UTEUZI: Suzan Kaganda ateuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu

UTEUZI: Suzan Kaganda ateuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu

Huyu mama akiendelea na msimamo huo, heshima itarudi kwa jeshi la polisi. Kwa sababu wanao lichafua jeshi hilo ni baadhi tu.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Wakulyamba hakustahili kupata Ukamishna tangu mwanzo!!,nadhani mnakumbuka ile hotuba ya Mh.Rais kuhusu Mafuta!!,Sasa huyu ndio alikuwa Mlengwa Mkuu
 
Hongera sana Suzan Kaganda... kipindi yupo RPC kinondoni wakina paul makonda walimchongea mama wa watu mpaka akapelekwa makao makuu ... eti rpc knd anachukua hela kwa wafanyabiashara wa shisha na wauza unga
Makonda alimchukia sana. Kipindi Nape anatishiwa na Bastola, Kaganda alitaka aliyefanya hivyo atafutwe. Ndo akatolewa kwenye RPC wakampeleka makao Makuu akose nguvu za kulisimamia.

Nakumbuka siku Nape anatishiwa alikuja eneo la Tukio kvama dakika 5 tu baada ya tukio.. Wale jamaa walijua wakapanda gari nyeusi wakaondoka.

Soon naye akafika. Alikuwa kavaa zake Sketi na shati jeupe na miwani. Mnyenyekevu sana. Akienda msibani kama hayupo kazini, anavaa zake dera na unamkuta jikoni akisaidiana na watu wengine kupika chakula.

Hadi uambiwe huyu ni bosi Polisi vinginevyo huwezi kumjua
 
Kamishna Kaganda ndiye angefaa kuwa IGP
Na ndiyo anaandaliwa taratibu kwani tayari Poti wangu wa Kizanaki na Kikurya ( kutoka Mkoani Mara ) ameshaanza kuonyesha Mapungufu maeneo fulani japo anajitahidi kuweka sawa lakini Rekodi zake za Kiutendaji na mengine yanayoibuliwa yanaanza kumuweka katika hatihati ya kuendelea Kudumu katika hiyo Nafasi.

Hata hivyo asihofu GENTAMYCINE naendelea Kumuombea kwa Mizimu ya Kwetu huko ili adumu, haya Majaribu yapite na Mama (Mtemi wa Kike) aendelee Kumuamini.
 
Mmmh nijuavyo huyo jamaa ni mcha Mungu sana kuliko askari mwingine yoyote niliywahi kuona.
Sema hanaga msaada kivile.

Namfahamu kuliko
Kutokua na msaada,hiyo ni hulka ya watu karibia wote wenye asili ya Sumbawanga,they never help their people.Wakifika levo flani,aisee bora wamsaidie mtu baki na siyo wa kwao.Ni hopeless kabisa hayo majamaa.
 
Huyu mama hata u IGP anaumudu.
Hivi kaolewa huyu mdada?
 
Rais wa Tanzania ana majukumu mengi sana
Kabisa, yaani haya majukumu mengine yalitakiwa kufanywa na IGP au sekretarieti maalumu kutokana na katiba.

But hii ya sasa mmmh ni mantanange!.
 
Polisi hawawezi kumfurahia huyo mama maana aliwachana sana live kuhusu Rushwa , kuna clip yake maarufu sana inatembea inatembea mitandaoni akiwachana wenzie waache kujifanya miungu watu kwa kulazimisha rushwa kwa mitutu ya bunduki, kimsingi ni mama mwenye IQ kubwa huko pilisiisiiemu ila hawawezi kumpa cheo kikubwa sana maana itakua at their own disposal amri za kifala kama zile za wale waliomsimaisha mnyika Morogoro wala hatazikubali. Akili ni nywele
 
Huyu ndio anaandaliwa kuja kua IGP , halafu huyu ni mtu mzito sana hata hapo alipo ana mizizi kwenye hizi serikali za bongo sio mtu wa kuondolewa sehemu yoyote kirahisi rahisi tu...Hongera sana Suzie Kaganda IGP mtarajiwa. asie na masikio na askie sasa.
 
Rais Samia Suluhu Hassana amempandisha Cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi.

View attachment 2396498
Vile Vile Rais Samia amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi. Kamishna Kaganda anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi (CP) Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi umeanza rasmi.

Tazama video hapa chini kuona alivyowafokea Trafiki wanaoendekeza Rushwa




Sijamuelewa Kamanda huyu wa polisi anaposema haya:
1. "haiwezekani askari unaomba rushwa mpaka unatumia nguvu." Je, hapa kwake issue ni nguvu au rushwa?
2. "inapofikia unatumia nguvu ya ziada kuomba rushwa." Je, hapa issue ni kutumia nguvu ya ziada au rushwa?
3. "ili upate rushwa kwa makosa yasiyokuwepo." Je, issue hapa ni makosa yasiyokuwepo au rushwa?

 
Abaki wa nini yule katili linafokea kila mtu bila kujua wengine ni vijana wa kanisani sasa wacha akasome magazeti pele makao kwanza
Ila ukumbuke mwenzako tayari ni kamishna(CP). Tayari ameshafanikiwa hata kama wewe unafurahia kuondolewa nafasi ya uongozi.
Ukute wewe constable tu umejichokeaaa na huongezeki vyeo sababu ya WIVU na CHUKI TU KWA WENZAKO.

Kataa hiyo roho
 
Back
Top Bottom