Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Hili ni kosa tuu la photo misplacement ni kosa la kawaida sana kwenye printing ila hilo ni tangazo moja la mtu mmoja yule yule walichanganya picha, wakarekebisha na kurudiwa kutangazwa.

Pasco


si sahihi. Hii ni mtu kacheza na photoshop tu. wala gazeti halina makosa hapo!

angalia namba iliyopo kulia chini ndipo utagundua. Kama gazeti wangerudia basi nafasi hiyo ingekuwa na namba mpya!
 
Chabruma na Kigwa please, jitokezeni hapa kujibu tuhuma zinazowakabili. Pongezi kwake Mh. Lameck Madelu Mkumbo kwa ufafanuzi wake.
 
ok, kumbe ndio hivyo....na watu mnajua kwanini hamkusema
 
Mfano baba anaitwa john shija masalakolangwa
Mtoto ni lazima aitwe
Emanuel john masalakolangwa,jina la mtoto laweza kubadilika lakini la baba na ukoo ubaki palepale,sasa ikitokea mtoto akaitwa peter samwel nyakukungu hapo kuna walakini
 
Majina yake Ni ya kisukuma Ila yeye si msukuma au nakosea?- tafakari
Mkuu Gigo, unataka watu tutafakari nini wakati mwenyewe kasema hayo majina ni given names tuu na dakitari, angeweza hata kuitwa Joginder Sing na bado hakuna kosa lolote!.

Pasco
 
Dhana ya kwamba atang'oka kwa hii issue haitowezekana. Nadhani tuendelee na maisha yetu tu maana hata yule Diamond siyo jina lake halisi lakini sisikii mtu akiuliza
Kwani ana vyeti vilivyoandikwa jina la Diamond?. Kifupi bwana mheshimiwa alizaliwa akaitwa Lameck na wazazi wake na akasomea jina hilo mpaka alipofeli darasa la saba kilichofuata alirudia au aliiba nafasi ya Mwigulu Nchemba hilo liko wazi sasa mengine yaliyobaki ni story tu. Kama si kosa kisheria aungame yaishe na watu waliopita njia kama zake waachwe maana mtafukua mengi.
 
Kuna muvi moja inaitwa three idiot inaeleza vya kutosha,mwenye jina akijitojeza kuanza kudai jamaaa ana vyake,ndio maana serikali kabla hujafanya mtihani wa kidato cha pili kma ulikuwa unatumia jina la mtu huwa wanapewa fursa ya kubadili majina
 
Mfano baba anaitwa john shija masalakolangwa
Mtoto ni lazima aitwe
Emanuel john masalakolangwa,jina la mtoto laweza kubadilika lakini la baba na ukoo ubaki palepale,sasa ikitokea mtoto akaitwa peter samwel nyakukungu hapo kuna walakini
Mkuu Lazaro, hakuna walakini yoyote as long as huyo baba john shija masalakolangwa, jina hili ndilo lililoko kwenye cheti cha kuzaliwa kama baba wa mtoto, pia ndilo lililopo kwenye vyeti vya kuandikishwa shule, vyeti vya NIDA na Uhamiaji, vikieleza majina ya mtoto ni peter samwel nyakukungu, majina hayo hayana tatizo kabisa popote kwa sababu tangu shule , uhamiaji na NIDA, majina yatakayoonekana ni peter samwel nyakukungu Emanuel john masalakolangwa. Hakuna mwisho wa idadi ya given names, ndio maana namtetea Mhe. Mwigulu kwa haki kwa vile hakuna anayejua birth certicate yake na DN number yake ina majina gani.

Pasco
 
Mwigulu alifeli darasa la 7 akatumia cheti cha mtu aliefaulu darasa la 7 kujiendeleza. Kwahiyo ana cheti bandia na majina bandia.
Pasco anajichanganya tu hivi jamaa kabla ya kuacha shule na kwenda kuchunga alikuwa anaitwa nani?na kwanini alibadili jina ,mimi ninachokiamini huenda jamaa baada ya kurudi shule alichukua jina la mtu kama sio cheti,na hiyo ni kawaida kwa sie tuliosoma kijijini watu hawataki shule wanaenda kuchunga,kwa mfano mimi nimechukua cheti cha mtu cha kidato cha nne nikajiendeleza nikafika mpaka PhD, cheti cha kidato cha sita,digrii,digrii ya uzamili,digrii ya uzamivu vyote vyangu isipokuwa cheti cha kidato cha nne na jina sio vyangu, je hapo nimeghushi au sijaghushi?
 
Mkuu Maseni, asante kwa somo hili
Pasco
 
MWIGULU katia aibu, kumbe na mbwembwe zote hizo alichukua jina la mtu aliefaulu hili alitumie yeye?, aibuu
 
Sasa mtu anaruhusiwa kutumia majina ya bandia kigombea urais wa nchi? Maana Pasco ameeleza vizuri kabisa kuwa majina ya Mwigulu Nchemba ni ya bandia (fake), lakini huyu mwenye haya majina bandia aligombea urais akitumia majina hayo hayo fake? Jee lilikuwa ni kosa kisheria?
 

Mkuu maelezo yako mazuri lakini nadhani Tanzania hatuna "Surname System", kwamba ni lazima kuwe na jina la ukoo tena lisiwe la kizungu. Jamii ya Tanzania tuko Waislam, Wakristo na wenye imani zingine. Kwa Waislam mtoto anatakiwa aitwe kwa jina lake na la ubini wake yani baba yake. Kwa hiyo wasemapo jina kamili huwa ni majina matatu yani la mtoto, likifuatiwa na la baba yake nalo likifuatiwa na la baba yake (ambaye ni babu wa mtoto). Majina haya si lazima yawe ya kilugha. Yanaweza kuwa Ali Juma Omari au Fatuma Jumbe Zuberi n.k. Na inaonekana hata jamii ya Wakristo hutumia mfumo huo ingawa kwa ufuatiliaji wangu inaonekana kwa Wakristo ndiko hasa kwenye majina ya Kilugha baada ya yale ya awali na kati ambayo huwa ya kizungu kama Frank John Mnyalukolo, Steven George Mwakatange n.k.
 
Sheria inaruhusu kubadiri jina so hili la majina nadhani aachiwe mwenye maana hata mi Leo nikipenda Nina naadaa deed poll naanza kuyatumia.
 
Mkuu Samari, alichoeleza humu Mwigulu ndio ukweli wake, usitake kumlisha maneno kwa kulazimishwa ukweli unaotuka wewe!, kuna kweli za aina tatu,
1. Ukweli unaosemwa kuwa ni kweli -spoken truth
2. Ukweli unaotakiwa kuwa ni ukweli-the purported truth
3. Ukweli halisi - the real and plain truth.

Kati ya kweli hizi, ni ukweli halisi tuu ndio utasimama mpaka mwisho, ukweli unaosemwa kuwa ni kweli unaweza kuwa ni uongo unasemwa na kuitwa ni kweli, ukweli unaotakiwa ni ule ukweli unaohitajika, ili uwe ukweli mfano miongini mwa sifa za rais, lazima awe ni Mtanzania, akitokea kijana wa banyamulenge kule mipakani, na anautaka urais, na akaupata, then hata ukweli ukiibua kuwa sio Mtanzania, ukweli unaotakiwa kuwa ni kusemwa ni Mtanzania.

Pasco
 
kama nakuelewa, ishu ni kua mwigulu alifaulu la 7 then hakufaulu kwa jina la mwigulu ila lingine ambalo ndilo analitumuia hadi leo kwenye vyeti, ila hilo mwigulu alipewaga tuu kama nick names
Mkuu Kibao cha Kaburi, alipozaliwa alipewa majina ya kwao unyirambani, alipopelekwa hospitali, dakitari wa Kisukuma akamuuliza mama yake kama ana majina mengine yoyote, mama akasema hana, mama akamruhusu dakitari ampe yeye majina anayotaka, kwani majina ni nini, ndipo dakitari huyo akampa majina hayo na ndio aliandikishwa nayo shule na kuendelea kuyatumia mpaka leo.
Japo ni very interesting!.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…