UTEUZI: Rais Samia afanya teuzi za Wakurugenzi Watendaji wa Hospitali ya Muhimbili na JKCI

UTEUZI: Rais Samia afanya teuzi za Wakurugenzi Watendaji wa Hospitali ya Muhimbili na JKCI

Alikuwa dakitari wa jiwe huyu!hongera sana kwake,binafsi namkubali sana amenisaidia mnooo
 
Kaka yangu Janabi umefanya kazi nzuri kwenye operesheni za moyo,sasa nimekuteua uende ukatizame kwa kina wewe na timu yako nini hasa tatizo la moyo wa hospitali ya Muhimbili.Kw upande wa mwanangu Dr Kisenge kwanza nikupe pole,viatu vya Kaka yangu Janabi ni vikubwa sana lakini kwa jicho langu legevu nimeo na naamini utaweza😁
 
Tulitarajia hilo hususani kwa Janabi, malipo hayasubiri kazi nzuri na zawadi yake.
 
Umeanza October 2 2022?
Ndiyo nchi yetu hiyo, tunakosa umakini kabisa. Makosa kama haya yanadhihirisha kuna mengine makubwa zaidi ambayo pia yanatokea na kupuuzwa.
 
Taasis ya Jakaya Kikwete ya Kisenge.

Muhimbili ya Janabi.

Safi pigeni kazi
 
Kwa nini hii taarifa imeandikwa 'London' hapo juu? Kuna umuhimu gani kufanya hivyo hata kama Rais yupo huko hivi sasa?

Wasomi wanaotakiwa watuvushe, tena wengine wana 'exposure' kama hawa kina Zuhura ndiyo hawa wanafanya kazi hivi. Au anadhani yuko BBC Swahili anarepoti kutoka London?
 
Uyo MoJa naskia ndo alikua mastermind wa kuling'oa lile jabali[emoji41]
 
Janabi yuko poa sema aache mambo yake ya ajabu ajabu mara bia inapanua moyo, mara tusile mkate, mara kunywa bia moja masaa 2, mara tembea kilomita 6 kila siku, janabi kwani umeambiwa hapa Duniani tunaishi milele?
Afu ndo dokta wake Lemutuz,
Sijui huwa anamshaur Nini[emoji1787][emoji1787]
 
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Mohamed Yakubi Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili.

Prof. Janabi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Prof. Janabi anachukua nafasi ya Prof. Lawrence Maseru ambaye amestaafu.

Aidha Rais Samia amemteua Dkt. Peter R. Kisenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Dkt. Kisenge anachukua nafasi ya Prof. Janabi.

Kabla ya uteuzi, Dkt. Kisenge alikuwa Mkurugenzi wa Tafiti na Mafunzo wa (JKCI).

View attachment 2361054
Prof Maseru alikuwa mtoto wa mjomba wa JPM
 
Back
Top Bottom