Uteuzi wa Biswalo Mganga kuwa Jaji wa Mahakama kuu kupingwa Mahakamani, Yadaiwa hana Maadili, zuio la kuapishwa kwake laandaliwa

Uteuzi wa Biswalo Mganga kuwa Jaji wa Mahakama kuu kupingwa Mahakamani, Yadaiwa hana Maadili, zuio la kuapishwa kwake laandaliwa

Hivi Huwa mkimbizi anajihusishaje na mambo ya nchi yake?mie sijaelewa kabisa.naomba kuelewa
 
Tumeanza maandamo hapa
Sifa ya mtu kuwa DPP ni lazima awe na vigezo/sifa ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hivyo Biswalo tayari alikuwa na sifa za kuwa Jaji wa Mahakama Kuu toka siku aliyoteuliwa kuwa DPP, njia za kumuondolea sifa hizo ni kwa uamuzi wa Rais kumuundia baraza la kumchunguza tuhuma za kwenda kinyume na maadili, Rais hajafanya hivyo, Mahakamani tafsiri itakuwa nyeupe tu kuwa huyu mtu bado ana sifa za kuwa Jaji maana ni DPP.

Njia nzuri na labda sahihi ya kumuondoa Biswalo katika nafasi hiyo ni kwa kumshinikiza Rais kutengua uteuzi huu kwa maslahi ya umma kwa kutumia labda maandamano ya amani.
 
Lema bana,eti kaagiza mawakili wake wazuie uapisho wa jaji
Mtu akisheteuliwa kuwa jaji,ni kamati zao tu za kimaadili zinaweza kupendekeza atenguliwe,sio mahakama
Akiisha apishwa. Kwa sasa hajaapishwa bado. Ndiyo maana Lema anazungumzia kuzuia kuapishwa.
 
Nimesoma uteuzi wa Majaji uliofanywa na Mh Rais ,nimeelekeza Mawakili wangu waweke pingamizi mara moja la kuzuia kuapishwa kwa aliyekuwa DPP Biswalo Maganga kuwa Jaji wa Mahakama kuu,hana sifa wala maadili ya kuwa mwamuzi wa haki za Watanzania,anastahili kuwa jela au jehanamu.
View attachment 1781259

Mytake : NI AIBU KUBWA SANA KWA MTEULE WA RAIS KUPINGWA MAHAKAMANI .


Wekeni majina ya hao majaji humu ndani wengine tuko remote bado hatujayaoni
 
inamaana inawezekana Uteuzi wa Majaji ukafanyika kwa kujuana juana tu na kuwekana wekana tu!! siamini hata kidogo.

tatizo watanzania tumekuwa na tabia ya kupigana fitina na majungu sana kwa lengo la kuharibiana.

Biswalo amefanya kazi zake akiwa DPP kwa mujibu wa taratibu na sheria, amefanya kazi kubwa sana ktk Taifa hili na hivyo anastahili kabisa kuwa Jaji wa mahakama kuu.
Ngoja Mahakama iamue
 
Nimesoma uteuzi wa Majaji uliofanywa na Mh Rais ,nimeelekeza Mawakili wangu waweke pingamizi mara moja la kuzuia kuapishwa kwa aliyekuwa DPP Biswalo Maganga kuwa Jaji wa Mahakama kuu,hana sifa wala maadili ya kuwa mwamuzi wa haki za Watanzania,anastahili kuwa jela au jehanamu.

Mytake : NI AIBU KUBWA SANA KWA MTEULE WA RAIS KUPINGWA MAHAKAMANI .

Pia soma
Is there any substantial evidence that backs up that Biswalo Mganga is implicated in office abuse as quoted from the two attached threads and personal opinion by Godbless Lema a none legible fugitive in Canada? Is it justifiable for a none legible fugitive to curse a judiciary appointment into office suggesting Biswalo Mganga was not qualified to be a judge and that he was liable to be imprisoned or lamenting in hell. Does Godbless Lema have the moral authority to subscribe to such a punitive statement against a judiciary appointee?

Were you comfortable quoting such an animosity statement and post on the public shared platform and for what targeted purpose?

Personal hatred is now ground being staged by haters of all colors will surface beyond the expectations as the current regime enjoys seeing these kinds of confrontations prevail in the country.
 
Lema ni mkimbizi, afanye shughuli za wakimbizi huko,maji yalimzidi akayakimbia.
Afahamu kuwaTanzania ni sovereign state,inaendeshwa kwa katiba,sheria ,kanuni na taratibu ilizojiwekea ,yeye alikwishahamia nchi nyingine, mambo ya Tanzania ayaachie watanzania wenyewe wanaoishi Tanzania kila mwaka siku 365, yeye keshapoteza credibility.
Anakosa vipi credibility wakati bado ni mtanzania? Haki ulizonazo wewe hta lema pia anazo shida ipo wapi?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mkimbizi Godbless Lema unao ushahidi usioacha shaka kwamba Biswalo hana maadili?
Au ni chuki zako binafsi zinakutesa?
 
Chadema wanadeal na mambo ambayo hayagusi kundi kubwa la Watanzania bali ni ya ubinafsi wao tu. Watu wana shida ya maji, barabara mbovu kwa baadhi ya maeneo ya nchi lkn hawayaongelei bali wamebakia umbea tu mara Sabaya, DPP...!!!
Kwamba huoni shida majambazi kuingia kwenye mifumo muhimu ya utoaji haki? Hizo barabara na maji utapatia wapi ukiwa na mijambazi hii? Jipime akili
 
Mi sioni kama kuna shida hapo. Mahakama ipo kwa ajili ya kutafsiri sheria, itaamua Kama ni sahihi ama vp. Tusianze kumpa Mama Samia umungu wa kutokukosea kama tuliompa Magufuli hadi akajiona yeye ni mungu na watu wote ni takataka tusioweza kumfanya kitu
 
Imekuwa ni desturi kwa chadema kujiona wana haki ya kukosoa tu!
Kwa muda mrefu uhuru wa habari kichwani mwa Chadema unamanisha ni kutukana na kukosoa wengine ila wao kukosolewa hapana.

Ukiwakosoa chadema watakuita ni dikteta ila wao wakikukosoa wanaita ni uhuru wa habari!!!

Kitendo cha Chadema kuanzisha kampeni ya kuunfollow Clouds kisa tu wamehoji watu wanaowakosoa siyo haki kabisa na ni unyumbu na uzwazwa wa hali juu kwenye chama hicho.

Jiulize kama Lema ambaye hana cheo chochote anaishi kwa kulelewa na wanaume wenzake huko Ulaya anaweza kuanzisha kampeni ya kipuuzi namna hiyo kisa tu dikteta Mbowe amekosolewa, vipi Lema angekuwa rais wa nchi angechukua hatua gani kwa clouds na wakosoaji wa mienendo ya Chadema?

Bila shaka chadema wanaohubiri demokrasia na uhuru wa kutoa maoni hawana chembe hata tone la uvumilivu pindi wanapokosolewa.
Nimevutwa zaidi na sentensi hii, nanukuu;

"...Lema ambaye hana cheo chochote, anaishi kwa kulelewa na wanaume wengine Ulaya, anaweza kuanzisha kampeni ya kipuuzi...."

Nadhani una tatizo ktk fikra zako. Una tatizo kubwa la kufikiri vizuri na kuamua...

Ukipenda na ukiwa na muda tunaweza kujadiliana lakini kwa kwanza wewe kujibu maswali haya muhimu kwa faida yako:

1. Wewe unadhani ukiwa na "cheo fulani" ndiko kunamfanya mtu aishi vizuri? How?

2. Wewe hapo ulipo inaelekea una "cheo fulani kizuri" sana huko CCM na kwa hiyo hulelewi na wanaume/wanawake wenzio, au siyo?

3. Goodbless Lema hajaanzisha kampeni yoyote ili aungwe mkono. Godbless Lema katoa taarifa kuwa atapinga uteuzi wa Biswalo Mganga mahakamani kutokana na sababu za kimaadili. What's wrong with that hata uanze kung'aka kiasi hicho kama vile hiyo no ajabu sana?

Kama sheria zetu zinaruhusu raia kupinga hilo mahakamani, acha iwe hivyo na mahakama itaamua...

4. Mwisho, unaelewa maana ya "analelewa na wanaume wenzake?"

Kwa manufaa yako acha kujivunia dhambi zisizokuwa na sababu kwa kuzushia watu wengine mambo ya hovyo. Mfano una uhakika kuwa Lema "analelewa na wanaume wenzake?"

Au na wewe ni walewale wazushi na wambea wa kuhamisha hamisha maneno bila kuwa na uhakika wanachokisambaza na wakiulizwa unaweza kuthibitisha, wanaishia kusema, "...mimi nimesikia tu wanasema sema huko sokoni...!!"

Acha hizo bwana...
 
Back
Top Bottom