Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Mnajifariji tu......Mwenezi alikuwa juu ya Mawaziri hadi PM anabow down.
Kiukweli makonda hakuna mtu aliyekuwa anamtarajia kuwa atarudi ktk mfumo,lakini alipoteuliwa tu kuwa mwenezi binafsi sikuona akidum ktk nafasi hiyo,ile ilikuwa ni gear tu ya namna gani aingie kwenye mfumo,then apelekwe serikalini,sikia baada ya uchaguzi 2025 makonda atateuliwa tena ukuu wa mkoa then atateuliwa na mama kuwa mbunge wa kuteuliwa then apewe wizara nyeti,mambo ya ndani,utumish nk
 
Kiukweli makonda hakuna mtu aliyekuwa anamtarajia kuwa atarudi ktk mfumo,lakini alipoteuliwa tu kuwa mwenezi binafsi sikuona akidum ktk nafasi hiyo,ile ilikuwa ni gear tu ya namna gani aingie kwenye mfumo,then apelekwe serikalini,sikia baada ya uchaguzi 2025 makonda atateuliwa tena ukuu wa mkoa then atateuliwa na mama kuwa mbunge wa kuteuliwa then apewe wizara nyeti,mambo ya ndani,utumish nk
Kila la kheri ktk ndoto yako
 
Huu ni mtego kwa Makonda.Tena mkubwa sanaa.

Huenda mama ameamua kulipa fadhira akaona hafadhiriki.

Sasa amempa jiji gumu sanaa kisiasa.
 
Nguruwe hatuli peke yetu TU sisi mnaotuita wanaharamu kisa TU hatufanani Imani, tunakula pamoja na hao unaowaita ndugu zako katika Imani. Ila usione wivu sana sisi kula nguruwe, hata wewe hujakatazwa, ni shingo Yako ngumu kufuata Mila za mwarabu kwani wazee wako walikuwa wanakula hadi panya.
Mbwa na paka pia mnakula au nyinyi mnabagua vyakula?! Kuleni hata mavi ni sawa tu kwa maana imeandikwa "kiingiacho sio najisi" hata mavi ukiweza kuyameza yakaingia tumboni kwa mujibu wa biblia yenu sio najisi, kwahiyo siyo nguruwe tu kuleni mbwa, vyura, paka,panya, mijusi, majongoo na konokono vyote hivyo ni halali kwa mujibu wa maandiko mnayoyaamini!.
 
Huyo mdudu tumeharamishiwa kula, na amezungumziwa katika Qur'an, hivyo acha kupotosha watu.

Na waarabu wamewakaa kooni, hamuwapendi, chuki tuu zimewajaa vifuani, wakati wao hawana habari na wewe.

Poleni sana
Hiyo Quran unaiamini wewe. So, acha upumbavu mwingine akifuata njia tofauti. Au wewe kichaa!? Una_force kufanana!? By the way waarabu wamesababisha watani zangu kufukuzwa ngorongoro.
 
Mbwa na paka pia mnakula au nyinyi mnabagua vyakula?! Kuleni hata mavi ni sawa tu kwa maana imeandikwa "kiingiacho sio najisi" hata mavi ukiweza kuyameza yakaingia tumboni kwa mujibu wa biblia yenu sio najisi, kwahiyo siyo nguruwe tu kuleni mbwa, vyura, paka,panya, mijusi, majongoo na konokono vyote hivyo ni halali kwa mujibu wa maandiko mnayoyaamini!.
Qurani Yako ukiifata wewe inatosha. Mbona kama unachuki za kichawi!? Wewe kutokuala nguruwe kunakufanya uchukie anayekula. Mwambie huyo unayedai alikataza, akuruhusu kula.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.

iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.

v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.

vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.

ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.

xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.

xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.

xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.

Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

View attachment 2949540
View attachment 2949541
Teuzi usiku wa manane kama wachawi wa Bagamoyo na Tanga.
 
Naona Kuna uteuzi wa naibu waziri mwingine wa mambo ya ndani.
Huyu aliyekuwepo Jumanne Sagini katupwa nje ya kabinet? Maana sijaona kama kapqngiwa sehemu nyingine?
 
Kumekucha tena ! Hangaya kazini .
Hawa wateuliwa huwa wanapata muda wa kujifunza kazi kwa nafasi zao mpya wanazoteuliwa kabla hawajateuliwa kwingine tena?

Hii inaonyesha udhaifu mkubwa sana wa uongozi katika serikali hii.

Teuzi nyingi zinalenga kulinda maslahi ya walio madarakani na ni za kujinufaisha wao wateuzi badala ya kulenga manufaa ya wananchi. Sifa hii imejipambanua zaidi katika serikali hii ya Samia kuliko serikali nyingine yoyote tuliyowahi kuwa nayo. Teuzi za sasa ni za kulinda maslahi, zikilenga kuendelea kuwa madarakani baada ya chaguzi zijazo.
 
Back
Top Bottom