Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Nehemia Mchechu NHC tena? Ni sababu zipi zilipelekea kutumbuliwa? Hazikuwa genuine?Hivi hakuna watanzania wengine?
Wapo wabongo wengi wenye uwezo tatizo ni lack of connection ndugu,wanaishia tu nafasi za chini tu
 
Kama ni mjanja asiende maana huko Malawi katupiwa kaa la moto tu! Huko hakai baada ya mda wanamtumbua! Kwa ujumla hawamtaki! Maana mama hawataki kabisa watu wa Magufuli note hiyo!
siyo hawataki watu wa magufuli,hapendi kabisa kukosolewa,nadhani unakumbuka Ndugai alivokaripiwa, huyu anaenda hamalizi mwaka anatumbuliwa
 
Keshapewa Shamsi Vuai Nahodha aliyekuwa Waziri Kiongozi wa zamani
ki utaratibu ilitakiwa pole pole atangaze kujiuzuru ubunge kwanza ndiyo nafasi yake ijazwe...nakumbuka Dr. Possi alikuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais,baadae likatokea jambo la kikatiba,ikamlazimu Dr possi ajiuzuru ubunge wake alipoteuliwa kuwa balozi nadhani ujerumani
 
Nehemia Mchechu NHC tena? Ni sababu zipi zilipelekea kutumbuliwa? Hazikuwa genuine?Hivi hakuna watanzania wengine?
Nikiwaza huko kigamboni inasemekana eka moja ilinunuliwa kwa Tshs billion moja...acha tu ikae hivyo!!
 
Lands minister William Lukuvi announced in December that he was suspending Mr Mchechu to pave the way for investigations into various allegations which include abuse of office. Mr Lukuvi then tasked the NHC board of directors under the leadership of Ms Nyoni to conduct the investigations and handover the report to him.
The totozi ya mujini inakula kahawa huku imekunja nne vibarazani!

Anyway, just nature will decide
 
Rais Samia Suluhu amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Sambamba na hilo Rais Samia Suluhu amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Rais Samia Suluhu amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

Polepole na Kindamba wanatarajiwa kuapishwa kesho Jumanne tarehe 15 Machi 2022 Ikulu ya Chamwino Dodoma saa 04:00 Asubuhi.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mchechu ambaye amewahi kuhudumu kwenye wadhifa huo, anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Peter Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).

View attachment 2150380
View attachment 2150479
WAZIRI NAPE NNAUYE ALIVYOTANGAZA UTEUZI WA HUMPHREY POLEPOLE
Wala huhitaji Akili kubwa kujua kuwa Teuzi hizi zina Baraka na Maelekezo yote kutoka Msoga Chalinze.

Baada ya Kumteua Mwanae Ardhi sasa ameteuliwa mwana Mtandao mwingine hapo NHC ili Chemistry ya Upigaji na kuhakikisha Miradi muhimu ya Mstaafu inaenda kama alivyoipanga.

Nina neno moja tu kwa Polepole kwamba ajitahidi Kudadisi ni kwanini Watu ambao huwa ni Critical na Controversial hasa katika Siasa za nchini huteuliwa kuwa Mabalozi na baada ya muda mfupi huugua Ugonjwa wa Kupooza lakini pia huwa hawadumu sana Maishani.
 
Ameulamba hatimaye
IMG-20220314-WA0685.jpg
 

POLEPOLE KUWA BALOZI MALAWI…usiende.​

Ukienda unafanyiwa kile alichofanyiwa Dr Emmanuel Nchimbi kupelekwa Brazil kuwa Balozi sasa anachunga mbuzi kule Goba Dar.​

Kwani balozi wa Tanzania nchini Misri ni nani?
 
"Mwanamke hawezi ongoza nyumba"- Igbo proverb
Mama kuna mtu kamshikia mpini,mama hana namna lazima amsikilize na kumwaminu huyo mtu.
 
Back
Top Bottom