Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi unaofanywa na Samia ni mbwembwe tu za Madaraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii teua na tengua ni kufifisha ishu ya Chadema Mbeya
 
Kuna kila sababu ya kumsaidia Samia kwa kuwa ameonyesha hafahamu nini anataka au anataka kutupeleka wapi!

Samia ni hasara kwa ustawi wa Taifa!
 
Toka maktaba :
leo Januari 10, 2022,




Bungeni Habari Siasa Zetu

Kabudi, Lukuvi wapewa nafasi Nyeti Ikulu​

3 years ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema katika Baraza Jipya la Mawaziri ameamua kuwaacha kando Prof, Palamagamba Aidan Kabudi na William Lukuvi kwa ajili ya kumsaidia kazi maalumu Ikulu.
Rais Samia ameyasema hayo leo Januari 10, 2022, katika uapisho wa mawaziri na manaibu waziri wateule aliowateua mwisho wa Juma lilipota akifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Rais samia amesema kuwa wawili hao, kutokana na umri na busara zao ameona wanafaa kuwa washauri kwa viongozi vijana walioteuliwa na kumsaidia kufanya maamuzi ya Ikulu.

“Nimeshasikia jumbe mbalimbali zinawachoma huko hawa kaka zangu kuwa ooh wameachwa, hawafai, Hapana! Hawa wamekaa muda mrefu kwenye Baraza na wanajua kila eneo, hivyo nimeamua kuwapa kazi ya kuja kwangu kuwasimamia nyie vizuri,” alisema.

“Kakaangu Kabudi amefanya kazi nzuri sana ya kusimamia Serikali na Mashirika, na ndio kazi ambayo nataka nimkabidhi sasa kindakindaki aendelee n kazi hiyo. Ila kazi yake kwa sababu haiko kwenye Muundo haitangazwi wala nini lakini atasimamia hiyo kazi. Mashirika yote na kazi zote zitakazoingia ubia na Serikali Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba.” Aliongeza Rais Samia.

Aidha amesema kuwa Lukuvi ana kazi maalumu Ikulu ambayo kwa sasa hakuitaja na akiufahamisha umma kuwa itafahika baadae.

“Wengine wameanza kumletea meseji za ajabu ajabu wakidhani atagombania uspika, hatagombania! Ana kazi na mimi kwa hiyo hatakuwa spika wala hatagombania, msianze kumchafua. Ametumikia nchi hii kwa mda mrefu na kwa uadilifu msianze kumchafua muache aende na mimi tumalize kazi tutakayompangia.” Alisema Rais Samia Suluhu Hassan


View: https://m.youtube.com/watch?v=dcWkS3YpWAs
 
Nia ni kutuzuga tu
Ni kwamba hajui nini la kufanya wala watu sahihi wa kufanya kazi gani! Katika zama hizi unamfanya mwalimu kuwa Waziri wa Afya unategemea nini! Huyu mwalimu atateua watu aina gani kuambatana naye kwenye mikutano ya WHO!
 
Huwa wanasema Mbowe kakaa sana Chadema apishe damu changa. Akina Kabudi na Lukuvi wa nini tangu TANU!
Na utakuta huyo huyo aliyepigwa chini jana, kesho tena utasikia ni waziri, yaani hata huelewi kinachotakiwa nini!! Ila kama hujui uendako huwezi potea
 
Sasa ukiangalia ni lipi la maana anafanya!! Au mama wa ngekewa(mhagama) huwa hata sielewi anafanya nini lakininpanga pangua yumo tu
Ana Mjomba wake ni Chifu kule Songea,alikuwa Bungeni amevaa mangozi ya chui🤣🤣🤣
Mkuu watu wamejipanga!
 
Hii inferiority complex ni ya mwandishi wa huu uzi. Hajiulizi kwa kina ni kwanini anatengua na kuteua wala hatafuti sababu za kitaalam za kwanini teuzi zifanyike mara kwa mara anakimbilia kuja na hoja za kejeli kwa maamuzi ya kikatiba.
 
Alivyomteua yule fala aliyeandaa mkataba wa kuuza nchi kwa DP World kuwa AG,aisee nimecheka.
This man Hamza Johari!!!!
Nchi inaliwa na sasa hivi anakwenda kuhakikisha vikwazo vyote vilivyokuwa kero kwa DP vinaondolewa!
 
Alivyomteua yule fala aliyeandaa mkataba wa kuuza nchi kwa DP World kuwa AG,aisee nimecheka.
This man Hamza Johari!!!!
Hamza Johari kaandaa mikataba mingi sana ya kiserikali kuanzia miaka ile ya 2015 alipoteuliwa na JPM kuwa mkurugenzi wa TCAA, ni mmoja wa wanasheria vichwa sana waliopo hivi sasa hapa Tanzania.

Mkataba wa DP World umeleta ufanisi mkubwa pale TPA hakuna tena magumashi wala upigaji wenye uhusiano na vyeo vya serikalini.
 
Mwabukusi huyu huyu Kajunjumele ninayemfahamu?
Zero.
 
Mchezo wa Draft, kusukuma kete hii hapa na ile kule, kisha unadai umeshinda, loh!
 
Nchi inaliwa na sasa hivi anakwenda kuhakikisha vikwazo vyote vilivyokuwa kero kwa DP vinaondolewa!
Tupunguze hizi negativity za kipuuzi. Hamza ni mwanasheria makini sana kwanza alipigania serikali ikashinda kesi ya Ziwa Malawi.

Pili kapigania shirika la mafuta kiasi kwamba serikali imepewa mkataba mzuri. Akapigania maslahi ya kimkataba kati ya serikali na DPW na tumepata mkataba mzuri ambao unaongeza mapato kule TPA.

Samia kumpa uanasheria mkuu ni baada ya kuifahamu kazi yake vilivyo kuanzia mwaka ule wa 2015 mpaka leo. SSH sio mjinga pengine sisi tunaodhani kuwa yeye ni mjinga ndio wajinga wenyewe.
 
Si mbwembwe ndugu, ni hofu ya 2025 anajaribu kubalance makundi yote ndani ya chama ili ajiweke vizuri na akubalike kwa walau 75% ndani ya chama.
Wewe ulijua kwamba wazee hao 2 watarudi baada ya kutoswa kwa wale vijana 2.
 
Hii inferiority complex ni ya mwandishi wa huu uzi. Hajiulizi kwa kina ni kwanini anatengua na kuteua wala hatafuti sababu za kitaalam za kwanini teuzi zifanyike mara kwa mara anakimbilia kuja na hoja za kejeli kwa maamuzi ya kikatiba.
Hakuna utaalamu wo wote bali ni kuogopa kivuli chake mwenyewe! Hivi kwa D zako mbili ulizopata kuna utaalamu wa kumfukuza kazi mtu na baadaye kumrudisha bila maelezo ya kutosha tena kwenye nafasi ya kisiasa!

Inferiority complex unayo wewe kukubali ujinga wa wazi kwa kivuli cha katiba!
 
Acha kujipotosha! Mkataba umepingwa na wanasheria wote nguli wa nchi hii pamoja na TLS iliyokuwa chini ya chawa wake kasoro yeye, huoni walakini hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…