Imekuwa ni desturi kwa chadema kujiona wana haki ya kukosoa tu!
Kwa muda mrefu uhuru wa habari kichwani mwa Chadema unamanisha ni kutukana na kukosoa wengine ila wao kukosolewa hapana.
Ukiwakosoa chadema watakuita ni dikteta ila wao wakikukosoa wanaita ni uhuru wa habari!!!
Kitendo cha Chadema kuanzisha kampeni ya kuunfollow Clouds kisa tu wamehoji watu wanaowakosoa siyo haki kabisa na ni unyumbu na uzwazwa wa hali juu kwenye chama hicho.
Jiulize kama Lema ambaye hana cheo chochote anaishi kwa kulelewa na wanaume wenzake huko Ulaya anaweza kuanzisha kampeni ya kipuuzi namna hiyo kisa tu dikteta Mbowe amekosolewa, vipi Lema angekuwa rais wa nchi angechukua hatua gani kwa clouds na wakosoaji wa mienendo ya Chadema?
Bila shaka chadema wanaohubiri demokrasia na uhuru wa kutoa maoni hawana chembe hata tone la uvumilivu pindi wanapokosolewa.
Nimevutwa zaidi na sentensi hii, nanukuu;
"...
Lema ambaye hana cheo chochote, anaishi kwa kulelewa na wanaume wengine Ulaya, anaweza kuanzisha kampeni ya kipuuzi...."
Nadhani una tatizo ktk fikra zako. Una tatizo kubwa la kufikiri vizuri na kuamua...
Ukipenda na ukiwa na muda tunaweza kujadiliana lakini kwa kwanza wewe kujibu maswali haya muhimu kwa faida yako:
1. Wewe unadhani ukiwa na "cheo fulani" ndiko kunamfanya mtu aishi vizuri? How?
2. Wewe hapo ulipo inaelekea una "cheo fulani kizuri" sana huko CCM na kwa hiyo hulelewi na wanaume/wanawake wenzio, au siyo?
3. Goodbless Lema hajaanzisha kampeni yoyote ili aungwe mkono. Godbless Lema katoa taarifa kuwa atapinga uteuzi wa Biswalo Mganga mahakamani kutokana na sababu za kimaadili. What's wrong with that hata uanze kung'aka kiasi hicho kama vile hiyo no ajabu sana?
Kama sheria zetu zinaruhusu raia kupinga hilo mahakamani, acha iwe hivyo na mahakama itaamua...
4. Mwisho, unaelewa maana ya "analelewa na wanaume wenzake?"
Kwa manufaa yako acha kujivunia dhambi zisizokuwa na sababu kwa kuzushia watu wengine mambo ya hovyo. Mfano una uhakika kuwa Lema "analelewa na wanaume wenzake?"
Au na wewe ni walewale wazushi na wambea wa kuhamisha hamisha maneno bila kuwa na uhakika wanachokisambaza na wakiulizwa unaweza kuthibitisha, wanaishia kusema, "...mimi nimesikia tu wanasema sema huko sokoni...!!"
Acha hizo bwana...