Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu kwa ndoto niliyoota jana hatahudumu kama DG mpaka 2025Pengine huu ni mwanzo mpya wa mageuzi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mabadiliko haya ya uongozi yana maana kubwa sana kwa Idara yetu, ni matumaini yangu kwamba mabadiliko yatakwenda mbali zaidi kuguza muundo wa idara, mfumo wa idara, sheria na kanuni za idara ili kuendana na ulimwengu mpya wa dunia ya sayansi na teknolojia.
DGIS mpya Ndugu Said Masoro si mtu maarufu katika korido za Ujasusi Dar es Salaam ukimlinganisha na mtangulizi wake Athuman Diwani ambae umaarufu wake ulijengwa akiwa Intelijensia ya Polisi, DCI na katibu Tawala, Masoro anaweza kuwa chachu ya magezi ya chombo hiki muhimu na uti wa mgongo wa taifa letu ikiwa hataruhusu kumezwa na siasa chafu za Dar na Dodoma.
Moja ya Sababu kuu mimi kuamua kuandika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, ilikuwa ni "kuhimiza mageuzi ya idara ya Usalama Tanzania na mfumo mzima wa ulinzi na Usalama nchini".
Nilifanya hivyo baada ya utafiti mkubwa nilioufanya na kujiridhisha kwamba mfumo uliopo hauwezi kulisaidia taifa katika ulimwengu huu mpya zaidi ya kulirudisha nyuma na kudumaza utu na fikra za kijamii huku dunia ikisonga mbele katika mageuzi ya kilimwengu.
Katika kitabu, nimeeleza mageuzi makuu matatu ya muhimu na ya lazima kwa Idara ya Usalama wa Taifa kama tunalitakia mema taifa hili. Mageuzi hayo ni; kwanza yaanze kwenye Sheria iliyounda chombo hiki, pili ni Muundo wa Chombo hiki, na tatu ni Sera ya chombo hiki adhimu kwa uhai wa taifa letu.
Kwa mjibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977 Idara ya Usalama haitajwi moja kwa moja kwenye katiba hii tofauti na majeshi mengine yote ya Nchi. Yaani Katiba ya Tanzania haitambuwi uwepo wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Badala yake Chombo hiki kinatambuliwa na sheria ya Usalama wa Taifa ya 20 January 1997 iliyosainiwa na Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania. Kwa maoni yangu hili ni moja ya makosa, Katiba Mpya inatakiwa kutambua na kuipa nguvu idara/taasisi hii pamoja na kwamba Chombo chochote cha usalama kinachoanzishwa kwa mjibu wa sheria ya Tanzania au katiba ya Tanzania, chombo hicho kitakuwa mali ya Tanzania na kitafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na si vinginevyo.
Katika Kitabu cha Ujasusi nimeainisha mapendekezo yangu kwenye sheria ya Usalama wa Taifa ambayo nafikiri kwasasa sheria hiyo ni lazima ifanyiwe marekebisho ili kuendana na mageuzi ya dunia ya leo, tuko karne ya 21 sio enzi za zamadamu.
Moja ya vifungu katika Sheria ya Usalama wa Taifa iliyosainiwa 20 January 1997 na Rais Hayati Benjamiji W. Mkapa ambavyo ni muhimu sana kufanyiwa marekebisho ni. Mfano, kifungu 14 -(1), (2),(3), (4)-(a) na (b). Kifungu cha 15 -(1),(2), (3) -(a) na (b). Kifungu cha 16-(1) (a)na (b), (2) na (3).
Katika kitabu nimehimiza muundo wa Idara ambao umepitwa na wakati ubadilike, muundo huu unahusu kuanzia uajiri (recruiting) na mengineyo, Mfumo wa chama kimoja wa 1962 ulikuwa ndio mfumo wa uajiri wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, na ndio ulikuwa mfumo wa ajira zingine, ilikuwa huwezi kuingia katika vyombo vya ulinzi na usalama bila kupita TANU YOUTH League/UVCCM.
Hadi ilipofika 1992 ndipo mfumo huo ulianza kutoweka katika sekta zingine, lakini katika vyombo vya dola haukutoweka kabisa, Hivi leo watumishi wa vyombo vya dola wengi walioingia kazini kuanzia 1992 kurudi nyuma hadi 1962, hawa ni makada wa chama cha mapinduzi 100%.
Wengi wao leo ni watu wazima ndio ma RPC, OCD na wakuu wa vitengo mbalimbali katika vyombo vya utumishi na vya dola, Hivyo ukimuona RPC anashangilia ccm ikishinda sio kosa lake bali itikadi kwake imekolea na aliingia jeshini kwa tiketi ya chama na sio professional yake.
Kizazi kilichoingia kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama miaka ya karibuni angalau hiki msingi wa kuingia kwao ni elimu, undugulaizesheni na kuipenda kazi husika, japo ukada bado una nguvu ndani ya vyombo hivyo, kwamba leo unaweza kuona maajabu RPC anastaafu leo na kesho akagombea uenyekiti wa ccm mkoa au Ubunge utajiuliza lini aliuwa mwanachama kama katiba ya ccm inavyotaka awe mwanachama angalau miaka miwili.
Sera ama Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi kwakuwa hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe katika misingi ya Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI).
Hapa ieleweke sana, sina maana biashara na makampuni ya uwekezaji yawe ya vyombo hivyo vya ulinzi, au yawe ya serikali, la hasha, nina maana pana zaidi kwamba ushughulikiaji wa taarifa za biashara na uchumi utiliwe mkazo zaidi kuliko ilivyo sasa taarifa za kisiasa ndizo zenye nguvu ya nchi, Mapendekezo ni TIFF itilie mkazo taarifa za uchumi na biashara zaidi na kuzipa ulinzi shughuli na biashara zote za uwekezaji wa ndani na nje na wawekezaji wake. Hawa waitwe rasmi kuwa ni (asset).
Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe.
Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi hasa vijana.
Kwa undani zaidi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi popote ulipo duniani.
View attachment 2468554
Hakuna sehemu nimesema tufute wizara ya fedha au jeshi tubaki na TISS. Wala hakuna sehemu nimesema China iliendelea kwa kuiba teknolojia pekee. Kwani terabytes za data za F-35 walizochukua China zilikuwa za kutengeneza online game? Au blueprint ya atomic bomb waliyochukua USSR haikusaidia.China waliendelea kwa mageuzi makubwa ya uchumi wao na uongozi imara. China haijaendelea kwa kuiba teknolojia za Magharibi bali imeanza tabia za wizi wa teknolojia za biasahara baada kupata maendeleo makubwa.
Njia bora ya kupata maendeleo makubwa ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuchochea innovations, ku-retain na kuvutia talents badala ya kufikiria wizi wa teknolojia ambazo hata mkipewa bure kabisa hamtaweza kuzifanyia chochote cha maana.
Kenya inakuwa kituo kikubwa cha teknolojia mbalimbali Africa Mashariki sio kwa sababu ya ujasusi bali kwa sababu ya elimu, sera na mazingira ya biashara yanayovutia innovation na uwekezaji wa teknolojia.
Tindo umeathiriwa sana na propaganda za uvyama mpaka inafikia mahala watu wakijadili mpira wewe unaingiza uvyama, wakijadili mziki wewe unaingiza uvyama, wakijadili mambo mengine ya taifa vilevile unakimbilia kuingiza uvyama.
Kwa aina hii ya maisha unayoishi, usipokuwa makini ipo siku utakuja kujiuwa kisa chama chako kimeshindwa uchaguzi fulani, afu wale walioshindwa kwenye chama chako husika wakiendelea na maisha yao ya kula bata.
Hii inanikumbusha baba yangu mdogo fulani (ambae sasa ashafariki) alitakaga kuchoma nyumba yake mwenyewe na yeye mwenyewe akiwa ndani, kisa team yake ya Simba imefungwa na Yanga miaka ya 90.
Isingekuwa watu kuwahi kuuzima moto na kuvunja mlango ili wamtoe, jamaa angekuwa amewahi kujiuwa kabla ya muda wake wa kufa haujafika. Wakati huo huo viongozi wa team ya Simba na wachezaji wao walikuwa wanaendelea na maisha yao ya kula bata bila kujali kufungwa kwao.
Hili ninalokwambia ulitafakari, bila hivyo kwa aina hii ya wanasiasa wetu wa bongo waliojaa janja janja ya kupiga pesa za umma, au kulamba asali ili kujiandalia maisha yao na ya vizazi vyao kuna siku utakuja kuumia, au kupata ugonjwa wa moyo ambao haukuwa nao before.
Lazima ujue kuna maisha nje ya siasa na mtu ukaishi vizuri tu bila presha wala shutuma kwa mtu mungine.
Na wabongo wanavyopenda nafasi hiyo ya utiss, kila mtu utasikia mm tissHauogopi kumsema bosi wako mkuu? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Maana kuna watu walikuwa wanakuzushia eti wewe ni mtumishi wa umma kabisa.
Sawa, ni wazi TISS wanakazi kubwa sana, kwamba wanapaswa kujua kama IQ ya mtanzania inapanda au inashuka! Kama hili nalo ni jukumu la tiss, basi naamini mfumo wa elimu ungekuwa ulibadilishwa zamaniKiukweli Bwana Yericko lazima nikupe hongera kwa kuandika kitabu maana kuandika kitabu siyo mchezo. Lakini kwa sababu kitabu chako hukuandika kama matokeo ya utafiti kwa ajili ya taaluma, maelezo yako hayajasanifiwa (hayana peer review ya wataalam wa somo hilo). Kwa hiyo kitabu chako ni kama barua kwa wasomaji. Hii haina ubaya wo wote ila tu usitegemee kitabu kitumike kufanya mabadiliko makubwa.
Kwanza, suala la Usalama, ni suala la utawala. Kwa bahati mbaya sheria hiyo ilipotungwa uwezo unaotokana na uzoefu wa kiutawala katika ngazi za juu sana ulikuwa umeshatutoka. Pili, baada ya Siasa ya Vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, malengo ya kitaifa ya muda mrefu hayapewi kipaumbele na unajua suala la Usalama wa Taifa linahusu mstakabali waTaifa; ni la muda mrefu, si suala la kushinda uchaguzi ujao. Tatu, Usalama wa Taifa unahusu kuwa na mipango, mbinu za muda mrefu za, kulinda, kudumisha na ustawi wa nchi na watu wake. Sasa mambo muhimu hapo ni mengi: mipaka, afya ya jamii, elimu na vipaji vya jamii, sayansi na kuangalia masuala ya sasa yatakavyoathiri Taifa baadaye na kupendekeza mikakati. Nne, utaona hapo kuwa kila nchi usalama wake utatokana na historia ya nchi na taifa lilivyozuka, umakini wa watawala kuhusu mustakabali wa Taifa na uwezekano wa kuwa na uongozi, uendeshaji na zana ambazo ni zaidi ya wastani wa Taifa katika Idara yenyewe. Mwisho, itategemea hao viongozi wa kisiasa wa awamu mbalimbali wamejaliwa vipi katika kuelewa na kutambua masuala haya ya muda mrefu.
Kwa hiyo uchumi ni kipengele kimoja cha kati. IQ ya Mtanzania inashuka au inapanda pengine ndiyo suala la kwanza; na kama haipandi sababu ni nini? lishe, elimu, uongozi au hujuma!?
Umenena !Hakuna mzee mwenye mtazamo tofauti na uliomkuza. Yeye anaamini CCM itatawala milele. Mtu kama huyo hana mtazamo tofauti na huo. Sana sana ataishia kuleta porojo.
Afadhali umempa ufafanuzi kijana wetu, neno Usalama wa Taifa ni Pana sana zaidi ya kushika mabunduki na kulinda viongozi wa CCM .Alichoandika sio kazi kuu ya usalama wa taifa, ila ni kazi mojawapo. Mambo mengine yanafanyika, ulinzi na usalama wanafanya bado ujasusi wa kiuchumi.
Hao unaosema BoT na Finance hawawezi kufanya crandestine operations.
Wasovieti walioiba blueprints za atomic bomb kutoka Los Alamos pale Marekani sio wanasayansi wala watumishi wa jeshi, serikali ya Stalin ingeamua kusubiri jopo la wanasayansi lifanye testing na kila kitu wangetumia gharama kubwa mno na muda mwingi zaidi kupata breakthrough.
Wamarekani walioiba Lunik ya USSR ikiwa kwenye world tour hawakuwa wanasayansi wa NASA, walipiga picha na kukamilisha kazi yao kisha NASA wakatumia hizo taarifa.
Basically TISS isingekuwa na maana kama haitakiwi kufanya kazi fulani maana kila kazi ina wizara. Ulinzi na usalama si zina wizara zake, mambo ya ndani na ile ya ulinzi. TISS kamilifu inatakiwa iweze kusaidia popote pale, hata kampuni ya hapa nchini ikitaka kutengeneza pikipiki ikakwama kutengeneza injini, TISS inabidi iwe na uwezo wa kupata wapi la kupata ujuzi wa kutengeneza injini kwa namna yoyote ile. Ndio vitu duniani wanafanya, China mara nyingi tu unasikia wameiba TB za data kuhusu kitu fulani. Survival of the fittest
Ukisoma stori yote utaelewa ninasema nini? Usisome sentensi ya mwisho peke yake. Usalama wa Taifa unahusu mstabali wa Taifa. Masuala ya siku hata siku ni muhimu kwao kama yanatishia uwepo wa uwepo na ustawi wa mipaka ya nchi na wananchi wake. Kuna taasisi nyingine ambazo zinahusika na masuala ya siku hata siku. IQ hutokana na lishe, hususan protein, kuanzia kabla mtu hajazaliwa kisha huyo mtu kulelewa kwa matunzo ya kiafya, elimu sahihi na uongozi bora. Haya ni masuala ya muda mrefu na ni muhimu kwa Usalama wa Taifa ukisaidiwa na viongozi wa siasa wanakuja kwenye awamu tofauti. Huoni historia na maendeleo ya nchi zenye Usalama wa Taifa unaoeleweka?Sawa, ni wazi TISS wanakazi kubwa sana, kwamba wanapaswa kujua kama IQ ya mtanzania inapanda au inashuka! Kama hili nalo ni jukumu la tiss, basi naamini mfumo wa elimu ungekuwa ulibadilishwa zamani
😂😂😂 Unamkaribisha Putin!Mkuu karibu tena Jukwaani
Asante kwa elimu nzuri,ubarikiwe.Pengine huu ni mwanzo mpya wa mageuzi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mabadiliko haya ya uongozi yana maana kubwa sana kwa Idara yetu, ni matumaini yangu kwamba mabadiliko yatakwenda mbali zaidi kuguza muundo wa idara, mfumo wa idara, sheria na kanuni za idara ili kuendana na ulimwengu mpya wa dunia ya sayansi na teknolojia.
DGIS mpya Ndugu Said Masoro si mtu maarufu katika korido za Ujasusi Dar es Salaam ukimlinganisha na mtangulizi wake Athuman Diwani ambae umaarufu wake ulijengwa akiwa Intelijensia ya Polisi, DCI na katibu Tawala, Masoro anaweza kuwa chachu ya magezi ya chombo hiki muhimu na uti wa mgongo wa taifa letu ikiwa hataruhusu kumezwa na siasa chafu za Dar na Dodoma.
Moja ya Sababu kuu mimi kuamua kuandika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, ilikuwa ni "kuhimiza mageuzi ya idara ya Usalama Tanzania na mfumo mzima wa ulinzi na Usalama nchini".
Nilifanya hivyo baada ya utafiti mkubwa nilioufanya na kujiridhisha kwamba mfumo uliopo hauwezi kulisaidia taifa katika ulimwengu huu mpya zaidi ya kulirudisha nyuma na kudumaza utu na fikra za kijamii huku dunia ikisonga mbele katika mageuzi ya kilimwengu.
Katika kitabu, nimeeleza mageuzi makuu matatu ya muhimu na ya lazima kwa Idara ya Usalama wa Taifa kama tunalitakia mema taifa hili. Mageuzi hayo ni; kwanza yaanze kwenye Sheria iliyounda chombo hiki, pili ni Muundo wa Chombo hiki, na tatu ni Sera ya chombo hiki adhimu kwa uhai wa taifa letu.
Kwa mjibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977 Idara ya Usalama haitajwi moja kwa moja kwenye katiba hii tofauti na majeshi mengine yote ya Nchi. Yaani Katiba ya Tanzania haitambuwi uwepo wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Badala yake Chombo hiki kinatambuliwa na sheria ya Usalama wa Taifa ya 20 January 1997 iliyosainiwa na Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania. Kwa maoni yangu hili ni moja ya makosa, Katiba Mpya inatakiwa kutambua na kuipa nguvu idara/taasisi hii pamoja na kwamba Chombo chochote cha usalama kinachoanzishwa kwa mjibu wa sheria ya Tanzania au katiba ya Tanzania, chombo hicho kitakuwa mali ya Tanzania na kitafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na si vinginevyo.
Katika Kitabu cha Ujasusi nimeainisha mapendekezo yangu kwenye sheria ya Usalama wa Taifa ambayo nafikiri kwasasa sheria hiyo ni lazima ifanyiwe marekebisho ili kuendana na mageuzi ya dunia ya leo, tuko karne ya 21 sio enzi za zamadamu.
Moja ya vifungu katika Sheria ya Usalama wa Taifa iliyosainiwa 20 January 1997 na Rais Hayati Benjamiji W. Mkapa ambavyo ni muhimu sana kufanyiwa marekebisho ni. Mfano, kifungu 14 -(1), (2),(3), (4)-(a) na (b). Kifungu cha 15 -(1),(2), (3) -(a) na (b). Kifungu cha 16-(1) (a)na (b), (2) na (3).
Katika kitabu nimehimiza muundo wa Idara ambao umepitwa na wakati ubadilike, muundo huu unahusu kuanzia uajiri (recruiting) na mengineyo, Mfumo wa chama kimoja wa 1962 ulikuwa ndio mfumo wa uajiri wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, na ndio ulikuwa mfumo wa ajira zingine, ilikuwa huwezi kuingia katika vyombo vya ulinzi na usalama bila kupita TANU YOUTH League/UVCCM.
Hadi ilipofika 1992 ndipo mfumo huo ulianza kutoweka katika sekta zingine, lakini katika vyombo vya dola haukutoweka kabisa, Hivi leo watumishi wa vyombo vya dola wengi walioingia kazini kuanzia 1992 kurudi nyuma hadi 1962, hawa ni makada wa chama cha mapinduzi 100%.
Wengi wao leo ni watu wazima ndio ma RPC, OCD na wakuu wa vitengo mbalimbali katika vyombo vya utumishi na vya dola, Hivyo ukimuona RPC anashangilia ccm ikishinda sio kosa lake bali itikadi kwake imekolea na aliingia jeshini kwa tiketi ya chama na sio professional yake.
Kizazi kilichoingia kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama miaka ya karibuni angalau hiki msingi wa kuingia kwao ni elimu, undugulaizesheni na kuipenda kazi husika, japo ukada bado una nguvu ndani ya vyombo hivyo, kwamba leo unaweza kuona maajabu RPC anastaafu leo na kesho akagombea uenyekiti wa ccm mkoa au Ubunge utajiuliza lini aliuwa mwanachama kama katiba ya ccm inavyotaka awe mwanachama angalau miaka miwili.
Sera ama Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi kwakuwa hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe katika misingi ya Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI).
Hapa ieleweke sana, sina maana biashara na makampuni ya uwekezaji yawe ya vyombo hivyo vya ulinzi, au yawe ya serikali, la hasha, nina maana pana zaidi kwamba ushughulikiaji wa taarifa za biashara na uchumi utiliwe mkazo zaidi kuliko ilivyo sasa taarifa za kisiasa ndizo zenye nguvu ya nchi, Mapendekezo ni TIFF itilie mkazo taarifa za uchumi na biashara zaidi na kuzipa ulinzi shughuli na biashara zote za uwekezaji wa ndani na nje na wawekezaji wake. Hawa waitwe rasmi kuwa ni (asset).
Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe.
Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi hasa vijana.
Kwa undani zaidi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi popote ulipo duniani.
View attachment 2468554
Ninachokipinga kwa nguvu zote ni hiki;Hakuna sehemu nimesema tufute wizara ya fedha au jeshi tubaki na TISS. Wala hakuna sehemu nimesema China iliendelea kwa kuiba teknolojia pekee. Kwani terabytes za data za F-35 walizochukua China zilikuwa za kutengeneza online game? Au blueprint ya atomic bomb waliyochukua USSR haikusaidia.
Hayo mageuzi makubwa ya uchumi unayosema ya China kwani hayana nyenzo na mbinu tofauti au kuna kitu kimoja fixed kinaitwa mageuzi ya uchumi.
Nimekuuliza swali quote ya mwanzo, kama hutaki TISS ihusike kiuchumi kwanini unataka ihusike kiusalama na kiulinzi wakati tuna Wizara ya Ulinzi na tuna Wizara ya Mambo ya Ndani, ambazo zote hizo haziisimamii TISS. Unamaanisha tuifute
Wewe jamaa mbishi wa asili yaonekana,ujasusi unafanyika popote pale iwe mambo ya uchumi,kijamii ama kisiasa,taarifa yoyote inayopatikana kupitia hizo sehemu na ikachakatwa tayari kwa matumizi huo tayari ni ujasusi.Yapo Mashirika makubwa Duniani binafsi yanafanya ujasusi wa kiuchumi kwa wawekezaji na nchi kwa ujumla hivyo hivyo Serikali kupitia vyombo vyake vya ujasusi wanafanya.Nchi ikitaka kuwa kinara wa korosho, chai, tumbaku au bidhaa nyingine yoyote katika masoko ya nchi nyingine kinachotakiwa ni kuzalisha na kufikisha bidhaa bora zinazokidhi hayo masoko kwa gharama za chini kuliko wazalishaji wengine, sera nzuri za biashara na kodi ambazo zina support biashara za kimataifa na mahusiano mazuri ya kidiplomasia kati ya nchi. Huhitaji TISS au chombo cha ujasusi kufanikisha haya, ni mambo basics kabisa. Labda kama taifa linataka kupora uranium au mafuta kutoka taifa lingine au kuuza silaha ndio litahitaji majasusi rogue wanaofadhiliwa na corporations katika uhalifu huo.
Mashirika ya kijasusi ya Nchi yapo yanayomiliki Makampuni na Taasisi nyingine za kibiashara ila kupitia hayo Makampuni ndiyo shughuli za ujasusi hufanyika,kubali kupata elimu utajifunza zaidi.Kwa kifupi elewa hivi Kazi kuu ya ujasusi ni kusaidiq kuweka mazingira salama ya raia kufanya maisha yao kwa ufanisi, iwe biashara au jambo lingine lolote, sio kazi ya taasisi za ujasusi kutuoa muelekeo wa uchumi, kuelekeza au kuingilia jinsi uchumi wa nchi unavyopaswa kwenda. Hii ni kazi ya wanasiasa viongozi na watunga sera.
Kufikiria kwamba taasisi ya ujasusi inaweza kuwa mwarobaini katika kuukwamua uchumi wa nchi ndio kituko kikubwa zaidi.
Zipo models nyingi za maendeleo duniani ila hakuna hata model moja ya maendeleo ya uchumi kutokana na nguvu ya spy agency.
Uko sahihi hapa sasa ndiyo uone dhana pana ya kitu kinaitwa ujasusi,Hao Polisi wana Bureau of Criminal Intelligence(Imewahi kuongozwa na Aliyekuwa DGIS) wana madawati tofauti moja wapo ni la uchumi,lakini pia Ofisi ya CAG Polisi ni wengi wote hawa wapo kufanya shughuli za kijasusi katika milengo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa.Hata Polisi wana cover almost sector zote.
Mkuu unaona ni gazeti kwa vile comment imehusisha watu wawili. Wewe wa Chadema na yule wa Simba 😂😂😂Bro hili gazeti lote ni langu kwa kale kaparagraph kamoja?
Kwenye amani na utulivu wamefanikiwa lakini uchumi na umahiri katika ujuzi wa mambo ya maendeleo, daah tunahitaji namna nyingineHii idara ni nyeti mno.
Imebeba mambo Mawili UMASIKINI WA NCHI AU UTAJIRI WA NCHI.
KAZI KWENU TISS AMKENI.