Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Attachments

  • 1711784558665.jpg
    1711784558665.jpg
    224.2 KB · Views: 1
Mimi sina neno wala cha kuandika leo.Maana Mama anatupatia Sapraizi Watanzania Mpaka Unaona Nchi na wananchi wakitetemeka.
Hili litakusaidia kuwa na akiba ya maneno na kuendelea kukomaa kifikra. Ulishupaza sana shingo yako kwenye hili suala, ukiandika nyuzi ndefu zisizo na kichwa wala miguu. Hii nchi waanchie wenye nchi, pambana na hali yako tu.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.

iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.

v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.

vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.

ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.

xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.

xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.

xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.

Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

View attachment 2949540
View attachment 2949541
Inaonyesha Makonda alimfanyia kitu ambacho hawezi kusahau😂. Ukichunguza kwa umakini hizi teuzi za mama hazina toka yeyote zaidi ya kupeana nafasi za upigaji kila mtu kwa urefu wa kamba yake. Poleni sana watumwa Kigoma mnazidi kupukutishwa serikalini bado mbuyu mmoja
 
Unaleta jibu la kipumbavu sana; mimi nijifariji kwa kitu gani hapa.

Soma Katiba ujue muundo wa serikali ya Tanzania na kama hujui basi uulize ufahamishwe. Elewa kuwa Balozi, Mkuu wa Mkoa na Waziri wako katika level moja serikalini.

Hata naibu waziri anasimamia wizara sehemu yote ya nchi siyo mkoa mmja, lakini naibu waziri yuko cheo cha chini kwa mkuu wa mkoa. Ni vivyo hivyo huko mawizarani kuna wakurugenzi wanasomimai kurgenzi zao nchi nzima lakini hwako lev moja na mkuu wa mkoa.

Inawezekana wewe ni mmoja wa wasiolelewa mipaka ya madaraka unadhani ni kufuatana na ukubwa wa ardhi lililo chini yako,
Acha kudanganya umma. Waziri ni mshauri wa karibu wa Rais na anaingia kwenye Cabinet kupitisha sera za wizara/nchi.

Mkuu wa Mkoa ni mtu mdogo kicheo ambaye anashughulikia zaidi mambo ya kisiasa ndani ya mkoa tu hana mamlaka hata ya kuvuka mkoa fulani.

Rais,Makamu wa Rais na Waziri mkuu wakiwa nje ya nchi kwa wakati mmoja Rais anaweza kumteua Waziri yeyote kukaimu nafasi ya Urais kwa muda hadi mmojawapo wa hao hapo juu atakporejea wa kwanza nchini.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.

iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.

v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.

vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.

ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.

xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.

xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.

xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.

Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

View attachment 2949540
View attachment 2949541
NILITARAJIA MZEE WA MAIGIZO ANGEPEWA UNAIBU WAZIRI MKUU
 
Back
Top Bottom