UTEUZI: Rais Samia afanya teuzi za Wakurugenzi Watendaji wa Hospitali ya Muhimbili na JKCI

Alikuwa dakitari wa jiwe huyu!hongera sana kwake,binafsi namkubali sana amenisaidia mnooo
 
Kaka yangu Janabi umefanya kazi nzuri kwenye operesheni za moyo,sasa nimekuteua uende ukatizame kwa kina wewe na timu yako nini hasa tatizo la moyo wa hospitali ya Muhimbili.Kw upande wa mwanangu Dr Kisenge kwanza nikupe pole,viatu vya Kaka yangu Janabi ni vikubwa sana lakini kwa jicho langu legevu nimeo na naamini utaweza😁
 
Tulitarajia hilo hususani kwa Janabi, malipo hayasubiri kazi nzuri na zawadi yake.
 
Umeanza October 2 2022?
Ndiyo nchi yetu hiyo, tunakosa umakini kabisa. Makosa kama haya yanadhihirisha kuna mengine makubwa zaidi ambayo pia yanatokea na kupuuzwa.
 
Taasis ya Jakaya Kikwete ya Kisenge.

Muhimbili ya Janabi.

Safi pigeni kazi
 
Kwa nini hii taarifa imeandikwa 'London' hapo juu? Kuna umuhimu gani kufanya hivyo hata kama Rais yupo huko hivi sasa?

Wasomi wanaotakiwa watuvushe, tena wengine wana 'exposure' kama hawa kina Zuhura ndiyo hawa wanafanya kazi hivi. Au anadhani yuko BBC Swahili anarepoti kutoka London?
 
Uyo MoJa naskia ndo alikua mastermind wa kuling'oa lile jabali[emoji41]
 
Janabi yuko poa sema aache mambo yake ya ajabu ajabu mara bia inapanua moyo, mara tusile mkate, mara kunywa bia moja masaa 2, mara tembea kilomita 6 kila siku, janabi kwani umeambiwa hapa Duniani tunaishi milele?
Afu ndo dokta wake Lemutuz,
Sijui huwa anamshaur Nini[emoji1787][emoji1787]
 
Prof Maseru alikuwa mtoto wa mjomba wa JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…