UTEUZI: Rais Samia ateua Balozi mmoja na kumhamisha Humphrey Polepole kuwa Balozi nchini Cuba

UTEUZI: Rais Samia ateua Balozi mmoja na kumhamisha Humphrey Polepole kuwa Balozi nchini Cuba

Ama kweli mambo yamebadilika na JPM hayuko tena duniani.

Hadi wewe Kichuguu tunayekufahamu mtetezi wa kila jambo la serikali leo unalalamika!

Inashangaza sana.

Watu wanamsema Pole Pole wanasahau kuwa Mlowola aliyekuwa Cuba hakupangiwa popote.

Hata hivyo, tabia ya kuteua kutengua na kubadili mara kwa mara haijengi ufaninisi kiutendaji. Ni kweli kuna haja ya kuwaondoa walioshindwa kazi lakini siyo hii ya dana dana ya kila baada ya wiki mbili
 
Tuliosomea Cuba tunaelewewa.
Mr pole pole kapelekwa mbali na Tz kusudi kuvuruga zile movements zake za chini chini.

Maana ilikuwa haipiti mwezi bila kuja Tz.

Next stage watamla kichwa kabla ya 25.
Japo, hii itakuwa risk kwa SSH.
Maana watamrahisishia mipango yake.
Naliona hili pia
 
Movement zipi Mkuu? Polepole ni nzi tu CCM hakuwa hata na miaka 5 so Hana hiyo power mnayofikiria anayo. Kahamishwa Ili tu asipige kelele awe busy muda wote ila Sio kwamba ana uwezo wa kushawishi chaguzi za 2025.

Kama kinana, makamba, membe n.k walikua na miaka zaidi ya 40 CCM walitulizwa na JPM walipotaka kumuondoa 2020 ndio sembuse Polepole na Bashiru waliokaa 5 years pekee?? Mkuu CCM Ina wenyewe na ndio waliokamata serikali so hao kina Kabudi, Polepole na Bashiru ni wageni tu
Mbona mnaweweseka mkimsikia shujaa polepole?
 
Polepole ameponzwa na kitendo Cha kutaka kupoka madaraka ya amiri Jeshi mkuu kwa kutamka salamu ya "himahima" Tanzania....ni kwa wale wanajeshi waliokuwa wanaenda Malawi kutoa msaada. Akilenga umaarufu binafsi wakati akijua wale wameenda kwa amri ya SSH. Mwanajeshi anatakiwa kumtii amiri Jeshi pekee,au bosi katika mfumo wa kijeshi.

Pia muda mwingi alikuwa anazurura tu Tanzania bila kufanya kazi. Mara Yuko Sinza, mara Mbeya. Sasa ngoja akajifunze maisha Mapya na watu wasiojua kingereza au kiswahili.

Sasa hivi akipost jambo Instagram linapata likes kumi au mia, message hazifiki 50. Muda utasema, na Diblo Dibala anahaha tu. Diblo Dibala ndiye mgombea pendwa wa Polepole ...bado Wana Nia ya kurejesha utaratibu wa kutupa watu baharini, kuteka, na kubambika kesi, kujizolea fedha kwenye akaunti za watu.

Watanzania wengi wivu na majungu huwa vinalimit na ku influence aina ya kufikiria kwenu. Kwanza mlidai katupwa ka nchi kadogo Tu kaafrica. Sasa kahamishwa kwenda Cuba ningezani mngesifia kuwa bado anatambulika, Ila mnakuja na hoja za kikombe kipo nusu empty Badala ya kimejaa nusu. Msiwaze mbali sana wabongo. Maisha Kama Sio yako binafsi huwezi kuyapangia na kuyapatia.
 
Ninashauri: 1. January makamba
2. Nape Mnauye
3. Mwigulu Nchemba
4. Riziwani Kikwete
5. Doto Biteko
6. Hussein Bashe
Wote nilio wataja hapo juu, Wateuliwe kuwa mabalozi wa kuiwakilisha Tanzania nchi watakazopangiwa itapendeza na itapunguze ufisaidi mkubwa .
 
Ila kiukweli aina ya watu kama Mh. Balozi Polepole huwa wanakuwa viongozi wenye ushawishi mkubwa sana..
Natamani kumwona siku moja akiwa Rais wa nchi yetu.
 
Polepole ameponzwa na kitendo Cha kutaka kupoka madaraka ya amiri Jeshi mkuu kwa kutamka salamu ya "himahima" Tanzania....ni kwa wale wanajeshi waliokuwa wanaenda Malawi kutoa msaada. Akilenga umaarufu binafsi wakati akijua wale wameenda kwa amri ya SSH. Mwanajeshi anatakiwa kumtii amiri Jeshi pekee,au bosi katika mfumo wa kijeshi.

Pia muda mwingi alikuwa anazurura tu Tanzania bila kufanya kazi. Mara Yuko Sinza, mara Mbeya. Sasa ngoja akajifunze maisha Mapya na watu wasiojua kingereza au kiswahili.

Sasa hivi akipost jambo Instagram linapata likes kumi au mia, message hazifiki 50. Muda utasema, na Diblo Dibala anahaha tu. Diblo Dibala ndiye mgombea pendwa wa Polepole ...bado Wana Nia ya kurejesha utaratibu wa kutupa watu baharini, kuteka, na kubambika kesi, kujizolea fedha kwenye akaunti za watu.
Sawa bwana Malope
 
Back
Top Bottom