UTEUZI: Rais Samia ateua Majaji wa Mahakama Kuu

mbona date ni August 23, 2022? Au mimi ndiye sielewi? Lusungo
Funguwa macho yako vizuri, uteuzi umefanyika tarehe 4 mwezi wa 8, tangazo la uteuzi limetoka leo tarehe 6 mwezi wa 8, hiyo tarehe 23 iliyopo chini inasisitiza kampeni ya sensa inafanyika tarehe 23 mwezi wa 8.

Punguza K- Vant.
 
Mayala vipi, maana naye hujinasibu kama mwanasheria.
Mayala hajawahi kupractice uwakili, hapo wenye sifa ni kariba ya Kibatala na awe amefanya kazi yake ya uwakili kwa miaka 15 ndio anakuwa kwenye sifa yakuteuliwa kuwa Jaji na bado kuna mambo mengi yanazingatiwa pia.
 
Mbona uteuzi umefanyika tarehe 4? au hamsomi documents?
 
Mkuu Pasco,tafadhali jiangalie katika kipindi hiki,vinginevyo lile jambo letu litayeyuka punde.
 
Hao manaibu wasajili wa mahakama huwa wanafanya kazi gani? Mbona ni wengi sana?
 
..Nimeona kuna Mzanzibari ameteuliwa.

..Hii ni mahakama kuu ya Tanganyika, ndugu zetu wa Zanzibar wanayo.mahakama kuu yao.

..Mzanzibari anaweza kuteuliwa ktk mahakama ya Rufaa kwani hiyo ni ya muungano.
 
Mkuu Pasco,tafadhali jiangalie katika kipindi hiki,vinginevyo lile jambo letu litayeyuka punde.
Kiukweli nimekuwa natatizwa na kuwa mkweli daima. Kwenye lile jambo letu, nimeliomba kwasababu najijua nina uwezo wa kusaidia kitu, kama nitakatwa kwasababu ni mkweli too much, then be it!.
P
 
..Nimeona kuna Mzanzibari ameteuliwa.

..Hii ni mahakama kuu ya Tanganyika, ndugu zetu wa Zanzibar wanayo.mahakama kuu yao.

..Mzanzibari anaweza kuteuliwa ktk mahakama ya Rufaa kwani hiyo ni ya muungano.
Elimu ya uraia inahitajika sana hata kwa GT wetu humu. Mzanzibari kwanza ni Mtanzania ana haki zote za Mtanzania kama Mtanzania mwingine yoyote ikiwemo haki ya ajira ndani ya serikali ya JMT.

Uzanzibari wake ni an added advantage kwa Zanzibar ambayo Watanzania Bara don't enjoy!.
P
 
Mafuta yamepanda sana na hali ya maisha ni sana mama
 
Nani kakudanganya bongo watu wanazingatia weledi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…