Hii nchi ya Tanganyika haina mwenyewe.
Niseheme ya kufanya anachotaka mkuu.
Kosa kubwa lilifanyika awau ya pili labkuvunja katiba na sasa awamu ya nne kwa kuteua naibu Waziri mkuu .
Nafasi ya Waziri mkuu ipo kikatiba na imeelekeza majukumu yake na upatikanaji wake lakini wameamuaakusudi kuinajisi kwa manufaa yao na kuwatwisha wananchi mzigo wa gharama na matumizi makubwa ya serikali .
Sidhani kwamba kuna nchi ya kidemokrasia duniani yenye rais mwenye mamlaka makubwa kama Tanzania. Labda nchi za kijeshi.
Wananchi walipaswa kupinga uteuzi holela wa Rais kwa sababu unawaongeza matumizi makubwa ya kodi za wananchi.
Kwa hali hii ya madaraka makubwa ya Rais kwa nchi hii ya Tanganyika yenye kuwatajirisha wageni kwa muda mfupi na kujigawia madaraka na rasilimali za umma wanavyotaka ni upuuzi mtupu kwa wapinzani kuingia kwenye uchaguzi ujao bila katiba mpya na tume huru iliyopo Kikatiba. Wanamaindikiza mwenyekiti wa CCM na chama chake kujitangazia ushindi wa kishindo .
Wapinzani wajipange tu kuanzia sasa kwa kuwaambia wazi wale wanaotaka tume huru na Katiba mpya baada ya uchaguzi 2025 eti Katba mpya ipatikane 2026 kuwa hakuna uchaguzi 2025 kama hakuna Katiba mpya.
Yaani kama Katiba mpya ni 2026 basi uchaguzi uwe 2027. Full stop.
Yaani wakilazimisha 2025 uchaguzi basi the same week ya mandalizi ya kusambaza vifaa mpaka siku ya uchaguzi ni masmdamana kuhakikisha kila kitu kinasimama.
Katiba mpya ni jawabu la kulinda rasilimali na fedha za uma na haki na kulinda uhuru na uchumi wa Tanganyika.
Hawa watu wanadanganya sana .
Huyu Rais akirudi 2025 wapinanza wasahau kabisa kabisa Katiba mpya.
Samia atatishwa na kundi la matajiri na mafisadi kwenye Chama kuwa Chama kitafia mikononi mwake na hawapo Tayari kwa hilo na yeye wamemweka wao kulinda Chama na Katiba iliyopo sio vinginevyo.
Baada ya ushindi na Katiba kukosekana Rais aliyepo atataka kumaliza muda wake na chama kitakuwa na watu wenye uchu mkubwa na tamaa kubwa sana ya kuingia Ikulu . Hawa hawatakubali kuikosa Ikulu ya Tanganyika yenye maslahi ya kuchota na kukimbia kwa uhuru kabisa.
Niwaambe tu wapinzani bàada ya 2025 Katiba mpya Itapatikana kwa nguvu kubwa sana na dola itatumia nguvu kubwa sana kwa sababu utakua wakati wa Watanganyika ndani ya Mfumo na mifumo ndani ya vyombo vyote kujipanga 2030 kwa kuwaza mali za kujichotea na kuteuana wanavyotaka.
Kwa hiyo walinzani washtuke kabla ya 2025 Bila Katiba mpya wajue katiba mpya itapatikana kwa yao wenyewe na wananchi watakua wamekata tamaa kuwa sasa Hakuna cha kufanya ni kuacha CCM wafanye wanavyotaka wenyewe na nchi yao .
Yaani nchi ya Ajabu ambayo Rais Mstaafu ana nguvu kubwa ya kuweka anayemtaka na kumsimamia bila katiba mpya kabla ya 2025 ni wazi haitakuja kirahisi kamwe.
Ni bora kuitafuta kwa nguvu kubwa sasa kuliko kuitafuta wakati wakina Makamba ,Mwigulu,Ridhiwani,Nape ,Kigwangala, Makonda ,Polepole , ,Biteko,Mpina wakiwa wanajianda kutumia Wakurugenzi na Tume kumweka Rais wa makundi ndani ya CCM.
Walinzani wasibweteke kwa wakati huu wa Rais wa awamu ya Tano na ya mwisho wa Ilani ya JPM na CCM ya 2020 mpaka 2025 ni kipindi cha mpito wa Rais aliyefia madarakani .
Anaweza akasema anaileta 2026 na yale makundi ya kuelekea 2030 kwenye urais wa CCM yakauvuruga kama kipindi cha Samweli Sita na makundi yao walivyouvuruga uchaguzi