Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

Huyu kwa ndoto niliyoota jana hatahudumu kama DG mpaka 2025
 
Hakuna sehemu nimesema tufute wizara ya fedha au jeshi tubaki na TISS. Wala hakuna sehemu nimesema China iliendelea kwa kuiba teknolojia pekee. Kwani terabytes za data za F-35 walizochukua China zilikuwa za kutengeneza online game? Au blueprint ya atomic bomb waliyochukua USSR haikusaidia.

Hayo mageuzi makubwa ya uchumi unayosema ya China kwani hayana nyenzo na mbinu tofauti au kuna kitu kimoja fixed kinaitwa mageuzi ya uchumi.

Nimekuuliza swali quote ya mwanzo, kama hutaki TISS ihusike kiuchumi kwanini unataka ihusike kiusalama na kiulinzi wakati tuna Wizara ya Ulinzi na tuna Wizara ya Mambo ya Ndani, ambazo zote hizo haziisimamii TISS. Unamaanisha tuifute
 

Bro hili gazeti lote ni langu kwa kale kaparagraph kamoja?
 
Isingekuwa Rahisi mkurugenzi aliyesimamia kuhakikisha vyombo vinazuia uhuru wa watu Kutoa maoni,

Asingeweza kubadilika ghafula kupeleka vyombo kulinda WAPINZANI mikutanoni.

BARAZA la mawaziri soon litafanyiwa changes, Mwigu na Marope wanaelea kama unnyoya.
 
Sawa, ni wazi TISS wanakazi kubwa sana, kwamba wanapaswa kujua kama IQ ya mtanzania inapanda au inashuka! Kama hili nalo ni jukumu la tiss, basi naamini mfumo wa elimu ungekuwa ulibadilishwa zamani
 
1)utoroshwaji wa rasilamali za nchi kama madini,wanyama,pembe za ndovu n,k
2)mikataba mibovu na upigaji unaosababisha upotevu wa fedha nyingi.
πŸ‘†
akuna namna tiss wakahusika kudhibiti hayo mambo.yamekua yanafanyika sana mpaka yanakera.
 
Hakuna mzee mwenye mtazamo tofauti na uliomkuza. Yeye anaamini CCM itatawala milele. Mtu kama huyo hana mtazamo tofauti na huo. Sana sana ataishia kuleta porojo.
Umenena !
 
Afadhali umempa ufafanuzi kijana wetu, neno Usalama wa Taifa ni Pana sana zaidi ya kushika mabunduki na kulinda viongozi wa CCM .

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Sawa, ni wazi TISS wanakazi kubwa sana, kwamba wanapaswa kujua kama IQ ya mtanzania inapanda au inashuka! Kama hili nalo ni jukumu la tiss, basi naamini mfumo wa elimu ungekuwa ulibadilishwa zamani
Ukisoma stori yote utaelewa ninasema nini? Usisome sentensi ya mwisho peke yake. Usalama wa Taifa unahusu mstabali wa Taifa. Masuala ya siku hata siku ni muhimu kwao kama yanatishia uwepo wa uwepo na ustawi wa mipaka ya nchi na wananchi wake. Kuna taasisi nyingine ambazo zinahusika na masuala ya siku hata siku. IQ hutokana na lishe, hususan protein, kuanzia kabla mtu hajazaliwa kisha huyo mtu kulelewa kwa matunzo ya kiafya, elimu sahihi na uongozi bora. Haya ni masuala ya muda mrefu na ni muhimu kwa Usalama wa Taifa ukisaidiwa na viongozi wa siasa wanakuja kwenye awamu tofauti. Huoni historia na maendeleo ya nchi zenye Usalama wa Taifa unaoeleweka?
 
Asante kwa elimu nzuri,ubarikiwe.
 
Ninachokipinga kwa nguvu zote ni hiki;
"Sera ama Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi kwakuwa hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe katika misingi ya Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI)"

Aidha natambua polisi, jeshi, mgambo, immigration na hao idara kwa namna moja au nyingine wanahusika na hali ya uchumi "indirectly" kwa kuhakikisha usalama, amani, kuzuia hujuma n.k katika wigo husika na mahususi wa majukumu yao.
 
Wewe jamaa mbishi wa asili yaonekana,ujasusi unafanyika popote pale iwe mambo ya uchumi,kijamii ama kisiasa,taarifa yoyote inayopatikana kupitia hizo sehemu na ikachakatwa tayari kwa matumizi huo tayari ni ujasusi.Yapo Mashirika makubwa Duniani binafsi yanafanya ujasusi wa kiuchumi kwa wawekezaji na nchi kwa ujumla hivyo hivyo Serikali kupitia vyombo vyake vya ujasusi wanafanya.
 
Mashirika ya kijasusi ya Nchi yapo yanayomiliki Makampuni na Taasisi nyingine za kibiashara ila kupitia hayo Makampuni ndiyo shughuli za ujasusi hufanyika,kubali kupata elimu utajifunza zaidi.
 
Hata Polisi wana cover almost sector zote.
Uko sahihi hapa sasa ndiyo uone dhana pana ya kitu kinaitwa ujasusi,Hao Polisi wana Bureau of Criminal Intelligence(Imewahi kuongozwa na Aliyekuwa DGIS) wana madawati tofauti moja wapo ni la uchumi,lakini pia Ofisi ya CAG Polisi ni wengi wote hawa wapo kufanya shughuli za kijasusi katika milengo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…