kukuthamini halafu unaanza kumsifia ex wako, huwezi kutoboa
 
Huyu Mwl na sheria wapi na wapi
Ualimu ni Field inayoweza kumwandaa Kiongozi katika sehemu nyingi sana na akafanya vizuri tu

Mwalimu yeyote ni Mult tasking, unawezaa shangaa angewekwa Mwanasheria hapo aaingefanya lolote...ndio nchi yetu hii
 
Makonda wenye chama wameona anawadhalilisha, wameona wampangie kazi nyingine ili aisiendelee kuaibisha chama.
Makonda haaibishi chama aisee ni msumbufu tu ila ni mtu fresh hana tabu yeyote ila kwa kumpiga mke na kunyanyapa hapo simpendi nakutembea na mastaa hapo kaua ila kikazi makonda ni mtu fair kabisa . Si bira yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…