Oooh kumbe ni auto-correction, hapo sawa. Huwa nakereka tu ule ujinga wa kutokujua hata kuandika sawasawa halafu mtu akajifanya ni mwerevu wa mambo mazito zaidi.
Tukirudi katika huo uteuzi wa mara kwa mara unaoungelea ... sasa nikuulize kwanini raisi alipewa fursa hiyo ya kuteua na sio watu kugombania hizo nafasi? Obviously ni nafasi za utekelezaji kulingana na muongozo wa kile kinachosimamiwa na Raisi. Ikiwa hivyo ndivyo basi ana haki ya kuteua na kutengua hata kila wiki ikiwa yule aliyehisi atamfaa kufanya hiyo kazi hajafikia mategemeo yake, ama labda ameona anaweza kumsaidia zaidi kwenye nafasi nyengine.
Loyalty ni muhimu sana kwa nafasi za kuteuliwa otherwise kama mtu haamini katika kile alichotumwa basi ajiuzulu.