Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Acheni majungu ya kuhadithiwa.
Kama mtoa mada ni mkweli na si mnafiki
ELEZA hapa hapa jamvini, uhuni na ubadhirifu ulionfanywa na Mchechu.
Nafikiri reverse Chatonaisation ndio inawasumbua.
 
Tangu Mchechu aoundolewe NHC, miradi yote ilisimama. Kama alikuwa mbovu, mbona yule aliyeteuliwa baada yake hakuweza hata kukamilisha miradi ya NHC? Kwa uteuzi huu, angalau miradi ya mabilioni ya walipa kodi iliyosimama itakamilishwa.
 
Alituaamunisha hivyo hakuwa sahihi. Asante mama Kwa kuliona Hilo. Ponya maumivu ya watu ktk mioyo Yao.
 
Ili uonekane kwamba wewe ni mtu OBJECTIVE. Ungetwambia hapa ubadhilifu wa msechu . Kama alikuwa mchafu kwann hajapelekwa mahakamani???
 
awamu ya mafisadi
JPM alijenga uwanja wa ndege kwao bila kufua sheria ya manunuzi
Alipora korosho za watu.
Aliua watu
Alinunua ndege bila kufuata sheria yyte ya manunuzi
Huu siyo ufisadi????
Kamfufueni
 
Watu wale wale, miaka nenda rudi utafikiri hii nchi Mchechu, Mafuru, Makamba, Nape nk ndio wasomi pekee na wenye akili pekee.

Huyu mama sijui hata anawaza nini
Hao washajiona wao ndio wanastahili kuteuliwa kushika nafasi kubwa kubwa serikalini ndio maana wanadharau

Magufuli atakumbukwa sana.
 
Tuliambiwa alianza biashara na shirika analoliongoza. Akaanza mambo ya viwanja. Kwa sifa hizo, kwa sasa tulistahili kuelezwa nini ilikuwa uongo au nini kimebadirika. Bila maelezo, ninachokiona. Kama kweli ni suala la urafiki wa Kikwete na Samia, basi hakuna sababu ya kuwa na rais mpya. Tunaomba arudishwe kikwete kuwa rais. Hii ya kuwa na Samia akiongozwa na Kikwete ni kuharibu kabisa mfumo wa uongozi.
 
Uchungu wa wivu wa kike.Wamewekwa Ma Dr wamefanya nini serous kwa miaka mitano kinachoonekana?.Tatizo ni kuendeleza fikra za marehemu kulazimisha kila alichokataa yeye (bila sababu) na wote tufuate mkumbo tu.Mama amekataa hayo.Mchechu ni genius na kama angekuwa mwizi kama mbavyodai Mwendazake angehakikisha anafia jela.
 
Mbona zote zimeisha kununuliwa ?.
 
Nashauri tunapokuwa tunaleta objections za vitu/mtu/watu walau tuwe na orodha za vinavyofaa/anayefaa/wanaofaa,hii itasaidia sana.
Kwa kuanzia pengine sisi /JF ianzishe Forum ya CVs /Profiles/ au vyovyote vile ili kusaidia jamii kupata huduma ya nguvukazi/maarifa/ajira/rejea.nk

Binafsi sioni tatizo la uteuzi, tatizo naliona kwa watu kutofahamu umuhimu /maana/dhima ya NHC.

Badala ya kulaumu ni bora pengine tungelishauri Serikali kuwa na chombo kimoja kinachojihusisha na Majenzi.
 


Tatizo ni vijana wetu wengi wanasubiri kazi serikalini badala ya kufanya biashara. Biashara ya kilimo inalipa ukijipanga lakini vijana wana kaa mijini na ku follow Diamond na Zuchu! Sasa ni wivu tu ! Fanyeni biashara mpate pesa🤔
 


Addict wote huwa wanapelekwa rehab…hawawekwi kwenye mazingira yaleyale yaliosababisha…
 
Kurudishwa Msechu NHC ni mkakati wa Kikwete kutaka kukomba hayo mabillioni yaliyopelekwa huko!! Anaandaa mtandao wa Uchaguzi wa 2024 hivyo sehemu zote zenye fedha atateuliwa mtu atakaye wezesha upatikanaji wa fedha za Uchaguzi!!
Mkuu acha kumzushia mstaafu uongo.
 
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.

Nikwambie kitu mkuu…kwa jinsi hali ilivyo mimi ninavyoona katiba sio suluhu…km kiongozi kahusishwa na ufisadi…kashfa zote yumo…lakini bado anateuliwa na system za kiusalama zote zipo…what makes you think katiba itafuatwa na system ile ile…

Hv unafikiria Nyerere angekuwepo huu upuuzi ungeusikia…kwa kifupi kichaa kapewa rungu….watu wana exercise power at the expense ya maendeleo ya nchi …sasa watanzania akili kichwani it’s unfortunate elimu duni ndio mtaji wa watawala…ninaamini itakula kwetu mpaka atokee mkombozi ambae ataweka misingi imara tena…na atatengeneza system ya maana…sio kwa miaka 10…lazima huyo mwamba ashike nchi not less than 20yrs…ndio tutasogea…naamini mapinduzi ya kweli sio lelemama huwa yanafanywa na the very powerful leader ambae anaipenda nchi kuliko pesa…bila hivyo na chama hichi hata chochote kile cha upinzani na drama wanazotuchezea kila siku km mapunguwani hatutoboi….
 
Hao washajiona wao ndio wanastahili kuteuliwa kushika nafasi kubwa kubwa serikalini ndio maana wanadharau

Magufuli atakumbukwa sana.
Kwenye uteuzi hata yeye alikuwa na nepotism ya hali ya juu. Two wrongs never make a right...Mimi kinachonisikitisha ni mambo kufanyika bila aibu na hadharani, hii inatisha sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…