Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

mtu aliyefanya aibu zote HIZO ikiwa ni pamoja mauaji ya vifaranga visivyo na hatia. Nashauri kumbukizi yake ya mwaka mmoja iwe na slogan ya UKOMBOZI KUTOKA KWENYE AIBU
Never Never Again itafaa sana
 
Kuna ujinga gani hapo sasa, kaangalie apartment za kule morocco kama kuna watu wanakaa na wakutajie bei yake....
Watakaaje wakati zilisimamishwa uendelezaji wake?.Nadhani kuna watu humu wanazungumza tu kwa sababu hawalipii
 
aliyepo na anaowaleta wote wana lao moja, wanataka kuifanya nchi hii yakwao na wajukuu zao!.
 
Kwani kutofikishwa mahakamani ndio kusema hakukuwa na tatizo mahala?!
Marehemu, mambo yake mengi alikuwa anafanya bila weledi. Anawasikiliza wambeya akiwa kwenye mkutano, hajachunguza, hajampa nafasi ya kujitetea anayepigiwa majungu, anatamgaza hapo hapo kuwa anamtumbua. Yote ilikiwa kutafuta sifa toka kwa wajinga wa kumpigia makofi kwa kila jambo, hata kama ni haramu.

NHC, chini ya uongozi wa Msechu, lilitangazwa kuwa shirika la nyumba, bora kuliko mashirika yote ya nyumba barani Africa.

Tuukubali ukweli kuwa awamu ya 5, ulikuwa utawala primitive uliokiwa umekosa upeo na dira.
 
Hakuna laana kubwa kwa taifa hili kupata wazazi waliotuletea watoto laana sampuli ya wewe Bams
Mimi sina laana maana sijawahi kuteka mtu, sijawahi kumtesa mtu, sijawahi kumbambikia kesi mtu, sijawahi kumnyima uhuru mtu yeyote, wala sijawahi kumjeruhi mtu hata kwa fimbo, achilia mbali kwa risasi 16 kama walivyofanya wale baradhuli waishio chini ya laana kuu.
 
Walivyoondolewa ulipewa sababu? Uliona wakipelekwa Mahakamani?

Kwa nini useme Rais ana udhaifu?

Kwa taarifa yako Samia haongozwi na chuki
SSH hana nongwa. Marais wetu wakristo wanafundishwa maana ya upendo lakini wanashindwa kuuweka kivitendo katika uongozi wao.

Unabaki kushangaa Mwinyi na Kikwete wanazeeka wakiwa na tabasamu usoni tena lile halisi sio la kulazimisha, ni moyo wa upendo na kusamehe walionao.

Ukiwa mtunza hasira lazima siku zako za kuishi ziwe chache, ni lazima utauharibu moyo na afya yako kwa ujumla itaharibika.
 
Rais Samia anatengeneza Serikali ya kistaarabu. Anajaribu kuondoa utawala primitive wa Marehemu Magufuli.

Muda si mrefu, mambo yataanza kubadilika taratibu. Marehemu aliua uchumi, aliua demokrasia, aliua ustaarabu, aliua mifumo ya utawala. Kwa kweli uongozi wa marehemu, kama alivyosema yule gavana wa Kenya, ulikuwa ni aibu kwa Watanzania na Afrika nzima.

Tuliombee Taifa letu, ili taifa lisijekupatwa na laana kama ile ya wakati wa utawala wa Marehemu, utawala ulioishia kuteka watu, kupoteza watu, kuua watu, kubambikia kesi watu, kuharibu mahusiano ya kimataifa, kushusha ukuuaji wa utalii toka 15% mpaka 3.6%, kushusha ukiaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%, kuangusha thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo kwa 50%.

Kwa kweli uongozi wa marehemu ulikuwa ni laana kwa Taifa, hasara kwa Watanzania. Tuzidi kumwombea maana hatujui ndani ya roho yake kulikuwa na nini hata mtu akapenda uovu dhidi ya binadamu wenzake kwa kiasi kile.
We jamaa bana na vihadithi vyako vya chuki visivyoisha kwa JPM kila ukitinga JF! Huwezi kuandika sentensi bila chuki, matusi kwa JPM!

Kuna kiwango cha chuki usipokidhibiti ni kuelekea wewe mwenyewe kubeba dhambi bure wakati unayeshughulika nae hawezi kukujibu na tayari yupo kwenye kiti cha hukumu.

Huyo mwendazake hayupo tena na sasa tulio hai ndio tutapimwa kwa moto matokeo ya kazi zetu.
 
Kwani kutofikishwa mahakamani ndio kusema hakukuwa na tatizo mahala?!
Hakukuwa na matatizo yeyote na MCHECHU. Magufuli alikuwa hapendi watu wenye fedha, mafanikio au akili kuliko yeye
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
Si mlisema anaupiga mwingi. Subirini wenye chama chao waneemeke.
 
We jamaa bana na vihadithi vyako vya chuki visivyoisha kwa JPM kila ukitinga JF! Huwezi kuandika sentensi bila chuki, matusi kwa JPM!

Kuna kiwango cha chuki usipokidhibiti ni kuelekea wewe mwenyewe kubeba dhambi bure wakati unayeshughulika nae hawezi kukujibu na tayari yupo kwenye kiti cha hukumu.

Huyo mwendazake hayupo tena na sasa tulio hai ndio tutapimwa kwa moto matokeo ya kazi zetu.
Marehem aliishi maisha ya chuki na visasi sana,,acha apewe za uso hukohuko aliko.
 
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.
tusadie pia kujua katiba mpya itafanya nn kuhusu hili???
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
Mimi ninampongeza sana mama kwa kumrudisha Mchechu NHIC..mlifanyia fitina atoke Ila Sasa amerudi...kazi iendelee.shirika lilikuwa linaelekea shimoni..Ila Sasa Kama ni upele umepata mkunaji..
 
Nijibu swali hili: Je, Mchechu alifunguliwa mashtaka ya Ubadhilifu wa mali/pesa za umma?
Kama hajafunguliwa basi wewe ni maiti na ndondocha nambari 1, maana uliiona Ubadhilifu wa mali za umma ukifanyika na ulikaa kimya hukwenda mahakamani wala kwenda polisi kutoa taarifa.
Una haki kama mwananchi kuzilinda mali za umma kwa namna yoyote na si kuja kulalamika mitandaoni
 
Mtandoa wa wizi unarudishwa kwa kasi. Ule mtandao wa Jk wa upigaji unarudishwa wote. Ingekuwa kenya wasingenyamaza,lakini kwa hapa kwetu tutaishia mitandaoni
 
Nijibu swali hili: Je, Mchechu alifunguliwa mashtaka ya Ubadhilifu wa mali/pesa za umma?
Kama hajafunguliwa basi wewe ni maiti na ndondocha nambari 1, maana uliiona Ubadhilifu wa mali za umma ukifanyika na ulikaa kimya hukwenda mahakamani wala kwenda polisi kutoa taarifa.
Una haki kama mwananchi kuzilinda mali za umma kwa namna yoyote na si kuja kulalamika mitandaoni
Mnajikanyaga tu il-hali mnajua kabisa watu hawawezi kwenda polisi wala mahakamani. Ksbb huko hakuna haki tena. Bali mwenye nacho ndio anapewa haki
 
Back
Top Bottom