Leo wakati rais Magufuli akipokea ripoti ya Uchunguzi wa Madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na Bunge, ameataka wateule wake wote waliotajwa kwenye hiyo report wakae pembeni.
Lakini Eliakim Maswi bado yupo Ofisini. Hiki kiburi anakitoa wapi?
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi naye amepaswa kupisha uchunguzi ambao Rais ameagiza ufanywe na vyombo vya ulinzi na usalama haraka iwezekanavyo.
Hizi sio zile nyakati za kuwaita watu Tumbili. Tupishe mzee, umekula vya kutosha.
Nashauri TAKUKURU waanze na wewe.
Rais John Magufuli baada ya sakata la ESCROW, alimrejesha bwana Eliakim Maswi kuwa katibu tawala wa mkoa wa Manyara baada ya kukamilisha kazi maalum aliyomtuma katika mamlaka ya mapato Tanzania(TRA).
Kabla ya kurejeshwa, bwana Maswi aliteuliwa kuwa Kaimu naibu kamishna wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA).