tamuuuuu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 21,329
- 28,063
Hao wadudu shida tupuuuNgoja tuone kama atawaweza wadudu[emoji23]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao wadudu shida tupuuuNgoja tuone kama atawaweza wadudu[emoji23]
Tuhabarishe, kwani alimfanyaje?Au ni lile suala la Salah?
🤣🤣🤣Atamleta Salaah wa Gsm kula nyamachoma kw Mromboo
Konda boy awachokoze🤣🤣🤣🤣
Mwenzake Kabudi alikuwa anamsifu Magufuli kwa kumtoa Jalalani! Imagine huyo ni Profesa.Bahati mbaya boss wangu ni shamba langu!! So mbolea ndo shukrani kwa shamba langu.... Rais ni breadwinner wa anaowapa kazi!!
Zile kauli za Makonda ooh Magufuli asitenganishwe na Samia sisi wazee wa administration theories tulijua hatafika mbali... Ndalichako naye alikua nyuma sana kwenye kumsifia her Majesty!!
Huwezi kunyqmqza hata kumtupia tusifa twilight tutatu aliyekupa uwaziri aisee!!
Nchi imejaa ujinga mwingi.Kazi kweikwei,
Huyo makonda na kutuvuruga kwa ziara zake mpk kapata ajali juzi tu hapo.
Sasa kapelekwa wapi sijui.
Miezi miwili tu kahamishwa.
Ujinga gani huu
Huyu Makonda aliwahi kuwa mkuu wa wilaya, then mkuu wa mkoa, recently katibu mwenezi, na sasa mkuu wa mkoa tena.Hakuna kitu kama hicho.
Watu wanautoroka Ukuu wa Mkoa wanakuja kwenye vyama
HahaaaBahati mbaya boss wangu ni shamba langu!! So mbolea ndo shukrani kwa shamba langu.... Rais ni breadwinner wa anaowapa kazi!!
Zile kauli za Makonda ooh Magufuli asitenganishwe na Samia sisi wazee wa administration theories tulijua hatafika mbali... Ndalichako naye alikua nyuma sana kwenye kumsifia her Majesty!!
Huwezi kunyqmqza hata kumtupia tusifa twilight tutatu aliyekupa uwaziri aisee!!
Muda wote umerudi leo? Multiple IDs 😂😂Tushwa tushwa tushwa, kashindwa kufika bei
Watatoana ngeu...Chadema tunasonga mbele mdogo mdogo na mambo yetu kimya kimya.Jumuiya ya WAZAZI CCM nako mtendaji mkuu ameonekana amepwaya.
Kila UTEUZI,Kuna Jinsia Ile inatemwa!!!TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.
iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.
vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.
vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.
ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.
xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.
xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.
xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.
Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
View attachment 2949540
View attachment 2949541
Amelipeleka lile dubwasha Arusha ili likamdhibiti Lema na CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu ujao! Wacha tuone itakuwaje!Kumekucha tena ! Hangaya kazini .
MAKONDA amekata tamaa, JK Yuko naye Kila konaAmelipeleka lile dubwasha Arusha ili likamdhibiti Lema na CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu ujao! Wacha tuone itakuwaje!
Pamoja na kulamba kalio bado umetoka patupu?Mimi sina neno wala cha kuandika leo.Maana Mama anatupatia Sapraizi Watanzania Mpaka Unaona Nchi na wananchi wakitetemeka.
Makonda ana uwezo kuliko MazaMakonda aliiweza Sana kazi ya ukatibu mwenezi
Kumtoa hapo ni kufanya kosa kubwa Sana .
Haya ngoja tuone sijui itakuwaje huko mbeleni.
Lema awe makini. Huyu mtu ni Mmoja wa walioongoza genge lilijaribu kumuua Lissu. Ni kichaa huyu.Kumekucha na nini? Makonda hataiweza na haiwezi Arusha. Akija anatakiwa awe mpoleeeee. Aliwaweza nyie wala 🍟 wa Dar ila huku haiwezi ng'ooooooo. Kashindwa Ukatibu uenezi, ataweza ukuu wa mkoa. Ptuuuuuuuu